Kizazi cha wazee vijana wasio na hekima kinakuja

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515
Habari wakuu,

Husika na kichwa cha habari tajwa,

Vijana wengi wamekuwa hawataki kuzeeka na imefika mahali wamekuwa wakiona uzee hauna maana kwao.

Wengine wamekuja na majina kabisa kwamba uzee mwisho chalinze.

Ukitazama wazee wa zamani walikuwa ni wazee wenye hekima na busara.

Ila ukitazama wazee wajao watakuja kuwepo wale wazee ambao ni wazee ambao hawajui kuwa ni wazee.

Wanajiita wazee vijana, yaani wanakuwa na uzee na kijana ndani yao.

Ni wazee ila wanafanya mambo ambayo ni ya vijana na wanaona sawa.

Sio kwa kuongea kwao tu hata mavazi ya wazee wa Sasa Yana ujana ndani yake.

Utakuta Mzee mzima anaongea kama kijana wa mdogo.

Hajui lipi la kuongea lipi akae kimya, maana amekosa busara za uzee.

Hajitambui kuwa yeye ni mzee na muda umepita analazimisha kuwa kijana.

Hajui lipi la kushauri vijana maana analazimisha kuwa bado yeye ni kijana.

Si wazee wanawaume tu hata wazee wanawake wapo.

Tutapata wapi wazee wenye hekima?

Kizazi cha wazee wasiojitambua kuwa muda wao wa ujana umepita na wakubali kuwa ni wazee kinakuja...
 
Its not us ni utandawazi umeibadiliasha jamii lakini uzee humfanya mtu kuacha mambo ya ujana automatic maana anajiona jamii itamshangaa.. mfano mzee wa miaka 80 kwenda club automatically anajiona sio busara na jamii itamshangaa pisi kali zitamkimbia na anajiona yupo njee ya muda hana budi kwenda tena anabaki mtu wa kushida nyumbani au aende live bend,
 
Mkuu naona umekuja na Uzi kuua Uzi wangu...

Ungecomment hapa jamani
Hapana sijaja kuua bali nimekuja kukazia hoja za uzi wako.

Unajua kuna wazee wa hovyo sana watatokea huko mbeleni, hawana hekima, wasiojua kushauri, wahuni, ni wazee lakini wanajiita ni vijana ilhali hata nguvu za kiume kama za ujanani hawana.

Nakazia uzee hauepukiki.
 
Hapana sijaja kuua bali nimekuja kukazia hoja za uzi wako.

Unajua kuna wazee wa hovyo sana watatokea huko mbeleni, hawana hekima, wasiojua kushauri, wahuni, ni wazee lakini wanajiita ni vijana ilhali hata nguvu za kiume kama za ujanani hawana.

Nakazia uzee hauepukiki.
Hapana ulitakiwa ukazie kwa Uzi wangu umekuja kibiblia, hata Mimi ningeweza kuweka kibiblia...

Ila nilitaka iwe hoja ijadiliwe kihoja...

Sasa wewe mbona hukuanza kuandika binafsi, umeiba Uzi wangu na ukauweka kidini...

Sijafurahishwa...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom