Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Uzinzi ni dhambi ya mauti...

Kuna watu uzinzi unatutesa Sana, na ndo tunaongoza kwa kuipenda Sasa, na tukiweza kudhibiti hapo hata mafanikio huja kwa urahisi kabisa
Pole mkuu. Ukiamua kwa dhati unaweza kuepukana nao. Ingawa kwa sehemu ni lazima na Mungu aingilie kati.
 
Hizo ni propaganda za westerns kutukwamisha tusizaliane. Haiwezekani tendo la kuunganisha jinsia mbili ili zitoe kiumbe kipya liwe tendo baya.

Kwanza lilipaswa kuwa tendo takatifu kwani wote tumepatikana kwa kufanya Hilo tendo. Haijarishi limefanyikia wapi na mazingira Gani, Hilo ni tendo takatifu.

Hebu tufikirie vizuri maana hizo Imani zenu na dini zinawapotosha pakubwa. Tuwaze upya
Ni kweli usemayo.
Haiwezekani Mungu aumbe tendo tamu hivyo tena lenye hisia nyingi halafu useme ni dhambi ya mauti.
Ametuwekea matamanio ya hali ya juu na kusababisha kushindwa kuvishinda vishawishi halafu leo liwe tendo baya kiasi hicho...je alivyotuumba hakuujua udhaifu wetu au anatufanyia kusudi?
 
Sawa Bibiye
Ni kweli usemayo.
Haiwezekani Mungu aumbe tendo tamu hivyo tena lenye hisia nyingi halafu useme ni dhambi ya mauti.
Ametuwekea matamanio ya hali ya juu na kusababisha kushindwa kuvishinda vishawishi halafu leo liwe tendo baya kiasi hicho...je alivyotuumba hakuujua udhaifu wetu au anatufanyia kusudi?
 
Mkuu, umesema wazinzi wataadhibiwa wakifika mbinguni?
 
Kuna watu uzinzi unatutesa Sana, na ndo tunaongoza kwa kuipenda Sasa, na tukiweza kudhibiti hapo hata mafanikio huja kwa urahisi kabisa
Wee vipi tena...huo uzinzi ndio tyati mafanikio yenyewe au wee mafanikio ni kuwa na majumba na magari?
 
Nini maana ya kukufuru?
Ni maneno ya dhihaka, dharau, kejeli, matusi kinyume na Mungu.
Ayubu 2:9 Ndipo mkewe akamwambia,je wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Umkufuru Mungu ukafe.
Walawi 24:16 Na yeye atakayelikufuru jina la BWANA hakika atauawa, mkutano wote watampiga kwa mawe....
Agano la kale(torati) aliyemkufuru Mungu ilimpasa auawe kwa kupigwa kwa mawe.
Agano jipya imeenda zaidi kwa anayekufuru kutosamehewa milele,na na imekuwa specified kumkufuru Roho Mtakatifu.
Kwa tunaoamini kuhusu uungu nafikiri tutaelewa kirahisi kwanini sio Mungu baba,wala Mwana bali Roho Mtakatifu?
Marko 3:28-29 Amin nawaambia dhambi zote watasamehewa wanadamu na kufuru zao watakazokufuru zote,
29.bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele ila atakuwa na dhambi ya milele.
Luka 12:10 Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa,bali aliyemkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Kwanini Roho Mtakatifu?
Yohana 16:8 Naye akiisha kuja huyo,atauhakikishia ulimwengu kwa habari ya dhambi,na haki,na hukumu.
Roho Mtakatifu ndiye anayetushuhudia kwa habari ya dhambi zetu,huachilia hali ya kusikia hatia(convict)tunapokosea mioyoni mwetu ili tutubie dhambi zetu kwa toba,hutuelekeza kwenye haki.
Yeye ndiye anayewavuta wenye dhambi kwa kuweka hali ya kujutia makosa yao na kuamua kuokoka.
So Biblia inamaanisha huyo Roho Mtakatifu akifanya hayo yote kwako na kumjua Mungu na kumtumikia chini ya nguvu ya Roho Mtakatifu ukaona kwa dhahiri nguvu na uwezo wa Mungu kwa dhahiri watu wakajua na kukuheshimu kama mtu wa Mungu na shetani amejua,ghafla ukiiacha hiyo neema na kuanza kukufuru matukufu ya Roho Mtakatifu ndio inaitwa dhambi ya kumkufuru Roho Mtakatifu.
Unakuwa umemhuzunisha na kumnyamazisha ndani yako unasaidikaje?
Unakuwa kama mnyama tu,husikii hali ya hatia,huhisi tena hukumu ukikosea ili utubu nafsi inakuwa imekufa haiwezi kufanywa hai tena maana aletaye hali ili utafute kuwa hai anenyamaza kwa kumnyamazisha makusudi kwa dhihaka,dharau.
2 Petro 2:12 ...Kama wanyama wasio na akili...wakimufuru....wataangamizwa.
Waefeso 6:4 Kwa maana hao waliokwisha kupata nuru na kukionja kipawa cha nguvu,na kufanywa Washirika wa Roho Mtakatifu,
5,na kulionja neno zuri la Mungu na nguvu za zamani ,zijazo
6.Wakaanguka baada ya hayo HAIWEZEKANI kuwafanya UPYA TENA hata WAKATUBU,kwa kuwa wamsulubisha Mwana wa Adamu mara ya pili kwa nafsi zao na KUMFEDHEHI KWA DHAHIRI.
Shukrani kwa ufafanuzi pia katika ZABURI 33:1 imeandikwa "Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki, Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo" je mtu anaposifu na kuapoabudu akiwa anajijua ana dhambi na hajatubu hiyo ni kufuru au sio kufuru.
 
hahaaaaa hua nacheka sana nikicheki movie(MISSING IN ACTION) CIA FBI wanakua sehemu ya kuungama dhambi zetu
Yote sawa tu maana huko zamani wana wa israeli walikuwa 'wanaungama' kwa kuweka dhambi kwa mbuzi mbele ya kuhani.
 
Back
Top Bottom