Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 8,988
- 11,862
Uzinzi siyo tu dhambi ya mwili, bali ni silaha kali ya adui inayotumika kuvunja, kuiba, na kuharibu kibali ambacho mtu amepokea kutoka kwa Mungu. Katika ulimwengu wa roho, kuna vitu ambavyo si rahisi kuviona kwa macho ya kawaida, lakini vina uzito mkubwa sana katika maisha ya kiroho na kimwili. Moja ya vitu hivyo ni kibali cha kiroho neema ya kipekee ya Mungu inayofungua milango, inayokufanya upokelewe mahali ambapo wengine wanakataliwa, inayokuinua bila maelezo ya kawaida, na inayosababisha baraka zako zitiririke bila kusimama.
Lakini sehemu ambayo mtu hupoteza kibali chake kwa haraka mno ni pale anaporuhusu mwili wake kulala na mtu ambaye Mungu hajampangia kuwa naye. Ni siku hiyo ambapo mwili unapochukua nafasi ya roho; hisia zinaposhinda maono; tamaa zinapoziba macho ya kiroho; na agano la kimwili linapoundwa kinyume na mapenzi ya Mungu. Mtu huyo hujafanya naye agano la ndoa, lakini kupitia tendo hilo, anajikuta amejiunganisha kiroho na mtu ambaye hakuwa sehemu ya mpango wa Mungu katika maisha yake.
Kwa nje, mwili unaweza kufurahia kwa muda mfupi, lakini ndani rohoni kuna uharibifu mkubwa unaotokea. Roho yako inachafuka, dhamira inachafuliwa, na ule utukufu uliokuwa umewekwa juu yako unaanza kufifia. Mungu huchukia sana tendo la uzinzi, si kwa sababu tu ni uvunjaji wa sheria zake, bali kwa sababu lina madhara makubwa katika nafasi ya mtu ya kiroho. Kila tendo la uzinzi huacha alama, huleta vifungo visivyoonekana, na mara nyingi huchangia kuvuja kwa kibali cha kiroho.
Uzinzi ni kama mnyang'anyi wa baraka. Unaweza kuiba ndoto yako, kufuta mwelekeo wa maisha yako, au kufunika mlango wa fursa ambao ulikuwa umefunguliwa na Mungu. Kile ambacho Mungu alikuwa amekupangia iwe ni ndoa ya baraka, huduma yenye matokeo, biashara yenye mafanikio, au hata vipawa vya kipekee vinaweza kusimama ghafla kwa sababu mlango wa roho yako ulifunguliwa kwa mtu asiye sahihi.
Kwa kawaida, kibali hakipotei mara moja. Kinaanza kupungua taratibu. Utaanza kuona vitu ambavyo vilikuwa rahisi kwako hapo awali vinakuwa vigumu; mahali ulipokuwa unapendwa huoni tena ile heshima; hata kibinadamu, watu wanaanza kukushangaa kwa mabadiliko yasiyoeleweka. Huo ni mwanzo wa mwisho wa kibali kinapungua kidogo kidogo mpaka kinapokauka kabisa.
Uzinzi ni agano la giza. Linaweza kufungwa kwa dakika chache lakini likakugharimu miaka mingi ya kupigania maisha yako ya kiroho na ya kimwili. Linaweza kukufanya upoteze mwelekeo, amani, heshima, na hata tumaini.
Watafiti wanasema Wanaume wengi waliopoteza mwelekeo wa maisha, waliokatika baraka, au waliofirisika kabisa si kwa sababu hawakuwa na akili au juhudi, bali ni kwa sababu ya uzinzi. Uzinzi umevuruga maisha ya wanaume wengi kimya kimya. Kwa nje anaonekana anafanya kazi au biashara, lakini kwa ndani kuna agano baya lililofungwa ambalo linaiba nguvu, kibali, na baraka zake taratibu.
Utakuta mwanzo wake ulikuwa mzuri biashara zilikuwa zinaenda, milango ilikuwa inafunguka, watu walikuwa wanamkubali, maisha yalikuwa na mwanga. Lakini baada ya kuingia katika uzinzi, ghafla vitu vinaanza kubadilika. Biashara zinaanza kuanguka, mapato yanapungua bila sababu, hata nguvu ya kupambana na changamoto inapotea. Unajiuliza tatizo liko wapi, lakini huoni kumbe ni mlango wa roho alioufunguwa kwa tamaa ya mwili.
Kila mtu ambaye unalala naye kinyume na mapenzi ya Mungu, hasa nje ya ndoa, ni agano linalojifunga kiroho. Hujui huyo mtu anatoka na mzigo wa aina gani: roho za laana, roho za umaskini, vifungo vya familia, au roho za kuangamiza. Mnapoingiliana, yale mapepo na vifungo vinakuwa sehemu ya maisha yako bila kujua. Na huanza kuvuruga eneo la fedha, afya, maono na hata mahusiano ya kifamilia.
Mungu anapokupa kibali cha kusonga mbele, anataka ukubali pia nidhamu ya kiroho na maadili. Ukivunja hiyo nidhamu kwa uzinzi, ni kama unamwambia Mungu: “Sina haja na ulinzi Wako, naweza kujitawala mwenyewe.” Na matokeo yake ni kwamba roho ya uharibifu inaanza kazi yake polepole.
"Mwenye kuzini hana akili; afanya hivyo hujiangamiza nafsi yake." Methali 6:32