Vampire | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vampire

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by TONGONI, Aug 7, 2011.

 1. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Msaada wana JF nini kiswahili cha neno hili...VAMPIRE
   
 2. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,664
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  mhh! sijui

  labda neno MSUKULE linaweza lika fit
   
 3. Humphnicky

  Humphnicky JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 1, 2010
  Messages: 1,809
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  kizuka
   
 4. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  KIzuka si neno sahihi kwa sababu KIZUKA: ni mfiwa na mume...(MJANE)
  Isipokuwa neno Mzuka linakaribiana na maana ya VAMPIRE kwa sababu MZUKA =GHOST
   
 5. SaidAlly

  SaidAlly JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 1,689
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />

  Sema la kwako sasa, sio kusahihisha tu ya wenzio. Tunasubiria!
   
 6. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  MSUKULE inaendeana lakini bado inatuacha na walakini kwa sababu tukiichambua mbeleni inaachana ki-maana.
  MSUKULE wanao amini ni kuwa anachukuliwa mtu kimazingara watu wakiamini amekufa lakini hao wanao daiwa kuwa na hiyo taaluma wanakuchukua kwenda kukufanyisha kazi,na mambo mengine wanayo yajua wao.
   
 7. enhe

  enhe JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 894
  Likes Received: 310
  Trophy Points: 80
  "Mumiani" ndio maana sahihi,kama mnakumbuka enzi za nyonya damu!
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,664
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  lakini wale muminiani si walikuwa ni watu..? i mean binaadamu kama sisi...
   
 9. GABOO

  GABOO Senior Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi mavampaya TZ wapo?
   
 10. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #10
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  ujinga sio sifa ila ni kashfa mimi ndio nimeleta hili hapa na nia yangu ya dhati ni kujifunza na wala si kushindana,najaribu kuchangia mawazo na wachangiaji,mbona kama umekurupuka toka usingizini,unaropoka tu!...siku hizi wana maeno wanasema umeshindwa kunisoma!!
   
 11. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #11
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa kumbukumbu zangu MUMIANI ilikuwa ni uvumi kuwa kuna watu wakikukamata wanakunyonya damu.na tulikuwa tunawakimbia wazungu enzi za mashamba ya mkonge.
   
 12. TONGONI

  TONGONI JF-Expert Member

  #12
  Aug 7, 2011
  Joined: Feb 18, 2011
  Messages: 1,024
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwa Tanzania sina hakika lakini nikijibu kilimwengu,miaka ya 1730 imani hii ilikuwepo sana Ulaya ya Mashaririki,hasa hasa sehemu za Hungary.
   
Loading...