Companero
Platinum Member
- Jul 12, 2008
- 5,609
- 1,738
Ni kweli. Kuwa uzuri wa ndani ni muhimu sana. Lakini tusidanganywe. Wala tusijidanganye. Eti kuwa uzuri wa nje si muhimu. Tena tusidanganyike eti kuwa uzuri wa nje unachuja na kuchakaa. Ukiupenda, ukauzoea - utadumu.
Hata kina Adamu na Abrahamu wa kwenye misahafu walikuwa na wenzi wenye uzuri wa nje. Tena Abrahamu mpaka akaogopa na kudai kuwa ni dada tu. Isaka alipata mwenye haiba ya ndani na nje naye akaishia kudai ni dada yake.
Ukipenda moyo wake penda na macho yake. Penda akili zake na wajihi wake pia. Ndio, mpende ndani na nje.