Uzinduzi wa Maktaba UDSM: Rais Magufuli amtaka Lowassa akawashauri anaowaongoza, otherwise wataishia magerezani wakajifunze kufuata sheria

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
Leo Rais Magufuli anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za uzinduzi wa Maktaba ya Kisasa na Kituo cha Kichina pale UDSM.

Imejengwa kwa ushirikiano wa China na inaweza kuhudumia Wasomaji 2100

Ni moja ya Maktaba za kipekee kabisa kwani ina Rafu (Shelves) zanazoweza kuchukua vitabu laki 8.

Pia ndani ya maktaba hiyo kuna ukumbi unaoweza kuchukua watu mia 6.

=========

Prof. Mutembei
Nawashauri watanzania wajifunze lugha ya Kichina kwasababu ndio lugha inayozungumzwa na watu wengi duniani, ikifuatiwa na Kiispanyola, Kiingereza na Kifansa. Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam kinawahimiza watanzania wazidi kujifunza lugha za kigeni ili waweze kuwa na upana wa lugha mbalimbali.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu
Napenda kuchukua fursa hii kukubaribisha Rais na Wageni wote katika warsha ya kufungua maktaba hii. Katika maktaba zilizojengwa na China, Afrika hii ndio kubwa na kama ingekuwa China ingekuwa ya 5 kwa ukubwa

RC Makonda
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana tena hapa katika tukio hili la kihistoria. Kwa taarifa fupi tu, mkoa wetu unaendelea vizuri kwa amani na utulivu huku wananchi wakiendelea kufanya kazi

Kwa masuala ya elimu mkoa wetu umekuwa wa kwanza kwa upande wa shule za msingi kwa ufaulu wa asilimia 92 . Kidato cha sita pia wamefanya vizuri sana ambapo tumepata ufaulu wa asilimia 97

Nashangaa hata wale wabunge wapinzani wa Dar es salaam ambao mara nyingi wanakuja vyuoni kuwarubuni wanafunzi wawapigie kura lakini hawatokei kwenye shughuli za maendeleo, kazi yao ni kukosoa tu.


Makamu Mkuu UDSM, Prof. Anangisye
Wanajumuiya wa UDSM tunaunga mkono mkoa katika utoaji wa huduma kwa umma. Katika kutambua hilo, tuliandaa kongamano ambalo wewe ulihudhuria ikiwa ni kwa ajili ya kutambua changamoto mbalimbali

Wakati wa Kongamano la Hali ya Uchumi Tanzania, tulifarijika sana uliposema barabara za chuo ziingizwe kwenye ukarabati wa barabara za jiji. Tulishukuru sana, Mungu akusaidie

Chuo Kikuu cha Dar (UDSM) kimekuwa na maktaba tangu kuhamia hapa mwaka 1994/95 na tunajua ni kubwa kuliko zote Tanzania. Hata hivyo, maktaba ilijengwa kwa ajili ya kuhudumia watu wachache

Idadi ya wanafunzi imeongezeka na Kampasi ya Mwalimu Nyerere ina wanafunzi wengi wanaosomea utafiti na kufanya kutegemea maktaba kwa kiasi kikubwa sana. Vile vile, chuo kimeongezeka
sana na hivyo maktaba mpya imekuja kwa wakati muafaka

Maktaba hii itahudumia wanafunzi; nyingine watafti binafsi na taasisi za umma watakaopenda kutumia - Ujenzi wa maktaba hii ulifadhiliwa na watu wa China na kuhusisha majengo mawili

Eneo la Maktaba lina ukubwa wa ekari 4.7 na jengo limechukua mita za mraba 20,000 na kuna maeneo mbalimbali ndani yake Yapo Maeneo ya kusomea ya kukalisha watu 2,100 na kuna eneo la wanafunzi wenye uhitaji maalum

Vifaa vyote vya Maktaba vipo na vimetolewa na China hivyo baada ya uzinduzi huu, itakuwa tayari kutumiwa - Pia imeunganishwa na mfumo wa umeme wa mionzi ya jua wenye uwezo wa kutoa Kilo Volts 280 hivyo kupunguza gharama za umeme

Chuo (UDSM) kimetenga Bilioni 71.78 katika mwaka wa fedha 2017/18 ili kununua majarida na vitabu - Mchakato wa ununuzi unaendelea na tunatarajia kupata nakala 12,640 za vitabu

