Uzanzibari usitumike kama kinga dhidi ya Watenda Maovu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
142,616
Reaction score
287,331
Angalizo: Uzi huu hauna mahusiano yoyote na Ubaguzi wa Rangi, Dini ama Ukanda, nimeuandika ili kutoa elimu tu kwa maono yangu.

Ni kweli kwamba Tanzania ni Nchi iliyotokana na muungano wa nchi mbili, marehemu Tanganyika na Zanzibar iliyo hai hadi leo, hizi nchi zote zilikaliwa na watu wake , tena wake kwa waume, wasomi na wasio wasomi.

Ni kweli kwamba Wazanzibar wanaruhusiwa kikatiba kuwa Viongozi wa Tanganyika (Muungano), bali Watanganyika hawaruhusiwi kuwa viongozi wa Zanzibar (kero ya muungano), hili kila mtu analifahamu, na nadhani linashughulikiwa.

Sasa ninachokiomba kwa viongozi wa Nchi hii, wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa, wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wapagani ni hiki, UZANZIBAR USITUMIKE KAMA KINGA DHIDI YA MAKOSA YA VIONGOZI WA KITAIFA WENYE KUTOKEA ZANZIBAR, kwamba sisi wakosoaji wa mambo mbali mbali ya msingi kwenye nchi yetu, tena ukosoaji wa kujenga, TUSIWEKEWE mipaka ya kumkosoa mtu kwa vile tu ni Mzanzibar, hata kama ametenda makosa au jambo baya linalopaswa kukosolewa, kitu hiki kinachotaka kupandikizwa kwenye nchi yetu kipingwe na kila mwenye dhamira njema ya kupinga maovu.

Ukosoaji wa madudu ya viongozi haukuanza leo, tulikosoa Nyerere na Viongozi wake, tulikosoa Mwinyi, Tukakosoa Mkapa, tulimpa za Uso Kikwete, tulikosoa Magufuli na Wapambe wake bila uoga wowote ule kwa vile tulikuwa na nia njema na nchi yetu, kwa hiyo tunapokosoa madudu ya leo tusionekane Wabaguzi, hatukosoi kwa Dini ya mtu wala kule atokako, TUNAHANGAIKA NA MAMBO ALIYOYAFANYA MTU AMBAYO TUNAONA KWAMBA NI MABAYA KWA MUSTAKABHALI WA NCHI.

William Lukuvi alisema maneno mengi mno ya kibaguzi kuhusu Zanzibar (Ushahidi umo humu JF), lakini hakuna kiongozi aliyepiga kelele, ndio kwanza akawa anateuliwa kwenye vyeo hivi na vile, nani amesahau? Mnataka tuamini kwamba Rais Samia alimtoa kwa vile aliibagua Zanzibar Wakati ule? La hasha, sisi wengine tunaendelea kuamini kwamba aliyemtoa alimtoa kwa kuzingatia utendaji wake.

Natoa wito kwa wale wanaotushambulia kwa kuwakosoa viongozi wanaotokea upande wa pili wa Muungano kwamba waangalie UKWELI WA HOJA ZETU badala ya kutaka kutufunga midomo.

Naomba kuwasilisha.
 
We chawa wa mbowe kamsikilize mbowe alivyombagua Samia kasema wazi wazi rais Samia na waziri mbalawa ni wazanzibar wameuza bandari za Tanganyika hawajagusa za Zanzibar
 
Kati ya maraisi wa kristo na maraisi waislamu mimi naona maraisi wakristo wanajua kazi ya uraisi na wanamchango mkubwa sana na pia hawana kujipendekeza kisa dini.

Haiusiani na ubaguzi ni ukweli na ukweli ni mgumu kueleweka mfano mwanamke hawezi kushika kiti cha uraisi lazima asaidiwe.
 
Sawa

Tanzania haina Udini ndio sababu kila Mtaa kuna Bucha ya Nyama ya Nguruwe
Nyama ya nguruwe ina shida gani hadi uitolee mfano? Bora kuku ama Samaki wasiuzwe Tanzania ila sio nguruwe. Niko tayari kujitoa mhanga pale watu watakapoleta ujinga juu ya kitimoto.

Yaani upate kutimoto choma ama ya kukaanga kavu, kachumbari iliyoandaliwa kwa umaridadi, ugali wa dona uliopokwa vizuri ukaiva, maji ya kunywa ya baridi halafu mtu alete ujinga eti kiumbe wake sijui anaitwa mungu hataki nguruwe, tutaonana wabaya.
Screenshot_20230613_170656_Instagram.jpg
 
Aiseeèe !!
 
