Uzinduzi wa Mahakama Jumuishi Dodoma

Uzinduzi wa Mahakama Jumuishi Dodoma

zandrano

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2017
Posts
8,569
Reaction score
9,513
Leo hii tarehe 6/10/2021 Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Samia S. Hassan anazindua Mahakama Jumuishi ambayo itarahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi wa Dodoma pamoja na viunga vyake.

Jambo moja la msingi ambalo tangu Hayati JPM atutoke Duniani ni Suala la matumizi ya Lugha ya Kiswahili katika mahakama zetu zote.

Hayati JPM alitamaani sana kuona mahakama zetu zote zinatumia Lugha ya kiswahili ktk mwenendo wa kesi na Hukumu zinazotolewa na hivyo kuhakikisha Sheria zinatungwa lkn jambo la kushangaza kasi ile imezima na sisi wananchi tunashangaa kuona Mahakama bado zinaendelea kutumia lugha ya kigeni/kiingereza, Je kwa nn hili linaendelea ?

Lugha ya kiswahili ni tunu kuuu ya Taifa letu sasa kwa nini inapuuzwa ktk kutoa haki za watanzania?!

Mhe. Rais Mama Samia wananchi wako tunaomba Lugha ya Kiswahili itumike ktk kutoa haki kwa watanznaia, Tunaomba mahakama zetu zote kuanzia Mahakama ya Wilaya, Mikoa mpaka Rufani zote zitumie Lugha ya Kiswahili ktk kuandika hukumu ili wananchi waelewe haki zao.

Nawasilisha.

Tangu nchi yetu imepata Uhuru miaka 60 Bado tunasuasua kutumia Lugha yetu ya Kiswahili katika kutoa Haki za watanzania!!
 
Kwanza Pongezi Kwa Mtendaji Mkuu wa Mahakaman pamoja na Jaji Mkuu Kwa kujenga majengo mazuri ya kutoa haki lkn bado Kilio CHA watanzania wengi ni pamoja na matumizi ya Lugha yao ya kiswahili.

Haki itolewe Kwa lugha ya Kiswahili na sio vinginevyo.

Naamini pia Moja ya sababu ZA ucheleweshwaji wa Haki ZA wananchi ni matumizi ya Lugha ya kizungu, sasa ni wakati muafaka wa matumizi ya lugha ya kiswahili.
 
wewe ongea kwa kiswahili sisi tutakujibu kwa kingerera.
mkuu hapo ndipo mashaka yanapo anzia.
yaani mimi niongee kwa kutumia lugha ya kiswahili halafu kwenye Hukumu nakuta kimeandikwa kizungu!!
kwa nini haswa iwe hivyo? na kwa malengo gani?!
tubadilike.
 
Mahakama jumuishi,hii ndio inakuwa vipi sasa...
Mahakama Jumuishi maana yake ni kuwa katika Jengo moja lenye gorofa tatu/nne litakuwa na mahakama za mwanzo, mahakama ya wilaya, mahakama ya Mkoa na Mahakama Kuu.
yaani ukitoka mahakama ya mwanzo unaweza kuingia wilaya, mkoa au mahakama kuu bila kupoteza muda.
hii onasaidia kupatikana kwa haki kwa haraka .
 
mkuu hapo ndipo mashaka yanapo anzia.
yaani mimi niongee kwa kutumia lugha ya kiswahili halafu kwenye Hukumu nakuta kimeandikwa kizungu!!
kwa nini haswa iwe hivyo? na kwa malengo gani?!
tubadilike.
usijali zitatolewa nakala mbili ya kiswahili na kingereza.
 
usijali zitatolewa nakala mbili ya kiswahili na kingereza.
hiyo nakala moja ya kiingereza ni kwa ajili ya Donald Trumph?![emoji1787][emoji1787] au nani?
mbona watanzania mnajipa kazi kubwa kiasi hicho!! hivi lengo ni nini?!
wananchi wanataka utekelezaji wa matumizi ya Lugha ya Kiswahili ktk kutoa Hukumu za wananchi kuanzia Mahakama za Mwanzo hadi mahakama za Rufaa.
 
ni kwa ajili ya mahakama na academicians.

nyie msiojua ngeli mtaishi na hiyo ya kiswazi.
 
Mtoa mada, sheria ina lugha yake Kama ambavyo fani ya utabibu, uinjinia au uhasibu zilivyo na lugha yake, Kuna maneno ya kisheria huwezi kabisa kuyaleta ktk kiswahili, by the way katika miaka yote hiyo 60 sijawahi kusikia mtu kanyimwa haki yake eti kisa Ni lugha inayotumika..acheni Mambo ya siasa katika fani za watu.
 