Gharama za ujenzi zinakadiriwa kuwa USD 41,280,000 na zote zilitolewa na China na hatua za awali zilianza Desemba 2015 - Jiwe la msingi liliwekwa na Rais Magufuli Juni 2, 2016 na ujenzi ulikamilika Julai 2018


Waziri wa Elimu, Joyce Ndalichako
Napenda nianze kwa kukushukuru Rais kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye shughuli hii ambayo tunaandika historia - Ni faraja kubwa wewe kukubali kuja kuzindua hasa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi

Kwa niaba ya wizara na jumuiya nzima ya UDSM nakushukuru kwa kuwa nasi na namshukuru Balozi wa China kwa kusimamia ujenzi huu - Rais, China ni marafiki wazuri kwa kuwa jana tumesaini mkataba wa wao kujenga Chuo cha VETA Bukoba

Maktaba hii itawezesha vijana kusoma vitabu na majarida kadri yatakavyotolewa badala ya kutegemea vitini ambavyo vilikuwa hadi vinabadilika rangi - Pia wataweza kusoma machapisho yanayopatikana katika mfumo wa kielektroniki

Muonekano wa maktaba unavutia sana na vifaa vilivyofungwa ni vya kisasa sana hivyo hatuna budi kulinda muonekano huu - Tutazidisha ulinzi kulinda vifaa na kuhakikisha Wanataaluma wanatoa huduma bora

Mchakato wa ujenzi wa ukumbi wa mihadhara katika chuo kishiriki cha Mkwawa umetutia doa sana, ukumbi wa bilioni 3.6 sasa unajengwa kwa bilioni 8.8 - Mambo yaliyofanyika ni ya hovyo sana ndio maana tulikuomba usiweke jiwe la msingi


Rais Magufuli: Kabla sijaanza kutoa hotuba yangu naomba niwaite baadhi ya wanafunzi waliosoma UDSM kwa miaka ya nyuma waje wawasalimu - Nimemuona rafiki yangu Lowassa ambaye kwa miaka mitatu iliyopita tumekuwa tukipishanapishana barabarani

Prof. Kabudi:
Mwalimu Nyerere wakati anaanzisha chuo hiki wengi walimuona hamnazo - Chuo hiki kilianza kama mbegu ndogo sana ambapo wanafunzi 21 walichaguliwa huku 14 tu wakiripoti


Rais Magufuli:
Tunaweza kusema Chuo Kikuu Dar ni baba lao au mama lao, hiki ndio chuo kikuu cha kwanza Tanzania - Sasa hivi kina Wanafunzi takribani 41 elfu pamoja na vyuo vyake vishiriki

Tupo hapa kuzindua Maktaba hii iliyojengwa kwa msaada wa Wachina yenye kuhudumia wasomaji 2100, ukumbi wa mkutano wa watu 600 - Pia jengo la kufundisha utamaduni wa kichina kwa Watanzania na watu wengine, hongera kwa mkandarasi

Napenda kuipongeza Serikali ya awamu ya nne chini ya Dkt. Kikwete ambayo ndio ilitafuta fedha na kufanya maandalizi - Wakati huo mimi nilikuwa Waziri tu. Awamu hii imefanya utekelezaji

China ni marafiki wazuri wametoa zaidi ya Bilioni 90 fedha za walipa kodi wao bila masharti, maana wengine wangetoa masharti - Naomba Balozi ufikishe asante zetu kwa Rais wenu, asante kwa wananchi wa China pia

Maktaba hii inamuwezesha mtu yeyote, wa dini yoyote au chama chochote kuazima kitabu ambacho labda asingeweza kununua - Ndio maana leo sijashangaa kukutana na ndugu Lowassa hapa. Kwanza hana kelele, hata nilipombwaga alienda akapumzika

Mzee Lowassa wewe ni mzalendo wala huna kelele wenye kelele ni hao wengine. Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ni SuperMan, Hongera mzee Lowassa tunataka Tanzania isiyo na chama - Nakupongeza sana ili hata ukawaeleze unaowaongoza kule vinginevyo wataishia magerezani kwa kuvunja sheria

Degree za desa hazitakiwi, degree iwe degree ya kweli maana inaheshimika dunia nzima - Yapo madogo madogo nilianza kusikia lakini sitaki kuzungumzia sana, simamieni heshima ya chuo

Wito wangu kwa Wanajumuiya ya chuo kikuu cha Dar es Salaam ni kuhakikisha mnatunza maktaba hii - Chapisho lolote lipatikane kwenye maktaba hii ili wanafunzi wakapate wavitakavyo

