Uzinduzi wa Mpango wa Maendeleo wa Wizara ya TEHAMA: Kumbe waliodhani ni Wizara ya VPN walikosea

Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,021
2,478
1625197619693.png

Katibu wa Wizara ya TEHAMA, Dk Zainab Chaula, na Waziri wake, Dk Ndungulile wakiteta jambo
Wizara ya Tekinolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) imezindua mpango wake wa maendeleo wa miaka mitano (2021-2026), mjini Dodoma leo.

Ni wizara ya kwanza kufanya hivyo ndani ya siku mbili baada ya mpango wa maendeleo wa Taifa, wa miaka mitano (2021-2026), kuzinduliwa mjini Dodoma.

Dira, dhima, na tunu za Wizara

Akizindua mpango wa Wizara ya TEHAMA mjini Dodoma leo, Waziri Dakta Faustine Ndungulile ametaja dira, dhima, tunu, dhamana na malengo ya Wizara anayoiongoza.

Aliliambia Taifa kwamba, Wizara hii iliyoanzishwa tarehe 05 Desemba 2020, chini ya serikali ya awamu ya tano, inayo dira, dhima, tunu, dhamana kama ifutavyo:

Dira: Taifa kuwa na uwezo wa kidijitali kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Dhima: Kuibadilisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kidijitali kwa kuhakikisha upatikanaji wa huduma za kidijitali katika sekta za kompyuta, mawasiliano ya simu na huduma za posta kwa kutumia mazingira yenye ubunifu unaoweza.

Tunu: Wizara inazo tunu tano, yaanu, uadilifu, uwazi, ushirikiano, weledi, ubunifu na uwajibikaji.


Dhamana na malengo ya Wizara

Dhamana: Kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa sera zinazohusiana na utoaji wa huduma za kidijitali katika sekta za kompyuta, mawasiliano ya simu na huduma za posta; Kusimamia ujenzi wa mkongo wa Taifa kwa ajili ya kusambaza intaneti nchini; na kuunga mkono ufanisi wa kazi za Wizara baki, Idara za serikali, mashirika ya umma, na mawakala wa serikali kwa kuwapa mafunzo ya TEHAMA.

Malengo: Aidha, katika uzinduzi huo, malengo ya Wizara yalitajwa. Malengo hayo ni pamoja na:

  • Kuboresha upatikanaji wa huduma za kidijitali katika sekta za kompyuta, mawasiliano ya simu na huduma za posta;
  • kujenga uwezo wa kidijitali kwa ajili ya kusukuma gurudumu la maendeleo ya kiuchumi na kijamii;
  • kufanya menejimenti ya uduma za kidijitali katika sekta za kompyuta, mawasiliano ya simu na huduma za posta; na
  • kujenga uwezo wa kitaasisi katika ngazi ya wizara ili iweze kutekeleza majukumu yake.
Malengo yasiyohusiana na Wizara ya TEHAMA

Hata hivyo, kuna malengo mawili yaliyotajwa katika uzinduzi huo ambayo hayahusiani kabisa na Wizara hii. Malengo hayo ni:

  • kupunguza maambuzi ya VVU/UKIMWI na tatizo la magonjwa yasiyoambukizwa kwa kutoa huduma stahiki, na
  • kuhakikisha kuwa utekelezaji wa mkakati wa Taifa dhidi ya rushwa unatekelezwa ipapsavyo.
Kwenye tovuti ya Wizara, malengo hayo yanasomeka hivi:

1625199330343.png

Picha ya malengo ya kimkakati ya Wizara ya TEHAMA: Malengo mawili ya kwanza hayapaswi kutekelezwa na Wizara hii


Wizara hii ilianzishwa katika kipindi ambapo huduma za intaneti zilikuwa zinafinywa na serikali. Wakati huo wananchi walikuwa wanapata huduma hii kwa shida kwa msaada wa tekinolojia ya VPN. Hivyo, Wizara hii ikabatizwa jina "Wizara ya VPN". Wengine waliibatiza jina "Wizara ya vifurushi."

Lakini, kwa mujibu wa dira, dhima, tunu, dhamana na malengo yake, hii ni Wizara muhimu sana. "Ni Wizara itakayowaleta wananchi karibu na serikali yao," alisema Dk. Ndungulile.

Alitaja mifano ya huduma za kutuma na kupkea fedha, kununua luku, na kazi kama hizo zinazofanywa na mtu akiwa ameketi sebuleni kwake.

