Uzinduzi wa Mama Samia Legal Aid Campaign

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
UZINDUZI WA MAMA SAMIA LEGAL AID CAMPAIGN DODOMA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameizundua rasmi kampeni ya msaada wa kisheria inayoitwa Mama Samia Legal Aid Campaign kwa mkoa wa Dodoma Alhamisi (Aprili 27, 2023) huku akiwataka watanzania kuitumia kampeni ya Huduma ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutoa taarifa kuhusu uwepo wa watu, au vikundi vya watu ambao ama wanajihusisha na ukatili wa kijinsia hususan kwa watoto.

“Kampeni hii pia itasaidia kuboresha upatikanaji wa haki kwa watu wasiojiweza, hususani wanawake, watoto na makundi mengine yaliyo katika mazingira magumu. Vilevile, itachangia kuimarisha amani na utulivu, kuongeza kipato cha mmoja mmoja na kuleta utengamano wa kitaifa”. Amesema

Kwa upande wake Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuwa kampeni hiyo ambayo ni maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wanatoa elimu ya sheria na kusaidia wahitaji ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, wamepanga kutoa elimu katika maeneo ya migogoro ya Ardhi, mirathi, ndoa, sheria ya mtoto katika maeneo ya Ukatili wa kijinsia na Maadili

Amesema kuwa kampeni hiyo itatekelezwa pande zote mbili za Muungano kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali na wasio wa serikali ikiwemo Ofisi ya Mashtaka, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ustawi wa Jamii, vyuo vya elimu ya juu, Wengine ni CHAMA cha Wanasheria nchini (TLS), Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria – (TANLAP), Taasisi ya Huduma za Kisheria (LSF), LHRC, EU, UNDP, WILDAF na Benki ya NMB
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.16(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.16(2).jpeg
    40.1 KB · Views: 9
  • WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.16(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.16(1).jpeg
    33.5 KB · Views: 11
  • WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.17(2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.25.17(2).jpeg
    43.4 KB · Views: 10
  • WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.19.27(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.19.27(1).jpeg
    39.1 KB · Views: 11
  • WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.19.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-04-30 at 16.19.27.jpeg
    32.3 KB · Views: 9
Nchi ya wanafiki na sifia sifia.
Uzuri atakufa kama aliyepita na tutamsahau
 
Back
Top Bottom