Wana JF,
Ujumbe huu uende kwa Rais Samia pamoja na TRA.
Huu mfumo mpya ambao TRA imeuanzisha katika kukusanya VAT umeleta matatizo makubwa sana hasa kwa kampuni za wilayani na mikoani.
Kawaida VAT huwa hivi. Mfanyabiashara unaauza bidhaa yako au huduma yako na kuongeza VAT juu ambayo mlaji huibeba. VAT haitakiwi kuwa mzigo kwa muuzaji bali mnunuzi wa huduma.
Sasa kinachotokea TZ hasa kwa kampuni kubwa zilizoko wilayani ni kwamba
1. Ukiwa VAT registered unaweza kuwa na ushindani na makampuni mengine ambayo sio VAT registered. Kwahiyo ukiongeza VAT kwenye bidhaa yako, inakula kwako kwasababu huduma yako itakuwa aghali zaidi. Hili linatokea sana kwa biashara kubwa huko wilayani. Kwahiyo hawaongezi VAT kwenye mauzo yao na badala yake wanatoa VAT kwenye faida zao. Mfano mauzo ya milioni 50 kwa mwezi, VAT yake ni milioni 9.
2. Inatakiwa utoe VAT ya manunuzi yote unayofanya katika kutengeneza mauzo yako. Bahati mbaya wilayani wafanyabiashara ambao ni VAT registered ni wachache sana. Kwahiyo unajikuta huna receipts kabisa za manunuzi yenye VAT. Kwenye expenses zako VAT ni zero
Huko nyuma mfanyabiashara alikuwa anaruhusiwa kuingiza VAT ya baadhi ya matumizi yake. Lakini sasa wamebana, kama huna receipt imekula kwako. Maana yake katika hayo mauzo ya milioni 50 ni kama wewe hujaweka matumizi yoyote. Yaani umezalisha milioni 50 bila ku invest hata senti tano.
Kwahiyo ikifika tarehe 20 mwezi unaofuata inabidi ulipe hiyo milioni 9 ya VAT. Na of course utakuwa hauna maana huenda hata fida tu ya biashara yako haifiki hiyo figure.
3. Unaweza kuta hao uliowauzia huduma yako hawalipi ontime. Kama sisi wengine hata sasa tunadai madeni ya October 2022. Sasa TRA wanataka VAT yao hapo hapo. Kwahiyo unatakiwa kulipa hiyo milioni 9 ambayo hujapokea malipo yake.
Matokeo ya hizo points tatu ni kufilisika. Yaakiendelea hayo mimi mimi miezi mitatu inayokuja huenda ikabidi kufunga biashara na kuondoa wafanyakazi kama 30. Kwasasa ni stress tu na kutoa pesa zangu zingine ili kulipa hizo VAT. Mwisho wa siku kila mwezi ni hasara tu.
Kwa mfano huko nyuma nilikuwa nalipa wastani wa VAT milioni moja kwa mwezi. Miezi miwili ya mwaka huu nimelipa average kwa mwezi milioni 9.
Wanavyofanya nchi zingine, mfanyabiashara anachagua kulipa VAT flat rate kwa mfano katika VAT uliyokusanya unalipa 25% na hakuna mambo ya kudai VAT ya matumizi au unadai VAT ya matumizi. Mfanyabiashara anachagua njia ambayo ni nafuu kwake.
Kwa TZ huu mfumo mpya wa kulazimisha unaenda kuua biashara zetu. Hivi hata kwa akili ndogo kweli kwenye biashara ya kama hoteli, unaweza kuzalisha mauzo ya milioni 50 bila kuwa na matumizi yoyote ya maana? Ina maana watu wanafanya manunuzi ila ni kwenye maduka ambayo sio VAT registered. Biashara kama ya hoteli faida haizidi asilimia 20. Sasa VAT pekee ikichukua asilimia 18, kuna biashara tena hapo?
Ukiwa Dar au miji mikubwa ni rahisi kununua kila kitu kutoka maduka ambayo ni VAT registered. Lakini wilaya kama kule Ngara huna luxury hiyo.
Wahusika chukueni hatua.