Katika tukio la leo, Wizara pia imezindua tovuti yake rasmi ambayo anwani yake ni
www.mawasiliano.go.tz

Kwa mujibu wa tovuti hii, Wizara inazo Kurugenzi tano, yaani TEHAMA, Mawasiliano ya simu, Sera na Mipnago, Utawala na Utumishi. Hakuna ufafanuzi kuonyesha chini ya Kurugenzi hizi kuna Idara gani.

Pia kuna vitengo vya manunuzi na ugavi, sheria, fedha, ukaguzi wa ndani na mahusiano na umma. Kwa pamoja idara na vitengo hivi vinapaswa kuleta uchumi wa kidijitali nchini Tanzania.

Kukosekana kwa fasili ya "uchumi wa kidijitali"

Wakati maneno "uchumi wa kidijitali" (digital economy) yanazo fasili zinazobadilika kutoka nchi moja hadi nyingine, Waziri hakutwambia jinsi serikali ya Tanzania inavyolifasili.

Lakini, nafahamu maana yake ya jumla. Neno hili limezaliwa mwaka 1995 kupitia kitabu Don Tapscott chake kiitwacho, "The Digital Economy: Promise and Peril in the Age of Networked Intelligence."

Hiki ni kitabu cha kwanza kuonyesha jinsi TEHAMA inavyoweza kutumika kubadilisha maisha ya kiuchumi, kiutawala na kijamii.

Toleo jipya la kitabu hiki, la mwaka 2015, limeambatanishwa hapa chini.


1625205369796.png

Dk. Ndungulile akizindua Mpango wa Maendeleo wa Wizara ya TEHAMA

Katika kitabu chake, mwandishi Don Tapscott (2015) anasema kuwa, uchumi wa kidijitali unazo sifa kumi na mbili, zikiwemo sifa kuu tano zifuatazo:
  • Kufanya kazi kwa kutumia maarifa yaliyo ubongoni badala ya kutumia mitulinga ya kimwili (Knowledge): Katika Zama za Maarifa zaidi ya 50% ni watu wanaofanya kazi za kupokea, kutunza, kuchakata, na kusambaza maarifa katika muundo wa sauti, maandishi ya herufi, maandishi ya tarakimu, picha mnato, na picha za video. Kihistoria mabadiliko yafuatayo yametokea: zama za uwindaji, zama za ukulima, zama za viwanda, na hatimaye zama za maarifa. Katika ulimwngu wa leo, maarifa haya yanasambaa kupitia mawasiliano ya kidijitali badala ya mawasiliano ya kianalogia (Digitization): Katika Zama za Kidijitali zaidi ya 50% ya maarifa yako katika muundo wa kielektroniki. Taarifa zilizoandikwa katika karatasi ni kidogo sana.
  • Kubuni mawazo mapya na kuleta mabadiliko katika miundombinu iliyopo tayari (Innovative Infrastructures and Creativity): Katika Zama za Kidijitali uwezo wa kubuni mabadiliko katika vitu tulivyo navyo ni jambo muhimu sana.
  • Kuwasiliana kwa njia ya mitandao (Networking): Katika Zama za Kidijitali watu wote wanaunganishwa na mitandao ya mawasiliano ya kielektroniki inayohusisha simu za mezani, simu za kiganjani, kompyuta, modemu, minara ya simu, nyaya za shaba, satelaiti zilizoko angani,na antena.
  • Maarifa yenye tabia ya kuvuka mipaka ya Mataifa na Mabara na hivyo kuunganisha nchi na nchi, taifa na taifa, bara na bara, sayari na sayari (Globalization): Katika Zama za Kidijitali kuna mwingiliano wa mifumo ya mawasiliano unaoyawezesha maarifa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mtu mtu, kampuni moja hadi nyingine, kaya moja hadi nyingine, Taifa moja hadi jingine, bara moja hadi jingine. Kwa sababu hii, dunia ni kama kijiji kimoja. Unaweza kutuma baruapepe kwenda ulaya ndani ya dakika moja, hata kabla gari halijasafiri kilometa moja. Pia unaweza kutuma fedha nchi nyingine kupitia mitandao ya tigopesa, mpesa, halopesa, ttclpesa, na kadhalika.
  • Mafunzo ya stadi za TEHAMA (Skills development): Zama za TEHAMA zinahitaji ujuzi na stadi mpya ili kuwawezesha watu kukusanya, kuchakata, kutunza, na kusambaza maarifa ya kidijitali kwa ufanisi.
Sifa hizi tano, mara nyingi hurejewa kama "Wafalme Watano wa Uchumi wa Kidijitali." Yaani, "The Five KINGS of Digital Economy."

