Uzi: Viwango vya mishahara na mawazo ya kimaendeleo

Top Boy

Member
Jul 15, 2022
16
77
Wazima Wote?!

Kama kichwa kinavyojieleza ndugu zanguni,

Leo ingekuwa vyema kama tukipeana mawazo ya kimaendeleo kulingana na kiwango cha mshahara mtu anachopata maana wapo wanao anza kazi na wapo wanaendelea kufanya kazi ila hawajui wafanye nini cha kimaendeleo au hawaoni faida ya mishahara yao kwenye maendeleo ya maisha yao.

Tungepata mawazo kulingana na Viwango hivyo hapo chini:

(Tshs): take home (unachopata kwenda nacho nyumbani)

300,000 - 499,999

500,000 - 699,999

700,000 - 899,999

900,000 - 1,000,000

Kulingana na research yangu asilimia kubwa ya Watanzania wa walioajiliwa iwe sekta binafsi au serikali wapo kwenye hizo scales hapo juu,

Ahsanteni
 
Binafs Huwa najibana sana hasa starehe Kwa umri wangu ndio muda wa wenyew lakini alhamdulillah vimenipita
Nachofanya karibia nusu ya mshahara ni savings ambazo Huwa natumia miez 5 had 6 kukusanya then nafanya ninachohitaji Kila muda ukifika
Inatak roho ngumu na ukatili Lakini muhimu kwangu ni chakula mavazi na malazi
Ukitaka kufika
1.acha kujilinganisha na watu wewe sio wao
2.ujana hauna maana kama utfaka utu uzima hujawekeza chochote
 
Sisi tuliojenga ninmwendo was ku top up tu mkuu!!

Wenye mishahara iliyotimia ni madams TU!

Sisi tunatop up tunajenga top up nyumba za biashara mwendo mdundo mkuu!!

Hiyo savings ni mateso sana!!labda Kwa madams lakini sisi men ni ku risk tuuuuu!!!
Ndo nimetoka Jana kutop up mzee baba muda si muda kibuda kitasoma January ninunue mifugo kama kawaida yangu M3 sawa na mbuzi 60, kati ya hao madume yatakuwa mengi
Kila mbuzi1 Tsh50,000/=

Baada ya mwaka atakuwa amezaa Watoto 2 au mmoja Kwa wastani.

Nauza woote wakubwa na Baki na hao Watoto. sikoswi Watoto 30+

Nikishauza na nunua mbuzi70 size Moja na mbuzi waliopo jumla watakua 100+

Baada ya miezi7-8 watazaa tenaa nauza wakubwa tu hapo sikoswi m15. Ndani ya miaka3 Tena bila stress.
 
Hesabu za abunuwasi hizi,yaani ulivyo calculate mdomoni unaweza kusema kweli Hela hii nenda field Sasa 😂
 
Binafs Huwa najibana sana hasa starehe Kwa umri wangu ndio muda wa wenyew lakini alhamdulillah vimenipita
Nachofanya karibia nusu ya mshahara ni savings ambazo Huwa natumia miez 5 had 6 kukusanya then nafanya ninachohitaji Kila muda ukifika
Inatak roho ngumu na ukatili Lakini muhimu kwangu ni chakula mavazi na malazi
Ukitaka kufika
1.acha kujilinganisha na watu wewe sio wao
2.ujana hauna maana kama utfaka utu uzima hujawekeza chochote
Acha namm nichukue huu ushauri hapa
 
Hesabu za abunuwasi hizi,yaani ulivyo calculate mdomoni unaweza kusema kweli Hela hii nenda field Sasa
Mkuu njoo inbox nikuonyeshe Kwa video wengine hatujui hata calculation Zenu ni vitendo tu Njoo kama unataka ku prove njoo uone inbox

Chap sasa
 
Ndo nimetoka Jana kutop up mzee baba muda si muda kibuda kitasoma January ninunue mifugo kama kawaida yangu M3 sawa na mbuzi 60, kati ya hao madume yatakuwa mengi
Kila mbuzi1 Tsh50,000/=

Baada ya mwaka atakuwa amezaa Watoto 2 au mmoja Kwa wastani.

Nauza woote wakubwa na Baki na hao Watoto. sikoswi Watoto 30+

Nikishauza na nunua mbuzi70 size Moja na mbuzi waliopo jumla watakua 100+

Baada ya miezi7-8 watazaa tenaa nauza wakubwa tu hapo sikoswi m15. Ndani ya miaka3 Tena bila stress.
Hao mbuzi wanakula upepo? Vipi gharama za kijana/vijana wa kuwahudumia?
Hapo sijazungumzia faini na ugomvi na majirani wanaolima, manake mbuzi walivyo wakorofi hawachelewi kuvuna shamba la mtu.
 
Nina miaka 4 nafanya ufugaji mkuu mwanzo changamoto ilikuwa fisi. Nikawazibiti Kwa kujenga Banda Bora na salama

Kijana wa kazi Kwa mwaka250k madawa chakula Wana chunga kienyeji wapo Kijijin na tumepakana na mstu mkubwa sana masika kama hii wanafunguliwa sa9 tu wanakula masaa2 wameshashiba vibaya mnoo mstu umenawili hatariii!
 
