Uzi kuhusu blogging

Uzi kuhusu blogging

ormystatus

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
262
Reaction score
464
Habari, kwanza nianze na lengo la mkeka uu ambalo ni
#To promote the brotherhood and collaboration among we tanzanian bloggers

Nlipitia nyuzi flan ambayo ilikuwa imeandikwa kwa umaridadi mkubwa na mtaalamu ambaye simfaham kwa jina,ilikuwa inahusiana na masuala ya blogging mengi yaliandikwa kwenye uzi ule lakn kwa ufupi inaonesha kuwa kuna bloggers wengi sana Tz ambao wanahitaji support kutoka kwa bloggers walioendelea ili nao waweze kufikia malengo, kama wanavosapotiana wenzetu wa nje kwa mfano wahindi huwa wanamagroup yao ya telegram ambayo yanakuwa na bloggers wa kutosha ndani yake wakipeana mbinu mpya na kuvisit kwenye blogs za wale wanaohitaji sapoti zaidi ili waweze kupata traffics wengi na mwisho watengeneze income, hivyo basi mtu ambaye ameguswa na mada atoe mawazo hapa nini kifanyike ili tuweze kupiga hatua wote kwa pamoja
 
1. Hakikisha niche yako una passion nayo. Usifanye blogging lengo kuu likiwa ni kupata pesa mwanzoni.

2. Fanya blogging kwa lengo LA kuleta impact Fulani katika maisha ya watu. Yaani gusa maisha ya watu kutokana na kile unachokiandika.

Pesa zitakuja either kupitia ads. Au watembeleaji wako watakutafuta na utaipata hiyo pesa.

Point ya msingi blogging fanya kwa nia ya kuleta mabadiliko fulani katika jamii yako, yaani ifanye kama daraja ya kuonyesha uwezo ulionao na watu sahihi watakutafuta kukulipa kutokana na uwezo wako. Usitegemee AdSense tu peke yake, ulimwengu umebadilika.

Unaweza kusanya pesa zaidi hata ile ambayo AdSense ingekupa kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom