Uzee: Maana, kuzuia uzee wa mapema,changamoto na jinsi ya kuwatunza wazee

xav bero

JF-Expert Member
Nov 24, 2016
5,134
7,307
Habari zenu wanajamii,
Namshukuru Mungu amenibariki na kupata vingi navyomiliki ambavyo havina mipaka wala pesa isiyoweza kuvinunua kuliko vingi nilivyonavyo ambavyo vinamipaka ambavyo pesa inaweza kuvinunua,,, imefika kipindi nautaman uzee.

Japo umri wngu bado sijafikisha hata miaka 40 lakini kila mara natamani sana niwe mzee,,,sasa sijui ni tatizo la kisaikojia au tatzo ni nini? Huwa nakua nafuraha sana nikimwona mzee ambae aidha amefanya kazi sana kuwajengea watoto wake msingi mzuri wa maisha,,wamekua wakubwa sasa wanamsaidia baba yao,kiukweli hua natamani sana kua katika hali hiyo.

============



Uzee au kuzeeka ni nini?
Uzee au kuzeeka ni hali ya mabadiliko ya kimaumbile, kihisia na kiakili inayotokea kwa mwanadamu kadiri umri wake wa kuishi unavyoongezeka. Mabadiliko haya huanza tangu mtu akiwa mdogo mpaka muda wake wa kuondoka duniani unapowadia.

Nini husababisha kuzeeka?
Mabadiliko haya ni matokea ya mambo makubwa mawili:
  • Vinasaba (genetics)
  • Mazingira
Dalili za kuzeeka
Kuzeeka huweza kuonekana kwa dalili mbalimbali, zikiwemo mwili kupungukiwa nguvu za utendaji kazi, kuchukua muda mrefu katika kufanya jambo fulani n.k. Pamoja na dalili hizi viungo mbalimbali vya mwili huweza kubadilika pia. ikiwemo:
  1. Ngozi
  2. Mfumo wa misuli na mifupa
  3. Mfumo wa Upumuaji
  4. Mfumo wa Moyo na Mishipa
Ngozi

Hiki ni kiungo muhimu kwa mwanadamu, kwani kina kazi kubwa ya kumkinga mwanadamu na athari mbalimbali za kimazingira zinazoweza kumdhuru . Ngozi hutengeneza kizuizi baina ya mazingira ya nje na mwili wa mtu. Na kuufanya mwili uweze kuhimili madadiliko ya hali joto, kuulinda mwili dhidi ya upotevu wa maji mwilini na dhidi ya mionzi hatarishi ya kutoka kwenye jua.

Kadiri umri wa ujana unavyoisha na kuingia umri wa utu uzima mabadiliko kadhaa hutokea kwenye ngozi ambapo unene na kina cha ngozi hupungua zaidi ya asilimia ishirini. Mishipa mbalimbali hupungua, seli hai pia hupungua ikiwemo na uwezo wa hisia wa ngozi kupungua kwa asilimia kubwa.

Uwezo wa kulinda mwili dhidi ya mabadiliko ya hali joto hupungua, ngozi huwa nyembamba sana na teketeke na uwezo wa kupona haraka hupungua. Tezi za jasho hupungua sana kwenye ngozi. Misuli na mifupa huweza kuonekana kirahisi chini ya ngozi kutokana na na mafuta yaliyoko chini ya ngozi kupungua sana.

Mfumo wa misuli na mifupa

Misuli hufanya kazi kubwa mwilini ya kuzalisha joto na kuupa mwili nguvu. Mfumo huu husaidia sana kazi ya kuzalisha nishati na kuupa mwili nguvu na ulingano (balance). Kadiri umri unavyoongezeka, misuli hupoteza nguvu kutokana na kupungua kwa tishu mbalimbali za misuli na hivyo mtu hupoteza nguvu na ulingano wa mwili na huweza kutembea kwa shida pia.

Mfumo wa upumuaji

Uwezo wa mapafu kufanya kazi hupungua kadiri umri unavyoongezeka. hii hutokana zaidi na misuli ya kifua na mfumo wa hewa na upumuaji kupoteza uwezo wake wa unyumbufu (elasticity and flexibility), kifua kuwa kigumu na kupungua kwa idadi na eneo la viriba hewa (alveolar surface area). Hali hii husababisha kupungua kwa ufanisi wa mfumo wa ubadilishaji hewa kwenye mapafu.

Mfumo wa moyo na mishipa
Kadiri umri unavyoongezeka na kuanza kuzeeka, mishipa ya kupitisha damu kutoka kwenye moyo kwenda sehemu mbalimbali za mwili (arteries) hukakamaa na kupoteza unyumbufu (elasticity) wake. Hii huipa moyo kazi ya ziada ya kusukuma damu ipite kwenye mishipa hii iliyokakamaa. Matokea yake ni kuongezeka kwa mgandamizo wa damu (pressure) , kutanuka kwa chemba za moyo na moyo kushindwa kufanya kazi.