Neno "KINGS" ni kifupi cha maneno haya: "Knowledege digitalisation, Innovative Infrastructures and creativity, Networking, Globalisation, and Skills Development."

Hivyo, mifumo ya kupima nguvu ya uchumi wa kidijitali katika nchi, kama vile mfumo wa "
Digital Adoption Index (DAI)" uliobuniwa mwaka 2016 na Benki ya Dunia, kwa sehemu kubwa, huangalia ni kwa kiasi gani nchi inazibeba sifa hizi.

Mfumo wa DAI, hupima ni kwa kiasi gani nchi inatumia tekinolojia za kidijitali kwa kumulika sekta tatu za uchumi, yaani, sekta ya watu, sekta ya serikali na sekta ya biashara. Chini ya mfumo huu nchi huweza kupata asilimia kati ya zero na mia moja.

Katika
sekta ya biashara mfumo wa DAI unaangalia ni kwa kiasi gani TEHAMA imetumika kuchochea tija na kasi ya ukuaji.

Katika sekta hii, mwaka 2016, Tanzania ilipata asilimia 28 ikiwa ni nchi ya 174 kati ya nchi 183, nchi zote zikiongozwa na Iceland iliyopata asilimia 97.

Katika
sekta ya watu mfumo wa DAI unaangalia ni kwa kiasi gani TEHAMA imetumika kupanua fursa na kuboresha ustawi wa watu hao.

Katika sekta hii, mwaka 2016, Tanzania ilipata asilimia 17 ikiwa ni nchi ya 152 kati ya nchi 183, nchi zote zikiongozwa na Hong Kong pamoja na China zilizopata asilimia 91.

Katika
sekta ya serikali mfumo wa DAI unaangalia ni kwa kiasi gani TEHAMA imetumika kuongeza kasi ya utoaji huduma na uwajibikaji wa serikali kwa watu wanaohudumiwa.

Katika sekta hii, mwaka 2016, Tanzania ilipata asilimia 57 ikiwa ni nchi ya 77 kati ya nchi 183, nchi zote zikiongozwa na Korea iliyopata asilimia 98.

Na hatimaye ukitafuta wastani wa alama hizi tatu ili kuipa alama nchi yetu, utaona kuwa, katika sekta zote, mwaka 2016, Tanzania ilipata asilimia 34, ikiwa ni nchi ya 135 kati ya nchi 183, nchi zote zikiongozwa na Singapore iliyopata asilimia 87.

Ni kwa sababu hii, baadaye hapa chini nitataja mikakati ya TEHAMA kutoka Singapore kama mifano rejea kwa ajili ya kuwaimarisha wakubwa zangu walioko Wizarani.

Katika sekta ya biashara, mfumo wa DAI unaangalia vigezo vinne: idadi ya tovuti za kibiashara, seva salama, kasi ya kupakua data, eneo la nchi lenye mitandao ya kizazi cha tatu (3G).

Katika sekta ya watu, mfumo wa DAI unaangalia vigezo vitatu: idadi ya simu za kiganjani kwa kila kaya, upatikanaji wa intaneti kwenye kaya, na gharama za intaneti.

Na katika sekta ya serikali, mfumo wa DAI unaangalia vigezo kumi na sita. Vigezo hivyo ni: matumizi ya TEHAMA katika kutengeneza bajeti, matumizi ya TEHAMA katika kusimamia bajeti, matumizi ya TEHAMA katika kuendesha akaunti kuu ya hazina, vyanzo vya taarifa za kifedha, matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa utumishi wa umma, matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa mishahara, matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa kusimamia kodi.

Aidha, katika sekta ya serikali, mfumo wa DAI unaangalia matumizi ya TEHAMA katika kupokea taarufa za wateja, matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa ushuru wa forodha, matumizi ya TEHAMA katika mfumo wa manunuzi ya umma, uwepo wa huduma za kidijitali kwa umma, matumizi ya sahihi za kidijitali, aina ya kadi zinazotumika, matumizi ya alama za vidole, na ukubwa wa huduma zinazopatikana kwa njia ya mtandao.

Lakini, mbali na mfumo wa DAI unaotumiwa na Benki ya Dunia, kuna mifumo mingine pia. Kwa mfano, Umoja wa Ulaya unatumia mfumo uitwao "Digital Economy and Society Index (DESI)".

