Uzoefu wa Kukaribia Kifo

Uzoefu wa Kukaribia Kifo

Hapana ni udadisi tu halafu hataki kufunguka!
Anakutania tu hakuna kitu kama hicho.
Meditation does not have to do with NDE kufa ni kufa tu...

Hata near death experience pale mtu anakuwa inaonesha kama amekufa ila bado you hai... Yaani mwili wake unakuwa na some sort of energy kupokea spirit..

Ndo maana huwa kuna kuwa na separation kati ya soul and body kwa muda kadhaa kabla soul haiajrudi ndani ya body..
 
Talking about meditation, inakufanya uwe na realization kuwa you aren't the body and mind alone....

You are essentially a soul habouriing the body and mind.

NDE makes you really and fully realize the incomprehensible power of your soul and spirit. Ndo maana mtu akishinda NDE huwa anarudi akiwa unstoppable
 
Anakutania tu hakuna kitu kama hicho.
Meditation does not have to do with NDE kufa ni kufa tu...

Hata near death experience pale mtu anakuwa inaonesha kama amekufa ila bado you hai... Yaani mwili wake unakuwa na some sort of energy kupokea spirit..

Ndo maana huwa kuna kuwa na separation kati ya soul and body kwa muda kadhaa kabla soul haiajrudi ndani ya body..

Haya mambo haya.
 
Nina miaka kadhaa kwenye mambo haya ila pia kuna mapya tunazidi kujifunza. Kadri unavyozidi kujifunza ndio unagundua safari ya kujifunza haina ukomo.

Science + spirituality + philosophy.
There's no amount of learning that will make you enlightened!

Labda kama unataka kuikuza ego?
 
Learning is an endless process and the more I learn the more I see myself that I know nothing.
Sasa why waste time learning and not unlearning?

Infact true zen spirituality entails the letting go of what you think you know. It's all about letting go of the need to know, thus knowing everything. Most of which unataka kujua ni smokes and mirrors
 
Je umewahi kumsikia mtu aliyepata ajali mbaya au moyo wake kusimama akiwa hospitalini, madaktari wakamtangaza amefariki, lakini baada ya dakika chache moyo ukaanza tena kudunda na akazinduka? Anapozinduka, anakupa kisa cha ajabu cha pale alipokuwa kwa hizo dakika chache!

Kitendo hiki huitwa Near-Death Experience (kuchungulia kaburi) au Uzoefu wa Kukaribia Kifo. mamilioni ya watu duniani kote waliowahi kukaribia kifo wanatoa ushuhuda unaofanana kwa takriban 90%, hata kama wanatoka kwenye dini, utamaduni, au nchi tofauti kabisa.

Mambo yanayojirudia Kwenye kukaribia kifo:

Kujitenga na Mwili: Mtu anahisi nafsi yake imetoka mwilini na inajiona ikiwa juu ya dari au pembeni, ikishuhudia madaktari wakipambana kuokoa mwili wake au ndugu wakilia.

Handaki la Mwangaza: Wengi wanaeleza kusafiri kwa kasi kubwa kupitia handaki la giza kuelekea kwenye mwangaza mkali sana ambao hauumizi macho, bali unatoa amani na upendo usioelezeka.

Video ya Maisha: Kwenye sekunde chache, mtu anaona matukio yote ya maisha yake yakipita kama filamu—kuanzia utotoni hadi sekunde ya mwisho—huku akihisi maumivu au furaha aliyowapa wenzake.

Kukutana na Watu Waliotangulia: Wengi wanaeleza kukutana na ndugu au marafiki waliokwisha kufa zamani, au viumbe vya mwangaza, wakimwambia: "Muda wako haujafika bado, lazima urudi duniani"🤔

Nini Kinasababisha hali hii?

Mitazamo ya Kisayansi: Wanasayansi wa ubongo (Neuroscientists) wanadai kuwa wakati moyo unaposimama, ubongo unakosa oksijeni. Kwenye sekunde hizo za mwisho, ubongo unajilinda kwa kutoa kemikali nyingi za Endorphins na DMT zinazotengeneza ndoto nene sana ili kumpa mtu amani asihisi maumivu ya kifo.

Mitazamo ya Kiroho: Viongozi wa dini na wanafalsafa wanaamini kuwa hii ni thibitisho kwamba mwanadamu si mwili tu, bali ni nafsi inayojitegemea, na kwamba kuna maisha au ulimwengu mwingine baada ya kifo cha kimwili.

Shuhuda kutoka kwa watu wote waliowahi kupitia uzoefu wa kukaribia kufa ni kwamba, baada ya kuzinduka, maisha yao yanabadilika kabisa. Wanaacha kuogopa kifo, wanaacha kufukuzia mali kwa tamaa, na wanaanza kujali upendo na mahusiano ya kibinadamu. Maisha ni mafupi mno; usiishi kwa chuki au wasiwasi wakati hujui sekunde inayofuata italeta nini!
Hii Kuna wanasayansi washa ifatilia Lakini sio Kwa mantiki ya kifo

Inaitwa Astral body projection
Fatilia hiyo Mkuu
 
Huku mtaani kwetu miaka ya nyuma kuna jamaa alikuwa mgonjwa akapelekwa hospitali, baada ya siku kadhaa madaktari wakathibitisha amefariki dunia na kuwajuza ndugu zake.

Akapelekwa mochwari then ndugu wakachukua mwili kwa ajili ya maandalizi ya maziko. Akasoshwa na kufanyiwa taratibu zote anazofanyiwa maiti, ajabu wakati wanataka kuswalia maiti watu wa karibu na jeneza wakasikia mtu amepiga chafya kama mara tatu na kama mnavyojua muda wa kuswalia maiti kunakuwa na ukimya, ghafla wakaona jeneza linatikisika.

Watu waliopo msibani wakaanza kukimbia huko na huko, masheikh na watu kadhaa ikabidi wachukue jeneza kulirudisha ndani, kufungua wakakuta jamaa macho yamemtoka, wakamtoa na kushauriana kumpeleka tena hospitali.

Kufika hospitali ikawa gumzo ika akalazwa tena na baada ya wiki akaruhusiwa kurudi nyumbani.

Ajabu ni kuwa hata baada ya kupona akawa sio mtu wa kuongea sana, akitaka kitu anaomba basi ila akiulizwa jambo lolote anajibu tofauti na swali, ni kama alichanganyikiwa. Hata watoto wake na mkewe akawa amewasahau hana habari nao. Kubwa kuliko yote ni kuwa wakati kabla hajafa alikuwa ni mkulima tu wa kawaida ila baada ya kufa na kufufuka akawa halimi tena akaanza kuuza pilipili mtaani ndio ikawa shughuli yake kuu.

Ikapita tena kama miaka mitatu hivi akagongwa na gari la kusomba magogo akafariki hapohapo ndio ikawa kifo chake halisi maana kwenye ile ajali hakuomba hata maji.
 
Sasa why waste time learning and not unlearning?

Infact true zen spirituality entails the letting go of what you think you know. It's all about letting go of the need to know, thus knowing everything. Most of which unataka kujua ni smokes and mirrors

Siwezi kuacha kujifunza mkuu kuna mambo mengi ya kujifunza hata hizo habari za Zen spirituality lazima ujifunze kwanza ndio uzijue.
 
Back
Top Bottom