Ukisikia mtu anaitwa mzee au tunasema amezeeka haya ni baadhi kati ya mabadiliko mengi yanayokuwa yametokea kwenye mwili wake.

katika hali ya kawaida hakuna dawa ya kutibu ya uzee, kwani hii ni hali ya kawaida kabisa ya kimaumbile. Lakini unaweza kusaidia kufanya mwili usizeeke haraka.

Kuna njia kadhaa zinazoshauriwa kuwa zinaweza kuzuia uzee wa mapema nazo ni:


1. Ulaji wa chakula chenye virutubisho vifuatavyo

Chakula chenye vitamini C
Utafiti uliofanywa kwenye kikundi cha wanawake wenye umri wa miaka zaidi ya 40 ulionyesha kwamba wanawake wanaotumia chakula chenye vitamini C zaidi walikuwa na mikunyanzi (wrinkles) kidogo zaidi na ngozi zao hazikuwa kavu ukilinganisha na wale ambao walitumia vitamini hiyo kidogo. Hii ni kwa sababu vitamini C ni antioxidant yenye nguvu inayozuia uharibifu wa seli na DNA za seli hivyo kulinda uzalishaji wa collagen ambayo ndiyo nguzo muhimu ya kulinda ngozi yako.





Unashauriwa basi upate angalau mg 75 za vitamini hii kwa siku. Kwa mfano unaweza kupata chungwa moja wakati wa kifungua kinywa na piliplili tano za njano ndani ya saladi kwenye mlo wako wa mchana. Chakula chenye vitamini C kwa wingi ni broccoli, strawberries, pilipili nyekundu, nyanya, tikitimaji, pomegranate n.k.

Chakula chenye protini
Tafiti zilionyesha kuwa wanawake waliotumia protini zaidi walikuwa na wrinkles chache zaidi kwenye ngozi zao kuliko wale ambao walitumia proteni kidogo, hii kwa sababu proteni hutoa viungo muhimu katika ujenzi wa collagen.

Ili upate proteni unashauriwa kula nyama ya kuku isiyo na ngozi, sehemu nyeupe ya mayai na samaki. Unapochagua kula nyama ya ng’ombe au nguruwe, pendelea kutumia ile isiyo na mafuta sana. Matumizi ya soya yameonyesha kusaidia kuondoa ile mistari myembamba kweye macho.

Samaki wenye mafuta
Samaki wa baharini wenye mafuta wamebainika kuwa na kiwango kikubwa cha “omega-3 fatty acids”, kitu ambacho husaidia kuilinda ngozi yako kutokana na mionzi mibaya ya jua ambayo hudhoofisha collagen.



Nafaka nzima
Utumiaji wa nafaka nzima badala ya wali mweupe, mikate inayotokana na ngano nyeupe na nafaka nyingine zilizokobolewa una faida nyingi. Moja ni kuzuia mwongezeko wa insulin katika mwili ambayo ina madhara ya kuharibu ngozi. Pia nafaka nzima ni chanzo cha madini ya selenium ambayo husaidia kuikinga ngozi yako kutokana na mionzi ya jua (UV rays).



Unashauriwa kutumia brown rice, shayiri na ngano nzima ili uweze kupata madini haya yatakayokusaidia kulinda ngozi yako.

Green tea
Green tea ni kinywaji chenye antioxidants nyingi. Unywaji wa vikombe viwili au vitatu kwa siku wa chai hii utaifanya ngozi yako kuwa nyororo. Chai hii pia huzuia mikunyanzi isitokee kwenye ngozi yako.

2. Mazoezi ya viungo
Mazoezi ya viungo husaidia kufanya mwili kuwa na ukakamavu, na mazoezi yanayoshauriwa hasa kwa wale ambao umri kidogo umeenda ni yale ambyo hayachoshi sana mwili.

3. Matumizi ya vipodozi visivyo na sumu
Kuna vipodozi ambavyo vimetengenezwa na vitu asilia kama matunda kwa ajili ya kuondoa mikunjo ya uso, hivi hushauriwa kutumika ili kuondoa mikunjo ambayo huanza kuonesha dalili za uzee, pia kunyoa nywele ambazo zimeweka mvi.