Mfumo wa DESI unatumia vigezo vya ufanisi 40 vinavyogusa sekta kuu tano za kisera zilizogawanyika kwenye vijisekta kadhaa. Sekta hizo ni mitandao ya kidijitali, kuendeleza rasilimali watu, matumizi ya intaneti, kufungamana kwa miundombinu ya TEHAMA, na huduma za kidijitali kwa umma. (Tazama picha)

1625344048774.png

Mfumo wa DESI kwa ajili ya Umoja wa Ulaya

Katika kutumia mfumo wa DESI Umoja wa Ulaya unajaribu kujibu maswali yafuatayo kwa kila sekta:
  • Connectivity
    • Connectivity is a necessary infrastructure for a digital economy and society.
    • A digital society can only develop if its members are connected to the Internet.
    • A high-speed Internet connection is essential to fully benefit from the developments of today’s digital world.
  • Human Capital
    • Digital skills are a necessary prerequisite for a digital economy and society.
    • Citizens must have the appropriate skills to take advantage of the Internet.
    • Basic skills enable individuals to take part in the digital society.
    • Advanced skills empower the workforce to develop digital goods and services for enhanced productivity and economic growth.
  • Use of Internet
    • Citizens consume online content (e.g. news, music, movies, TV or games).
    • Citizens communicate online in different ways (e.g. online video-calls or social networks).
    • Citizens engage in online transactions (e.g. banking or shopping online).
    • Such online activities are drivers for the development of broadband networks.
  • Integration of Digital Technology
    • Business digitisation is one of the main contributors to enhanced economic growth.
    • Adoption of digital technology enhances efficiency, reduces costs and allows for closer engagement with customers, collaborators or business partners.
    • The ability to use the Internet as a sales outlet pushes businesses to modernise and allows them to exploit new sources of revenue.
  • Digital Public Services
    • Digital technologies can improve business and citizen interaction with the public sector.
    • Public administrations can better address business and citizen needs, while reducing costs.
    • Better and more streamlined public services make citizens and businesses gain efficiency, both due to better functionality as well as to reductions in time spent.

Maelezo haya yanatosha kumsaidia msomaji kuelewa maana ya uchumi wa kidijitali na jinsi unavypimwa, japo kwa juu juu.

Mapendekezo muhimu kwa serikali

Baada ya kusema haya, sasa napenda kutoa mapendekezo ya aina mbili. Kwanza ni mapendekezo kwa Wizara, na pili ni mapendekezo kwa Rais Samia.


Mapendekezo kwa Vigogo katika Wizara ya TEHAMA: Katika uzinduzi huu wataalam wa TEHAMA walitarajia kusikia Taifa limetoka wapi, liko wapi, na linakwenda wapi katika suala zima la huduma za kidijitali kwa umma, kama maeneo ya kimkakati kuelekea Taifa la Kidijitali lenye Usalama, yaani "secure and smart nation."

Taifa la Kidijitali linaweza kuwa na nguzo kuu tatu: Yaani, uchumi wa kidijitali, Serikali ya kidijitali, na Jamii ya Kidijitali. Yaani, "digital Economy, digital government and digital society."

Wataalam wa TEHAMA walitarajia kusikia Wizara ikiongelea uimara, uadhaifu, changamoto, fursa na mikakati ya kubadilisha udhaifu kuwa uimara katika maeneo kama maeneo haya. Hotuba zote hazikukidhi matarajio.


1625219447821.png

Dk. Ndungulile akiwa na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu

Hivyo, inapendekezwa kwamba Wizara ya TEHAMA ifanye yafuatayo, kama itaona yanafaa:
  • Kusoma nyaraka zifuatazo ili kujifunza kitu:
  • Kurekebisha DIRA ya Wizara isomeke:
    • "Kuwa na Taifa linalosifika kwa usalama na udijitali katika sekta zote za maisha ya watu."
  • Kurekebisha DHIMA ya Wizara isomeke:
    • "Kufukuzia dira ya Taifa kwa kujenga uchumi wa kidijitali, jamii ya kidijitali na serikali ya kidijitali."
  • Kwa kuwa Wizara inayo maeneo ya kimkakati (Key Result Areas: KRAs) matatu, yaani, kujenga uchumi wa kidijitali, kujenga jamii ya kidijitali na kujenga serikali ya kidijitali, basi, malengo yake yaandikwe upya kwa kuonyesha ni lengo gani linaanguka chini ya eneo gani la kimkakati.
  • Kuweka Mpango wa maendeleo wa Wizara ya TEHAMA ya Tanzania kwenye tovuti tuusome kirahisi.
  • Kukamilisha tovuti ya Wizara kwa kujaza taarifa katika kurasa nyingi ambazo ni tupu.
  • Kuvunja Kurugenzi ya TEHAMA na kuanzisha Kurugenzi tatu zifuatazo badala yake:
    • Digital Economy Directorate,
    • Digital Government Directorate,
    • Digital Society Directorate.
  • Chini ya Kurugenzi mpya zilizopendekezwa kubuni Idara kadhaa kadiri ya mahitaji ya nchi na dhima ya Wizara.
1625219555655.png

