Uzembe ni kukata tamaa

then mkuu,unashauri vp mfano mtu akifeli shule?
Kufeli shule si kufeli maisha watu wengi wanapofeli shule mnakata tamaa mnaona kama mmepoteza ndoto zenu....

Baada ya kukosa maksi za kwenda kidato cha kwanza au cha tano usianze kufikiria vitu hasi fikiria vitu chanya, kaa na familia yako ieleze kuhusu matokeo yako baada ya hapo wasikilize ushauri wao halafu changanua kwa umakini na kujua je wanachosema ni sahihi je watakachoniambia nifanye ntafurahia kama sitafurahia kipi ntakachofanya kitanifurahisha huku kinanipa mafanikio?...

Ukishafanikiwa kujua vyote hivi sasa chukua hatua sahihi ya kufanya hicho kitu kama unataka kuwa mfanya biashara anza kwenda semina mbali mbali za kuhusu biashara/ ujasiriamali hapa utajifunza mengi

Halafu baada hapo anzisha biashara yako kutokana na pesa yako, usifikirie kuanzisha bisahara kubwa kuliko mtaji wako utaishia kupanga tu na haitaanza na sikuzote biashara ya kwanza usitumie faida iwekeze faida kwenye biashara yaani faida utakayoipata iongezee kwenye biashara hii itakuza biashara yako .....


Ntaandaa mada pia kuhusu swala hili ndugu yangu usijali
 
Mi sitakata tamaa na nimejiandaa kufeli hata mara 10000 sembuse kufaulu?
Vzr kutokukata tamaa lakini usijiandae kufeli zaid amini katika kufaulu kufeli itokee kama ajali tu
 
Vzr kutokukata tamaa lakini usijiandae kufeli zaid amini katika kufaulu kufeli itokee kama ajali tu
Nina maana kuwa ntatumia makosa niliyoyapitia kama chanagamoto ya kunipeleka mbele,sifurahii makosa ila nikiyasahihisha yatanipeleka mbele katika shughuli shughuli zangu
 
Nina maana kuwa ntatumia makosa niliyoyapitia kama chanagamoto ya kunipeleka mbele,sifurahii makosa ila nikiyasahihisha yatanipeleka mbele katika shughuli shughuli zangu
Jambo zuri sana kujua ulipokosea na kurekebisha
 
Back
Top Bottom