Uzi special wa nukuu mbalimbali kila siku

Uzi special wa nukuu mbalimbali kila siku

Mjusi Sharobalo

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2025
Posts
8,287
Reaction score
14,592
Watu wengi wakati huu, Wamefikia malengo au kuishi katika ndoto zao kupitia maoni na ufahamu wa watu wengine, Uzi huu wa nukuu utaangazia hekima na busara mbalimbali zitakazo weza kutupatia mwanga katika maisha yetu siku za leo na baadae, Karibuni sana tujifunze. NB. Tupia nukuu uliyo nayo, Tujifunze kutoka kwako.
 
"Ndoto zetu zote zinawezekana ikiwa tutakua na ujasiri wa kufuata.' - Walt Disney, Mtayarishaji filamu wa Marekani (1901 - 1966)
 
"Ikiwa unapitia kuzimu, Endelea.' - Winston Churchill, Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza (1874 - 1965)
 
"Njia ya kuanza ni kuacha kuzungumza na kuanza kufanya.' - Walt Disney, Mtayarishaji wa filamu nchini Marekani (1901 - 1966)
 
1.Nzi hata ajitutumue vipi hawezi kuzalisha asali.
2.Nzi hata umuweke kwenye mzinga miaka 1000 hawezi kuzalisha asali.
3.Ishi kama nyuki ana mgawanyo wa majukumu,msafi na anazalisha bidhaa (asali).
4.Usiishi kama nzi akiamka tu anawaza mavi yako wapi-kutoka kwa mjomba wangu kipenzi.
 
Maisha ni safari isiyo na kurudi nyuma. Kila hatua, iwe ndogo au kubwa, huacha alama. Jifunze kuthamini safari yako, maana thamani yake ipo siyo tu kwenye mwisho wake, bali pia kwenye kila hatua unayopiga.
 
1.Nzi hata ajitutumue vipi hawezi kuzalisha asali.
2.Nzi hata umuweke kwenye mzinga miaka 1000 hawezi kuzalisha asali.
3.Ishi kama nyuki ana mgawanyo wa majukumu,msafi na anazalisha bidhaa (asali).
4.Usiishi kama nzi akiamka tu anawaza mavi yako wapi-kutoka kwa mjomba wangu kipenzi.
Unapoint usikilizwe
 
"Sisi ni kile tunachofanya mara kwa mara, Ubora, Kwahiyo si kitendo bali ni tabia.' - Aristotle, Mwanafalsafa wa Kigiriki (384 BC - 322 BC)
 
"Weka malengo yako juu, na usisimame hadi ufike hapo.' - Bo Jackson
 
"Hatari kubwa zaidi kwa wengi wetu sio kwamba lengo letu ni kubwa sana na tunakosa, lakini kwamba ni ndogo sana na tunafikia.' - Michelangelo
 
Back
Top Bottom