Dk. Ndungulile akiwa na Waziri wa Habari na Michezo, Innocent Bashungwa

Mapendekezo kwa Rais Samia: Kwa mujibu wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo kwenda 2025 niliousoma, naona kuwa, dira ya Taifa letu ni kujenga "a secure and smart nation having a digitally-driven middle income economy by 2025". Huu ni mnyambulisho wangu wa dira ya Taifa.

Wizara ya TEHAMA inabeba dhamana ya kujenga uchumi wa kidijitali, serikali ya kidijitali na jamii ya kidijitali kwa kusababisha usambazaji wa bidhaa na huduma za kidijitali (digital products and services). Hizi ni dhana mpya katika historia ya dunia.

Lakini, kwa mujibu wa historia yake, Wizara ya TEHAMA inayopaswa kusukumua gurudumu hili ni changa sana kuliko Wizara zote.

KItaalam, kunahitajika muda wa kutosha wa kujifunza na kuweka katika vitendo mafunzo (learning curve) katika sekta ya TEHAMA.

Angalau miaka mitatu inahitajika ili mtu aweze kujifunza na kutekeleza alichojifunza. Na sio kila mtu anaweza kujifunza mambo haya ya TEHAMA.

Kwa jadi na historia hili ni eneo la watu waliosoma tahasusi ya PCM au PGM. Yaani Physics, Chemistry and Mathematics au Physics, Geography and Mathematics.

Aidha, kwa sababu ya dhamana yake ya kujenga uchumi wa kidijitali (digital economy), wizara hii ni kikonyo cha Mpango wa Tatu wa Maendeleo ya Taifa uliozinduliwa juzi Dodoma.

Kwa hiyo, ni wizara inayohitaji uangalizi wa karibu, pamoja na usimamizi usio wa kubahatisha kwa mawazo, kwa maneno na kwa vitendo.

Dhamiri yangu inaniambia kuwa, tangu mwanzo, ama uteuzi wako katika eneo hili haukuzingatia masharti ya Hati za Majukumu (Job Descriptions) kwa ajili ya Wizara hii, au hati za majukumu ulizopewa zilikuwa na dosari.

Yaani, uchambuzi wa mahitaji ya nafasi ya kazi na usanifu wa hati ya majukumu (job analysis and design) uliofanyika haukukidhi matakwa halisi ya nafasi husika. Vyovyovte iwavyo, kuna haja ya kufanya marekebisho ya haraka.

Hivyo, Mheshimiwa Rais, naomba nikushauri kufanya yafuatayo kama itakupendeza:

  • Mosi, teua waziri aliyesoma TEHAMA;
  • Pili, teua Katibu Mtendaji aliyesoma TEHAMA;
  • Tatu, simamia uteuzi wa wakuu wa idara waliosomea taaluma zinazoendana na idara wanazoziongoza;
  • Nne, ielekeze Wizara kuachana na lengo la kupambana na VVU/UKIMWI, kwa ni hii ni kazi ya "sekta ya afya".
  • Na tano, ielekeze Wizara kuachana na lengo la kupambana na rushwa, kwani hii ni kazi ya "sekta ya utawala bora".
Kuhusu wataalam nguli wa TEHAMA wanaoweza kuongeza nguvu, wambie wasaidizi wako wakupe nyasifu (profiles) za watu wafuatao na uone jinsi ya kuwatumia, wanaweza kuwa na Msaada Mkubwa sana: Dennis Mkwati, Christopher Hiza, Mashaka Ngunyale, na Cathbert Simalenga. Huyu Simalenga anasali pale City Harvest Church, Kunduchi.

KANUSHO: Sina ugomvi na Dk. Ndungulile wala Katibu wake, Dk. Chaula. Hawa wawili hatufahamiani kabisa.


1625204859042.png

Waziri Dkt. Faustine Ndugulile akizinfua tovuti ya Wizara tya TEHAMA
 

Attachments

  • The Digital Economy ANNIVERSARY EDITION Rethinking Promise and Peril in the Age of Networked I...pdf
    2.9 MB · Views: 6
Back
Top Bottom