Lugha ya kiswahili ni Lugha ambayo imekuwa na imekomaa.

sio tu Tanzania bali zaidi ya mataifa 10 ktk bara la Afrika wanazungumza Lugha ya Kiswahili.

SADC hivi karibuni walishaamua kutumia Lugha ya kiswahili ktk kumbukumbu za vikao vyote lkn pia sheria zake zote zimeandikwa ktk Lugha ya kiswahili.

tuache kuwa hadaa wananchi, Lugha ya kiswahili ni Tunu ya Taifa Letu la Tanzania hivyo lazima tuiheshimu Lugha yetu.
 
ni kwa ajili ya mahakama na academicians.

nyie msiojua ngeli mtaishi na hiyo ya kiswazi.
Lugha ya Kiswahili ni Tunu ya Taifa.
Tuenzi tunu yetu hii.
Lugha ndio utambulisho wetu.
Historia inaonyesha kizungu kilitumika kipindi kile kwa kuwa Majaji walikuwa wazungu na walikuwa hawajui Kiswahili, sasa Leo hii Majiji na Mahakimu wote ni Waswahili wa kuzaliwa lkn bado wanang'ang'ana na kizungu. je ni kwa faida ya nani?!
 
Wasomi wetu wanaogopa lugha ya Kiswahili, wakiongea Kiswahili mtajuwaje kua nao wamesoma ngeli!?
 
Lugha ya Kiswahili ni Tunu ya Taifa.
Tuenzi tunu yetu hii.
Lugha ndio utambulisho wetu.
Historia inaonyesha kizungu kilitumika kipindi kile kwa kuwa Majaji walikuwa wazungu na walikuwa hawajui Kiswahili, sasa Leo hii Majiji na Mahakimu wote ni Waswahili wa kuzaliwa lkn bado wanang'ang'ana na kizungu. je ni kwa faida ya nani?!
Jina langu ndiyo utambulisho wangu sio lugha.

Nyie tumieni kiswahilli sisi tutawajibu kwa kingereza na mje na wakalimani wenu ili twende sawa.
 
usijali zitatolewa nakala mbili ya kiswahili na kingereza.
Na kwa nn zitolewe mbili!??,kwani kesi niza waingereza!!??,mbona tunalazimishana Mambo amabayo siya kwetu,!?basi basi wahamie mahakama za uingereza ,maana ndiko waliko walengwa wa hizo hukumu za kiingereza wanazozitoa.sisi waswahili watuachie majengo yetu na lugha yetu pendwa ya kiswahili. halafu wanajiita wasomi ,wasomi uchara hakuna lolote,Kama mnaogopa kutumia lugha yenu wenyewe ambayo umezaliwa nayo ,si ujinga huu!!!hopeless kabisa!!
 
sisi tunasoma kwa kingereza since standard 1,
nakala ya kingereza ni kwa ajili ya wanaojua kingereza na ya kiswahihi na kwa ajili ya msiojua kingereza.
 
sisi tunasoma kwa kingereza since standard 1,
nakala ya kiswahili ni kwa ajili ya wanaojua kingereza na ya kiswahihi na kwa ajili ya msiojua kingereza.
Basi jengeni mahakama za aina mbili,nyny masalia ya malkia muwe mnahukumiana huko,na ss waswahili tuwe naza kwetu! Tuone Kama mtapata wateja!!
 
mbona watanzania mnajipa kazi kubwa kiasi hicho!! hivi lengo ni nini?!
Kwa Tanzania sifa ndiyo inapewa nafasi kubwa, usipozungumza kiingereza wewe siyo msomi yaani unakuwa derecategorized😆🤌🤏
 
kwa kuwa Mahakama zote za Mwanzo nchini zinatumia Lugha ya Kiswahili, sasa sioni sababu Kwa nini Mahakama za Wilaya, Mikoa, Mahakama Kuu na Rufaa zisitumie Lugha ya Kiswahili wakati ni watanzania walewale walio anzia Mahakama ZA mwanzo ndio hao hao wanao endelea kutafuta Haki zao ktk Mahakama hizo?!
Kama kweli Majaji wetu na Mahakimu wetu lengo lao ni Kutoa Haki Kwa wananchi wa Tanzania basi hawana budi kutumia Lugha ya kiswahili ktk kutoa Haki za Wananchi.
 
Back
Top Bottom