Baadhi ya matatizo yaambatanayo na uzee:
  • Kupungukiwa maji mwilini- Binadamu unapofikia uzeeni, mwili wake huhitaji maji mengi zaidi kuliko wakati wa ujana, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kupata choo kwa taabu sana (Constipation), jambo ambalo huchangia kuongeza ndita usoni mwao kwa maumivu,pia misuli ya kuchuchumaa huchoka kiasi kwamba hawahitaji mda mrefu kuchuchumaa kujisaidia.
  • Ini kushindwa kufanya kazi yake: kutokana na mikiki mikiki ya dunia katika ujana wao, wazee wengi hukumbwa na tatizo la ini kushindwa kufanya kazi yake, tatizo ambalo hupelekea miguu kuvimba pengine kupata maumivu makali ya mgongo n.k
  • Magonjwa mengi kama Kupooza na kisukari: Uzee unakuja na magonjwa kama hayo kutokana mwili kutofanya kazi ipasavyo.
  • Kiwango cha Ute kwenye mifupa hupungua: hii mtu anapofikia uzee uzalishaji wa ute hupungua, tatizo ambalo huchangia mifupa kusagana kirahisi kwenye maungio kiasi kwamba mwili hushindwa tena kusimama wima kama mwanzo, hilo hupelekea wazee wengi kupinda mgongo na wengine kutafuta magongo ili kuupa mwili msaada.
  • Akili huanza kuwa kama mtoto: Kutokana na mwili kuchoka pia na akili huchoka kutokana na kukosa mzunguko mzuri wa damu na oksjen ya kutosha, hii hupelekea akili kushindwa kufikiri na kutoa maamuzi sahihi, jambo ambalo hupelekea wazee wengi kuhitaji msaada kutoka kwa vijana.
  • Macho na masikio kuwa hafifu!: kutokana na ubongo kupoteza kumbukumbu basi huathiri hadi macho na masikio kupungua nguvu hivyo ni vyema kuongea na wazee kwa mbele huku tukiwa tunawatazama usoni ili kuwaongeza faraja .
  • Macho kuwa mekundu: wazee wengi wameuwawa kisa macho kuwa mekundu kwa tuhuma za kichawi lakini ukweli ni kwamba macho mekundu huchangiwa na moshi mkali pamoja na kukosa usingizi, Moshi wa moto hususani wa kuni na kibatari huchangia kwa kiasi kikubwa, Vibatari vingi huko kijijini vinatumia diseli kuriko mafuta ya taa, hii huongeza maumivu kwenye macho.
  • Midomo kulegea, zipo changamoto nyingi hutokea mwili unapolegea, maumivu makali yatokanayo mwili kukosa maji na ute huzalisha matumizi ya Ugolo na Tumbaku, jambo ambalo hulegeza midomo na taya.
  • Usiri; kutokana na upungufu wa nguvu za kutafuta basi hupelekea wazee wengi kuwa watunzaji wazuri wa vitu pamoja na usiri (kuficha), Mzee akikufichia kitu ndani utapata tabu sana kukipata,wengine huficha vitu na kusahau mahali walipoficha, jambo ambalo hupelekea vitu hivyo kuoza au kupotea
  • Kusali; kutokana na kukata tamaa basi njia pekee wazee ni ile ya kujiandaa na kifo kwa kuwa wacha Mungu kwelikweli;
Dokezo: Hivyo basi Ukiwa kama kijana jifunze kuwaheshimu wazee kutokana na changamoto hizo, ni vyema kujiandalia Uzee mwema.
  • Wapishe wazee kwenye huduma mhimu ambazo zitawapunguzia maumivu ya kusimama mda mrefu kusubiri huduma.
  • Wazee unapowaona wamekosea Tumia usitaarabu kuwaelekeza kwasababu vile wao wanavyopungukiwa akili basi tambua kwamba ndivyo wewe unavyoongezeka akili.
Mambo ya kuzingatia unapoishi na wazee
  • Kutokana na mfumo wa mmeng'enyo kupungua kasi kwa umri ni vyema sasa tukawapa wazee wetu vyakula vya matunda na mbonga mboga nyingi katika uzee wao.
  • Punguza mwanga mkali eneo ambalo mzee ana lala ili apate usingizi.
  • Ili kuamsha ubongo wao, hakikisha unawapatia michezo ya kuamsha bongo kama bao na draft ili kushtua bongo zao.
  • Waache wazee wacheze na wajukuu kwa wingi hii huwapa faraja na kuondoa upweke,
  • Ni vyema kuishi na wazee mbali na mji/kijijini ili kupata sehemu tulivu.
  • Usimkataze mzee wako anapofagia au kulimalima hapo nyumbani ukidhani anadhalilika, tambua hiyo ni sehemu ya tiba kubwa mno kwake muache afue, na afanye usafi apendavyo yeye.
  • Ikiwezekana mjengee nyumba mzee pembeni ili awe huru kabisa peke yake muulize kama anapenda kupika mnunulie jiko ili apike michicha na mbogamboga hii itamuongezea uwezo na ari ya kuishi vizuri.


