Uzoefu wangu katika maisha; niliyoyaona katika Mahakama za Mwanzo yanatisha

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,487
2,344
Wasalam,

Leo nimependa kushare nanyi baadhi ya mambo ya kusikitisha yanayoendelea katika mahakama za mwanzo na si kwamba yanafanywa na mahakimu wote la hasha bali wachache wenye nia ovu. Naandika haya si kuwa nimesimuliwa hapana ila ni mambo yaliyonitokea miaka ya nyuma kipindi biashara yangu imeyumba. Baada ya biashara kuyumba nikajikuta na madeni mengi yasiweza kulipika kwa wakati huo hiyvo wadeni wangu wakawa wanatumia mbinu mbalimbalia za kunibana, haya ndiyo niliyoyashuhudia.

1. Unaweza kusomewa hukumu imekaa namna hii ila siku ya kuchukua nakala ya hukumu ukakutana na kitu tofauti kabisa. Mfano unaweza kuambiwa unatakiwa kulipa laki moja ila kwenye hukumu ikaandikwa laki 6. Sasa kumbuka uliposomewa unalipa laki moja ulirelax hujujisumbua na rufaa kumbe huku kwenye makaratasi ngoma ni nyingine kabisa yaani.

2. Hakimu anaweza toa hati ya kukukamata kwa nguvu wakati unafahamika ulipo na wala si mtu wa shari l, hujaiba na kesi ni madai. Anayekudai anachonga na hakimu namna ya kukuharass anapewa hati ya kukukamata kwa nguvu anapeleka polisi msako unaanza. Ukidakwa unalala rumande wala hapo huwezi dhaminiwa polisi hadi mahakamani. Na siku ukipelekwa mahakamani hakimu husika anajifanya busy ili mradi tu ushuke magereza hapo kama unachochote lazima ujitikise.

3. Mdai anaweza kufungua kesi na usipewe summons ya kuitwa na ikaendeshwa upande mmoja. Siku moja niko mahakamani kwa kesi nyingine nikasikia jina langu linatajwa ile kuingia kule nikakuta ni kesi nyingine kabisa ambayo siijui na imeshafika mbali.

4. Inaweza kuwa ni madai ukafunguliwa jinai, japo una vielelezo au hata anayekudai akashindwa kuthibitisha jinai yake ila ukaambiwa ulipe faini au kifungo na siku ya pili ukatakiwa kulipa kiasi chote unachodaiwa.

Kiufupi ni mududu ni mengi, ndio maana kuna msemo wanasema mahakama za mwanzo hakuna sheria, serikali ijitahidi kuboresha hizi mahakama kwa kweli la sivyo haki za wengi zitakuwa zinapotea.
 
Ukiona mambo mengi rejea ule uzi wa waliowahi kukaa Jela utapata mbinu nzuri za kudili na hao wakuda.
 
Mi nilivyoona hakimu anaonekana kala rushwa tayari, niliandika barua ya kuhamishia kesi mahakama ya wilaya ksb ya kutokuwa na imani na hakimu.
Na hakimu mla pesa unamuona hata hamjafika mbali
 
Unaposhtakiwa kwa deni mahakamani unalipa deni pamoja na gharama za kesi (.......pamoja na gharama nyingine kama mahakama itakavyoona inafaa) ndivyo shtaka litakavyosomeka.
 
Nenda mahakama ya mwanzo Mbagala ukaone jinsi polisi waendesha mashtaka na makarani walivyo relax na majukumu yao km kuita mafaili ya kesi,taratibu za kutoa dhamana nk, kuwaachia watu ambao si wafanyakazi wa idara ya mahakama kufanya kazi hizo.

Majukumu hayo wameachiwa vibaka wanaotumia mwamvuli wa ulinzi shirikishi /sungusungu ambao ni mawakala wa mapolisi na makarani hao ili kufanikisha upokeaji/utozwaji wa rushwa bila wahusika hao kuishiriki na kujihusisha moja kwa moja.
 
Nenda mahakama ya mwanzo Mbagala ukaone jinsi polisi waendesha mashtaka na makarani walivyo relax na majukumu yao km kuita mafaili ya kesi,taratibu za kutoa dhamana nk, kuwaachia watu ambao si wafanyakazi wa idara ya mahakama kufanya kazi hizo. Majukumu hayo wameachiwa vibaka wanaotumia mwamvuli wa ulinzi shirikishi /sungusungu ambao ni mawakala wa mapolisi na makarani hao ili kufanikisha upokeaji/utozwaji wa rushwa bila wahusika hao kuishiriki na kujihusisha moja kwa moja.
Hawa jamaa ndio milango ya pesa
 
Unaposhtakiwa kwa deni mahakamani unalipa deni pamoja na gharama za kesi (.......pamoja na gharama nyingine kama mahakama itakavyoona inafaa) ndivyo shtaka litakavyosomeka.
Shida inakuja pale deni linapogeuka jinai
 
Mahakama za mwanzo ni ushenzi mtupu,
Nilikuwa na kesi moja,ya kugonga na kuua,unakuta mwendesha mashitaka,na Hakimu,huku uraiani,ni maswaiba,wanakula bia pamoja,mademu kwenda mbele,
Sasa Ili upate dhamana,inabidi uwe nao vzr,kiasi wanachotaka lazima uwape,bila hivyo kesi ikitajwa,wewe ni jera tu,
Kuna mwendesha mashitaka mmoja,ikifika jioni,anachukua gari yake,corona,na kijana wake mmoja,wanaenda kutega,kupiga hela kwa watu wa malori
 
Back
Top Bottom