Sisi tuliojenga ninmwendo was ku top up tu mkuu!!

Wenye mishahara iliyotimia ni madams TU!

Sisi tunatop up tunajenga top up nyumba za biashara mwendo mdundo mkuu!!

Hiyo savings ni mateso sana!!labda Kwa madams lakini sisi men ni ku risk tuuuuu!!!
Umetop up mpaka sacos na haufi wala nin, slip mapengo matupu na wazee wanadunda
 
Nina miaka 4 nafanya ufugaji mkuu mwanzo changamoto ilikuwa fisi. Nikawazibiti Kwa kujenga Banda Bora na salama

Kijana wa kazi Kwa mwaka250k madawa chakula Wana chunga kienyeji wapo Kijijin na tumepakana na mstu mkubwa sana masika kama hii wanafunguliwa sa9 tu wanakula masaa2 wameshashiba vibaya mnoo mstu umenawili hatariii!
Iko vizuri, vipi kuhusu magonjwa? Hawaumwi?
Natamani kufanya hiyo mishe.....Ila huwa naogopa na hii jinsia yangu sitaweza rabsha zake.

Bahati mbaya mume wangu hayupo interested na ufugaji..... proposal yangu kaiweka kapuni.
 
Ndo nimetoka Jana kutop up mzee baba muda si muda kibuda kitasoma January ninunue mifugo kama kawaida yangu M3 sawa na mbuzi 60, kati ya hao madume yatakuwa mengi
Kila mbuzi1 Tsh50,000/=

Baada ya mwaka atakuwa amezaa Watoto 2 au mmoja Kwa wastani.

Nauza woote wakubwa na Baki na hao Watoto. sikoswi Watoto 3
Nina miaka 4 nafanya ufugaji mkuu mwanzo changamoto ilikuwa fisi. Nikawazibiti Kwa kujenga Banda Bora na salama

Kijana wa kazi Kwa mwaka250k madawa chakula Wana chunga kienyeji wapo Kijijin na tumepakana na mstu mkubwa sana masika kama hii wanafunguliwa sa9 tu wanakula masaa2 wameshashiba vibaya mnoo mstu umenawili hatariii!
0+

Nikishauza na nunua mbuzi70 size Moja na mbuzi waliopo jumla watakua 100+

Baada ya miezi7-8 watazaa tenaa nauza wakubwa tu hapo sikoswi m15. Ndani ya miaka3 Tena bila stress.
Nunua ng'ombe ndama walau wa laki 3 baada ya miakq mitatu unauza laki 8 faida kilo 5,wanaokushangaa hawajui tu,kama upo location nzuri eneo la malisho lipo ufugaji wa malengo unatoa sana
 
Iko vizuri, vipi kuhusu magonjwa? Hawaumwi?
Natamani kufanya hiyo mishe.....Ila huwa naogopa na hii jinsia yangu sitaweza rabsha zake.

Bahati mbaya mume wangu hayupo interested na ufugaji..... proposal yangu kaiweka kapuni.
Wanaumwa lkn Kwa kiwango kidogo sana na hii imenifanya hatanisiweke kumbukumbuka za madawa madawa yanayotumika sana ni ya minyoo na kuogesha (kupe, utitiri,viroboto)
 
Nina miaka 4 nafanya ufugaji mkuu mwanzo changamoto ilikuwa fisi. Nikawazibiti Kwa kujenga Banda Bora na salama

Kijana wa kazi Kwa mwaka250k madawa chakula Wana chunga kienyeji wapo Kijijin na tumepakana na mstu mkubwa sana masika kama hii wanafunguliwa sa9 tu wanakula masaa2 wameshashiba vibaya mnoo mstu umenawili hatariii!
Wewe jamaa kwa unyonyaji huo ni hatari. Yani unamlipa mfanyakazi wako katika uwekezaji wako wa millions, elfu 20 kwa mwezi?
 
Makubaliano mkuu. Tena yeye anafaidi sana kwangu. Maana hatoi jasho!

Nitaelezea makubaliano ya Mimi na yeye na wazazi wake ilikuwa 150 k Kwa mwaka ila nilipoona ananidhamu nikapandisha Hadi Hela hiyo!(250k)

Ukumbke mbuzi Huwa anawaachia tu mlimani Hadi sa12:30 jion wanajirudisha wenyewe kiangazi ndo Huwa anawachunga Kwa masaa6 Kwa siku! Lkn Kwa Sasa ni masaa2-3 tu Kwa siku maana majani ya miti ni mengi sana. Kazi yake kuu kuwafungulia na kuwafungua WAKIRUDI na kuhakikisha wamerudi wote!

Bado Hela hiyo ndgo mkuu? Namvalisha na kumlisha pesa ya mtumizi juu yangu akiumwa Mimi Hadi wazaz wake natuma Hela ikibidi bila kukata mshahara wake?
 
Back
Top Bottom