Kwenye maktaba hiyo pia kuna jengo la kijifunza kichina. Nawasihi watanzania wenzangu mjifunze kwani kina manufaa sana - Mathalani, watalii wengi wanaokuja nchini na sehemu mbalimbali duniani wanaongea kichina

Mmemsikia Prof. Kabudi hapa jinsi chuo kilivyoanza na wanafunzi 14, hao ndo mashujaa wa elimu hapa Tanzania - Tusiogope changamoto, twende nazo ili kufanikisha maendeleo yetu

Tumejipanga kuleta maendeleo ya kweli tukishirikiana na development partners kama wachina - Vya bure vina gharama. Labda viwe vinatoka China ila kwa nchi nyingine vina gharama zake

Habari zaidi...

Rais Dkt John Pombe Magufuli amemmwagia sifa Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kwa namna anavyofanya siasa na kuwataka viongozi wengine wa vyama vya upinzani kuiga mfano wake.

Rais Magufuli amesema kuwa, alishindana na Lowassa katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, na baada ya kumshinda, Lowassa ameamua kutulia na kuendesha siasa za kistaarabu tofauti na wale wengine ambao wamekuwa wakipiga kelele, wakati hata hawakugombea kama ilivyokuwa kwa Mjumbe huyo wa Kamati Kuu wa CHADEMA.

Ameyasema hayo wakati akizindua maktaba ya kisasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) katika Kampasi ya Julius Nyerere, Mlimani na kusema kwa moyo wake wa dhati anampongeza Lowassa.

“Sitashangaa kumuona Mzee Lowassa kwenye maktaba hii. Kwanza nilishindana nae, nilipompiga chini, akatulia. Wale wanaopiga kelele hata hawakugombea. Tunahitaji watu kama Lowassa, hongera sana Mheshimiwa Lowassa,” alisema Rais.

Rais John Magufuli amesema, Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa ni SuperMan na amempongeza utulivu wake baada ya kushindwa alipogombea urais wa Tanzania mwaka 2015

Katika hatua nyingine amewaonya viongozi wa vyama vya upinzani na kusema kwamba kama hawatafuta sheria wataishia magerezani ambako watakwenda kujifunza kufuata sheria.

Akiyasema hayo amemsihi Lowassa kuwafundisha anaowaongoza namna ya kufanya siasa kama ambavyo yeye amekuwa akifanya tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu.

“Mheshimiwa Lowassa naomba uwaeleweshe wale unaowaongoza kule, maana wakiendelea hivi wataishia magerezani wakajifunze kufuata sheria.”

Licha ya kuwa Rais hakutaja moja kwa moja aliokuwa akiwalenga, lakini ni dhahiri alimaanisha viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani, kwani ndio wamekuwa mstari wa mbele kumkosoa na wakati mwingine wakikamatwa kwa kile kinachoelezwa ni ukiukwaji wa sheria.

Aidha, Rais amesema kuwa maendeleo hayana chama na kuwa, vyama vya siasa visiwe sababu ya watu kugombana na kusababisha mvutano wa namna yoyote.

Kauli hiyo ya Rais imekuja wakati Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Mbunge Esther Matiko wakisota rumande baada ya kufutiwa dhamana na mahakama, kwa kukiuka masharti ya dhamana waliyopewa.

4​

IMG-20181127-WA0021.jpg
IMG-20181127-WA0013.jpg
IMG-20181127-WA0018.jpg
IMG-20181127-WA0020.jpg
IMG-20181127-WA0014.jpg
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, leo Novemba 27, 2018, anatarajiwa kuzindua Maktaba ya Kisasa na Kituo cha Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam almaarufu kama UDSM.


Hivi ni vitu uchwara vya kumshughulisha the so called Rais!
 
Warembo wa Kichina wamejifunza utamaduni wa Tanzania na wameamua kucheza ngoma wakati wa tukio la ufunguzi wa Maktaba, katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jambo hili ni zuri katika kufundisha tamaduni zetu kwa nchi rafiki. Hongera sana Wachina wa Dar es Salaam.
 
Warembo wa Kichina wamejifunza utamaduni wa Tanzania na wameamua kucheza ngoma wakati wa tukio la ufunguzi wa Maktaba, katika chuo kikuu cha Dar es Salaam. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo jambo hili ni zuri katika kufundisha tamaduni zetu kwa nchi rafiki. Hongera sana Wachina wa Dar es Salaam.
Siku mtakapogeuzwa kuwa wachina weusi ndipo mtakapotoa pongezi zaidi.
 
Back
Top Bottom