Uzi wa kuishauri serikali sehemu ya kupata mapato!

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,938
4,354
Kwa vile serikali inahangaika sana ni vipi itapata mapato na kwenda mbali kuweka tozo zinazoumiza wananchi. Nimeona nifungue uzi wa kutoa ushauri ni wapi “Mwigulu” akatafute mapato.

1. Serikali ilikua na mpango wa kuokoa pesa kwa njia ya kukodisha magari kwa viongozi. Huku tutapata pesa nyingi sana.

2. Kampuni kubwa nyingi hapa Tanzania zina “understate” mapato. Hii ni kwa sababu ya serikali imeamua kutoa vibali na ku renew visa za muda za wageni ambao wanakuja kwenye haya makampuni kwa ajili ya kucheza na mifumo. Huku tunakosa pesa nyingi sana.

Ongezeni nyingine...
 
Kwa nini mnafikiria tu kuongeza mapato na sio kuongeza ajira?

Wengi wakiwa na shughuli za mapato na Serikali nayo itapata zaidi.
 
1. Rais na Majaji waanze kulipa kodi

2. Serikali iache mchezo, iwabane kweli wafanyabiashara walipe kodi, Wafanyabiashara wengi wanachezea EFD machines, hawalipi kodi.

3. Kariakoo kuna Wachina wanaendesha biashara , wanasuply mzigo kwa wafanyabiashara wa Kitanzania na wa nje na Wachina hawa wanakwepa kodi ajabu. Ukimuambia naomba risiti ya mzigo wangu anakwambia ondoka hata mzigo wenyewe uache!

4. Serikali iboreshe mifumo, yaani watu wahimizwe kutumia cashless system. Kwa sasa hivi tuna cashless system kama vile M-Pesa, Tigo Pesa etc, lakini hizi ziyo rafiki sana wa kufanya biashara sababu ya Makato na siyo userfriendly kivile. Serikali Itengeneze mfumo kama wa Wachina wa WECHAT MONEY ili watanzania waanze kuuziana bidhaa kupitia cashless platform. Kwa mfumo huu mapata yaserikali yataongezeka hata mara TATU kwa sababu hata buashara ndogondogo zitavutiwa kutumia huu mfumo na matokeo ya serikali itaongeza uwanda wa kodi kwa kiwango kikubwa sana. Mwigulu sikia, Fanya juu chini uintroduce kitu kama WECHAT MONEY nchini. Lakini hakikisha inakuwa owned na kampuni ambayo serikali itakuwa na shares nyingi sana.

5. Tuna vyanzo vingi vya utalii, tuna milima ambayo haijaendekezwa kiutalii kama vile Uluguru, Udzungwa,etc. Tuna maziwa madogo madogo kama vile Eyasi, Ikimba, na mengineyo, tuna visiwa vidogovidogo. Tuna beach kibao ktk ukanda wa bahari ya pwani hazijaendelezwa, nenda kimbiji DSM huko utaziona. Vyote hivyo vina potential ya kuingiza pato la Taifa.

6. Serikali inaweza kupata pesa nyingi kwa kubana matumizi. Ukubwa wa serikali upungue, Baraza la mawaziri na manaibu wao ni wengi sana, ni msigo kwa Taifa. Magari kama vile V8 siyo afya kwa matumizi ya pesa za mlipa kodi

7. Serikali irahisishe international transactions. Nashangaa mpaka sasa watanzania hawawezi kutumia PAYPAL. Pesa nyingi sana ya kigeni inashindwa kuja nchini kwa sababu watu wanakosa kupata gatway ya malipo yao yatokayo nje wakifanya huduma hasa za ubunifu mitandaoni.

8. Serikali iondoe urasimu wa vyama vya ushirika na itoe uhuru wakulima hasa wa mazao ya biashara walime wawezavyo, na watafute soko wawezavyo, Serikali isubiri kodi. Siyo kuwapangia wakulima bei ya kuuza mazao yao na kuwalipa miezi kibao ijayo!
 
Tuondoe sitting allowances zote, kwani hao wachache wanaopata wote wako kazini na ni kazi yao kutatua changamoto za kazi. Je, wafanyakazi wengine walio kazini hawalipwi chochote. Na wabunge nao wasilipwe chochote kwani tumeboresha mishahara yao waitumie hiyo kwani ni kazi waliyoomba, ukiondoa allowances zote tutaweza kupata fedha nyingi kuliko kumbebesha mwananchi mizigo yote.
 
NInakazia Kila mtu kulipa kodi kwa yote anayopokea kama malipo.

IMG_20220901_210256_685.jpg
 
Tuwashauri bure au watatulipa?

Hujui kuna watu wameajiriwa na wanaishi Oysterbay na kutumia ma V8 kwa kazi ya kufikiria vyanzo vya mapato? Kila mtu afanye kazi yake na anaeshindwa aachie ofisi
Dah!🤣🤣🤣🤣
 
Kwa vile serikali inahangaika sana ni vipi itapata mapato na kwenda mbali kuweka tozo zinazoumiza wananchi. Nimeona nifungue uzi wa kutoa ushauri ni wapi “Mwigulu” akatafute mapato.

1. Serikali ilikua na mpango wa kuokoa pesa kwa njia ya kukodisha magari kwa viongozi. Huku tutapata pesa nyingi sana.

2. Kampuni kubwa nyingi hapa Tanzania zina “understate” mapato. Hii ni kwa sababu ya serikali imeamua kutoa vibali na ku renew visa za muda za wageni ambao wanakuja kwenye haya makampuni kwa ajili ya kucheza na mifumo. Huku tunakosa pesa nyingi sana.

Ongezeni nyingine...
Kuna jambo Moja linafanyika sijui kama limefanyiws utafiiti hebu tujiulize biashara inayofanywa na wamachinga ni asilimia ngapi ya biashara ya rejareja ,kama ukipata jibu ujue ndio kiasi Cha Kodi inayokwepwa/,ni dhahiri Hawa chinnga hizo bidhaa wazipata Toka kwa walipa Kodi wakubwa .hata bajaji,boda boda,ni Mali ya wenye nacho na si za walala hoi,biashara za mama ntilie zimeuwa biashara za hotelli,sherria yoyote ya Kodi inayobagua(discreminative) ni lazima itasababisha serikali kukosa mapato.
 
Hapa atatafuta ugomvi na kutukanwa tu na wenye mitaji yao
 
Manunuzi yawe reflected moja kwa moja kwenye Tin, bila kuingiza Tin ya mnunuzi efd machine isiweze kutoa risiti.
Ili ufiche mauzo lazma uweze to kuficha manunuzi, Sasa ikiwa manunuzi hayafichiki tutaona namna watu walio kwenye informal sector au hela haramu na rushwa wanavyotumia kipato hivyo tutapatapo kodi
 
Kuna kitu kimoja naandika kwa herufi kubwa..

SERIKALI ITUMIE GARI ZA KAWAIDA LANDCRUISER HARDTOP...
WAACHANE NA V8 INA GHARAMA KUBWA SANA..

V8 zibaki kwa Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika.. Na watu wachache sana..
Mawaziri wote... Wakurugenzi, wakuu wa wilaya.. Majaji IGP nk ni HardTop tu

Serikali ikifanya hivi itabakiwa na kiasi kikubwa cha fedha kwa shughuli za maendeleo
 
Back
Top Bottom