Ebwanae naaaamZiwa kisiba Rungwe,Mbeya
Dah 😅Juu ya jiwe Gangilonga ,Iringa mjini...Picha ya pili ni Mtwa Mkwawa museum(makumbusho ya mkwawa ambapo kuna fuvu la mkwawa)
Yaani ndiyo sehemu ya kwanza kwenda Mungu akipenda, nimesikia taarifa zake 😋😋Ukirudi usikose kupitia na chemka hotspring, hutojutia.
Kwa uchache.I wish kufika Zanzibar,Hivi ni sehemu gani ntaenjoy zaidi nikienda, bajeti ni 300k🤔 naenda ijumaa kurudi jpili je itatosha? Napenda kuona wale watu wanaojirusha kwenye maji kutokea juu Hivi.
Mkuu apk , shukrani kwa kushare picha nzuri na mandhari ya vivutio tofauti vinavyopatikana nchini kwetu, nimependa picha za lindi....mwisho wa mwaka huu nina road drive ya kusini mwa Tz nategemea kupita moja ya maeneo haya uliyoyaweka hapa.Lindi beach ,Lindi mjini
Sea view beach & resort (hotel) mchana na usiku..Picha yenye mtu ni ya karibu na soko la samaki(ferry) asubuhi jua linapochomoza
Kwa lindi mjini kuna kaview kazuri kipindi bahari imerudi nyuma na kuna jua ila kipindi cha mvua panaboa hasa......Pamoja mkuu..
Nilienda mwaka Jana huko,aisee ni kuzuri, kwenye kushuka sasa huko bondeni ndo ilikua shughuli,lakini tulienjoy Sana .Mandhari nzuri na baridi la kwenda.Mad Max utoke huko mjini kwenye joto.
Mkaribie na Napuru waterfalls- Meru Camp
View attachment 2934874View attachment 2934875
Ahsante sana mkuu, kwa hako ka bajeti kangu ntatoboa kweli? Au niendelee kujipanga🙆♀️Kwa uchache.
Zanzibar
Kuna Upande wa town, Stone town......
Hapa kuna utajiri wa kihistoria kuanzia magofu ya mji mkongwe wa stone town uliojaa mali kale za tamaduni ya bara la asia, tamaduni za wazawa na historia ya utamaduni wa "waswahili" wa pwani, vyakula (forodhani), viungo asilia (karafuu, amdalasini, hiriki), michezo na matamasha (Sarakasi, Sauti za busara, mwaka kogwa n.k)
Upande wa Shamba
Huku ndio upande wa beach nzuri na mahoteli mengi ya kitalii, snorkeling & diving sites, activities kama kuogelea na dolphin, kasa n.k hupatikana upande huu.
N.k kutembelea shamba inahitaji uwe na bajeti nzuri zaidi kuliko Stone town.
Service na customer care bado ni changamoto maeneo mengi ya vivutio vya utalii mkuu.Mla Bata
Huku ni kuchele ya kitunda..Nilipapenda pamepoa..Zaidi sana waliopo ni wavuvi wako bize na kazi zao..Nimekumbuka pia kuna balcony moja walikuwa wanatengeneza kipindi hicho nadhani sahivi patakua pazuri zaidi kuongezeka kwa vikorombwezo hivyo.Beach ni nzuri na ni safi ila huduma za kijamii ndio kama zimekaa kushoto kidogo.
Kama sikosei umesema wastani wa siku mbili/tatu si ndio?Ahsante sana mkuu, kwa hako ka bajeti kangu ntatoboa kweli? Au niendelee kujipanga🙆♀️
Hapa nililala February kwa 50,000 ni jengo la zamani ila si mbaya. Nashauri budget ya accomodation aweke kuanzia 50,000 ndio standard. Huku ni juuKama sikosei umesema wastani wa siku mbili/tatu si ndio?
Hapo bajeti itakuwa kipengere mkuu, labda kwa kujibana mnoo na usitake makuu 😂😂.
