Uzi Maalumu wa Kuwakumbuka Bibi na Babu zetu..

Todito

Senior Member
Feb 6, 2013
154
357
Wakuu kwema?

Katika ukuaji wetu kiukweli ukitoa wazazi wetu, Bibi na Babu zetu walikua wakarimu wanyeyekevu na wenye upendo mkubwa sana.

Bibi yangu wakati wa likizo ilikua tukifika kijijin tu anatupokea kwa vigelegele na kuimba nyimbo za kilugha huku anaruka ruka na mara moja kuku atachinjwa wajukuu tunywe supu, Babu alikua mkali sana kwa wajomba ila sisi wajukuu tukifika atatupigia hadithi na kutuchekesha kila saa kama sio yeye

Vituko vya Bibi sasa ilikua akija mjini kutusalimia ni leo tu kesho ataanza kusema ng'ombe zake na mbuzi kijijin zinalia hazina majani mara kuku zake zitapotea ili mradi tu arudishwe kijijini.

Tutumie uzi huu kuwakumbuka ucheshi, ukarimu na vituko vya Babu na Bibi zetu na walipo Mungu awapumzishe kwa amani tu.
 
Uzi mzuri,binafsi,Bibi mzaa baba amefariki nikiwa mdogo kabisa,Babu mzaa Baba/Mama na Bibi mzaa Mama wote sikubahatika kuwaona,maana walitangulia mbele ya haki kabla sijazaliwa,Mwenyezi awalaze palipo pema InshaAllah...
 
Wakuu kwema?

Katika ukuaji wetu kiukweli ukitoa wazazi wetu, Bibi na Babu zetu walikua wakarimu wanyeyekevu na wenye upendo mkubwa sana.

Bibi yangu wakati wa likizo ilikua tukifika kijijin tu anatupokea kwa vigelegele na kuimba nyimbo za kilugha huku anaruka ruka na mara moja kuku atachinjwa wajukuu tunywe supu, Babu alikua mkali sana kwa wajomba ila sisi wajukuu tukifika atatupigia hadithi na kutuchekesha kila saa kama sio yeye

Vituko vya Bibi sasa ilikua akija mjini kutusalimia ni leo tu kesho ataanza kusema ng'ombe zake na mbuzi kijijin zinalia hazina majani mara kuku zake zitapotea ili mradi tu arudishwe kijijini.

Tutumie uzi huu kuwakumbuka ucheshi, ukarimu na vituko vya Babu na Bibi zetu na walipo Mungu awapumzishe kwa amani tu.
Bibi yangu alikuwa anataka niwe padre ila dah matarajio yameenda mbali kwa kweli, samahani bibi
 
Back
Top Bottom