Michango ya wadau:
----
----
 
Dah..
Uzee ni hali fulani ya kuchoka kwa mwili.... na umri ni muda fulani ambao mwili umeishi....Hakuna anayependa uzee... Ila umri haukwepeki... Japo dada zetu wengi hujaribu kukwepa umri...

Unaweza kukutana na mtu mwenye miaka 29 ukadhani ni mstaafu wa serikalini miaka 4 au 5 iliyopita.... au ukakutana na mstaafu ukadhani Labda ni Bavicha au Uvccm anayesubiri matokeo...
Uzee ni hali ambayo mwili hushindwa kufanya yale matendo uliyoyaweza wakati wa hali ya ujana.. kama kulima... kukimbia.. hata kupiga gem..

Uzee wa haraka unaepukika.... sio kwa kupunguza umri ulio nao... Bali kwa kula chakula bora na kufanya mazoezi ya mwili
Tupige vita uzee wa haraka 2017
 

Attachments

  • age.mp4
    3.7 MB · Views: 38
Naskia meditation inafanya mtu kuzeeka Ila sio kweli meditation isiyo ya kizembe inaweza kukufanya ustay energetic Muda wote ukiwa na nguvu mazoezi na Kula matunda Kwa wing zinapunguza muonekano wa kuzeeka.
 
Habari za asubuhi wapendwa,

Kuna wakati nilipata mwaliko wa kwenda nchini Uganda, tulifika Kampla na kupokelewa na mwenyeji wetu. Tulikuwa kikundi cha watu watano, tulipelekwa kwenye hoteli tuliyoandaliwa na kuambiwa tujiandae, baada ya masaa mawili mwenyeji wetu atarudi kutuchukua kwa chakula cha jioni.

Nyumbani kwa mwenyeji wetu ile karamu ilikuwa ya kukata na shoka, kulikuwa na vyakula vingi kuanzia; matoke, wali, samaki sato, nyama ya mbuzi (choma), mbuzi mchuzi, chapati, salad, matunda, nuts na vinginevyo. Katika kujitengea chakula, kaka mmoja nilimuona anakula salad tu, baada ya chakula tulijiwekea matunda na story za hapa na pale ziliendelea.

Baadae niligundua kaka yule ni daktari, alinifahamisha alipata scholarship baada ya kumaliza form six kwenda kusoma medicine China, alipofika kule aliamua kubadili na kusomea Chinese Medicine na katika process ya kusoma herbs ndiyo aligundua uharibifu wa chakula katika harakati za mapishi mpaka kumfikia mlaji.

Daktari yule aliniambia kwa miaka takriban 25 ameacha kula chakula kilichopikwa, alipoanza ilikuwa ngumu lakini sasa hivi hawezi tena kula chakula chochote kilichopitia moto. Kwa muonekano yule daktari anaonekana ana miaka 35, nilishangaa aliponiambia ameshagonga 50 kama miaka miwili iliyopita.

Dieat yake:
Breakfast; embe na ndizi mbivu au papai na ndizi mbivu pamoja na kikombe cha mchanganyiko wa nuts hii ndiyo supplement ya protein. Chai na kahawa ni sumu kubwa ya mwili, kunywa maji tu ukimaliza kula hivyo. Kwasababu digestion ya matunda ni haraka, hakikisha una matunda yaliyotaarishwa na unaweza kula baada ya saa moja au masaa mawili.

Lunch;
Kabich lililokatwa katwa, matango (cucumber), nyanya, unaweza kuweka limao kwa ladha pia ni source ya vitamin C, vipande vya mhogo au viazi vitamu unatafuna vibichi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts unamalizia na maji.

In between hakikisha unaandaa matunda na cucumber kama bites kwasababu digestion inakwenda haraka.

Dinner;
Carrots zilizokatwa katwa, kachumbari ya nyanya kitunguu na cucumber unanyunyiza olive oil kijiko kimoja cha chakula, nanasi na kikombe cha mchanganyiko wa nuts na glass ya maji.

Wengine wanafanya water therapy yaani in between meals wanakunywa maji haya yanasaidia pa kutokusikia njaa.

Ukianza hivyo hutaweza kuwa na excess fat.
 
mimi nimeanza hiyo!
siku ya 14.
sijaweza ile straight of cuz mwanzo mgumu lakini ndo naelekea huko!
next month ntakuwa mwaminifu zaidi!
ILA INAWEZEKANA KABISA!
NAKULA SALADS,SMOTHIES ,MATUNDA,MTINDI,NUTS MAJI NA NAFANYA MAZOEZI!
usiku nalala tumbo kama limeondolewa,jepesiiiiii!
 

Attachments

  • 17021997_1253753004661132_1318604302822719328_n.jpg
    53.3 KB · Views: 80

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…