Ngoja tuanze kubreak down.....300k Tsh.
- Nauli kwenda/kurudi , 🚢 daraja la kawaida- 35k x 2 = 70k
- Accommodation 🛌 - Hapa ndio mtiti sana, kwa zanzibar kupata malazi kwa bei nafuu ni issue hasa kipindi cha high season ambapo wageni wanakuwa ni wengi sana, nashauri kwa bajeti hiyo muda mzuri ni wa low season, kipindi hiki ni kizuri tena ni vema ukatumia applications kama airbnb, booking.com kufilter accommodation kutokana na bajeti yako. Nimeattach baadhi ya accommodation zenye bei nafuu kwa kipindi cha low season kutoka airbnb na booking.com.Hapa tuweke bajeti kuanzia 45k (Tsh) per night x 2= 90k laki ishakata hapo 😂😂
N.B: Mitandao mingine ya kupata malazi ya bei nafuu ni pamoja na agoda, homestay, hostelwords n.k hizi wenzetu wazungu wanatumia sana hasa wale solo travellers, packpackers na wasafiri wengine wa bajeti nafuu.
Kama utakuwa stone town muda wa jioni utahitaji kwenda forodhani kupata misosi, gharama za usafiri ni kama bara, boda boda ya kukutoa hotelini na kukurudisha kama accommodation itakuwa mbali. Mimi mara nyingi huwa kuna chimbo langu lipo karibu na bandarini nikifika S.town lazima nilale hapo na sihitaji usafiri kufika sehemu nyingi, ni mwendo wa "andha kanoon" tu kukata mitaa ya mji mkongwe kwa miguu.
- Chakula 🍲🥘🥂- Hapa nitakuachia wewe mwenyewe kutokana na ulaji wako. Ila naamini huwezi kumaliza laki kwa siku mbili/tatu.
Sasa mpaka hapo tumeshaona malazi na usafiri ushagharimu karibia laki na 80, bado hujala, hujanunua zawadi kwaajili yako na uwapendao (not important though) ila kuna jambo la msingi hupaswi kulikosa uwapo S.town. si jingine bali ni....
- Excursions- Ukiacha kutembealea maeneo kama Old slave market kwaajili ya kuona historia ya biashara ya utumwa, kukatisa mitaa ya stone town kujionea mandhari mazuri ya magofu ya kale, ngome kongwe na vivutio vingine vinavyopatikana katikati ya mji ambavyo vingi havina gharama Ni vyema ukatenga kiasi cha pesa kwa ajili ya kutembelea vivutio kadhaa ambapo utahitajika kuwa na kiasi fulani cha pesa.
Hapa kwa mTZ si chini ya elfu 80K Tsh kama utashare usafiri (boat) na wenzako.
- A day trip to (Changuu) "Prison Island" & "Nakupenda beach" -Changuu/ Prison island kisiwa kidogo kilichojitenga, utapata kujua historia yake lakini pia utaweza kujionea kobe wakubwa wenye umri mpaka miaka 200 wanaopatikana hapo, vile vile utaweza kwenda kutembelea beach nzuri ya "nakupenda" kama ni mpenzi wa snorkeling basi hapa ni mahala pake, packae huhusisha chakula (sea food plata, viazi mbatata mkaango, matunda na soft drinks) kabla hujamaaliza trip yako.
Mpaka hapo utakuwa umepata mwanga wa bajeti kiasi gani utapaswa kuandaa, NB: Hii ni breakdown ya kujibana sana (budget) ila ukitaka makuu ya kwenda kulala 5 star hotel, Boat First class chakula 3 courses kazi kwako😂😂 .
Nina imani nitakuwa nimekupa ABCs za kutosha kwaajili ya safari yako, kama kuna cha kuongezea basi wengine watakuja kuongezea. Elli apk Mshana Jr Depal Paula Paul RRONDO
Sio mufindi.. mashamba ya chai Uniliver?