Uzuiaji wa pombe ya viroba: Wamiliki wa viwanda kupata hasara

MZK

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
236
306
Hatimae ule muda wa kusimamisha uuzaji wa pombe ya viroba Nchini Tanzania umefika, huku Viwanda na Wauzaji wakiwa na shehena kubwa ya Pombe hio. Hili limethibitika leo wakati Mamlaka husika zilipofanya kazi ya kutembelea viwanda na wauzaji kuona utekelezaji wa agizo hilo. Kilichopatikana ni shehena kubwa sana ya pombe hio ikiwa bado ipo ktk mzunguko wa kawaida. Kinachofuata ni hasara kubwa sana kw Wafanyabiashara hio ambao wengi wao wanadaiwa na Banki mbalimbali.


1.JPG



Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Richard Muyungi akimuhoji mmoja

wa Wamiliki wa kiwanda cha Afro African Company kilichopo Mwenge jijini Dar es Salaam

ambao ni wazalishaji na watengenezaji wa pombe mbalimbali aina ya viroba. Ofisi ya Makamu

wa Raisi inaongoza uendeshaji wa ukaguzi wa viwanda vyote jijini Dar es Salaam vinavyozalisha

na kutengeneza pombe kali(viroba) na kufunga kwa vifungashio vya plastiki.



2.JPG

Mwanasheria wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira NEMC , Heche Suguti akiwaonyesha

waandishi wa habari aina mojawapo ya pombe kali (kiroba)

3..JPG

Mrundikano wa maboksi uliopo kiwandani hapo ambapo ndani yake tayari kumejazwa pombe za

aina mbalimbali aina ya viroba tayari kwa kuuza.
 
Hivi hasara ya hivyo viwanda inalingana na athari wanazopata wanywaji wa hivyo viroba?
 
Hivi hasara ya hivyo viwanda inalingana na athari wanazopata wanywaji wa hivyo viroba?[

Hasara sio kwa wamiliki wa viwanda hata kwa wafanyabiashara wadogo waliokopa pesa zao Pride na Bayport wataathilika, by the way nazani kungekuwa na steps za kuzuia sio maamuzi ya kukurupuka tu
 
Waiombe serikali iwape mtaji wafungue biashara tofauti na kutengeneza viroba kwasababu vibali walitoa wao,pia bora wange wapa muda hata wa miezi 3 wamalize stock hatakama vijana wanaharibaka lakini hawajaanza leo....!!!
 
Back
Top Bottom