Kwani kuna uongo hapo ?
Sasa unachotetea ni nini hapa kwenye thread yako? Mmekosa hoja za kuwaelewesha watz mmeanza kumshambulia Samia na mbalawa Kwa uzanzibar wao, nyie chadema ni wabaguzi wa kanda, dini na ukabila aiseee acheni ujinga mtatuharibia nchi nyie
 
Unaweza kukosoa pass kuacha viashiria vya ubaguzi.

Wengi wenu mnashindwa kukosoa kwani hakuna la kukosoa. Hivyo ili uonekane umekosoa unajikuta unatumia ubaguzi katika kukosoa...

Mpo wengi wa aina hii! Watu wa njia ya mkato....
 
Sasa unachotetea ni nini hapa kwenye thread yako? Mmekosa hoja za kuwaelewesha watz mmeanza kumshambulia Samia na mbalawa Kwa uzanzibar wao, nyie chadema ni wabaguzi wa kanda, dini na ukabila aiseee acheni ujinga mtatuharibia nchi nyie
nadhani hujaelewa uzi huu
 
nadhani hujaelewa uzi huu
Misukule ya mbowe mna taabu Sana Mie nafahamu kwanini umeleta thread hii, lkn Kwa sababu akili umemkabidhi mbowe ndo hujui kwanini akina waitara na kibajaji wanamshambulia mbowe ni sababu alishindwa kujenga hoja akaanza kumshambulia Samia na mbalawa Kwa uzanzibar wao nikuambie tu CCM hakuna anayemkingia kifua Samia na mbalawa sababu ya uzanzibar wao lahasha Ila tunalaani chokochoko za ukanda anazoeneza babu yako mbowe na lissu
 
Msikilize na babu yako lissu kakasa hoja ya kuwakataa do world kaanza propaganda ya uzanzibar na uzanzibara
 
Attachments

  • 5382328-99ec28d8a08ec3fb0f3ba0b553c66ff4.mp4
    7.5 MB
Ukosoaji wa madudu ya viongozi haukuanza leo, tulikosoa Nyerere na Viongozi wake, tulikosoa Mwinyi, Tukakosoa Mkapa, tulimpa za Uso Kikwete, tulikosoa Magufuli na Wapambe wake bila uoga wowote ule kwa vile tulikuwa na nia njema na nchi yetu, kwa hiyo tunapokosoa madudu ya leo tusionekane Wabaguzi, hatukosoi kwa Dini ya mtu wala kule atokako, TUNAHANGAIKA NA MAMBO ALIYOYAFANYA MTU AMBAYO TUNAONA KWAMBA NI MABAYA KWA MUSTAKABHALI WA NCHI.
Saluti mkuu
 
Angalizo: Uzi huu hauna mahusiano yoyote na Ubaguzi wa Rangi, Dini ama Ukanda, nimeuandika ili kutoa elimu tu kwa maono yangu.

Ni kweli kwamba Tanzania ni Nchi iliyotokana na muungano wa nchi mbili, marehemu Tanganyika na Zanzibar iliyo hai hadi leo, hizi nchi zote zilikaliwa na watu wake , tena wake kwa waume, wasomi na wasio wasomi.

Ni kweli kwamba Wazanzibar wanaruhusiwa kikatiba kuwa Viongozi wa Tanganyika (Muungano), bali Watanganyika hawaruhusiwi kuwa viongozi wa Zanzibar (kero ya muungano), hili kila mtu analifahamu, na nadhani linashughulikiwa.

Sasa ninachokiomba kwa viongozi wa Nchi hii, wa kuteuliwa na wa kuchaguliwa, wa vyama vya siasa, viongozi wa dini na wapagani ni hiki, UZANZIBAR USITUMIKE KAMA KINGA DHIDI YA MAKOSA YA VIONGOZI WA KITAIFA WENYE KUTOKEA ZANZIBAR, kwamba sisi wakosoaji wa mambo mbali mbali ya msingi kwenye nchi yetu, tena ukosoaji wa kujenga, TUSIWEKEWE mipaka ya kumkosoa mtu kwa vile tu ni Mzanzibar, hata kama ametenda makosa au jambo baya linalopaswa kukosolewa, kitu hiki kinachotaka kupandikizwa kwenye nchi yetu kipingwe na kila mwenye dhamira njema ya kupinga maovu.

Ukosoaji wa madudu ya viongozi haukuanza leo, tulikosoa Nyerere na Viongozi wake, tulikosoa Mwinyi, Tukakosoa Mkapa, tulimpa za Uso Kikwete, tulikosoa Magufuli na Wapambe wake bila uoga wowote ule kwa vile tulikuwa na nia njema na nchi yetu, kwa hiyo tunapokosoa madudu ya leo tusionekane Wabaguzi, hatukosoi kwa Dini ya mtu wala kule atokako, TUNAHANGAIKA NA MAMBO ALIYOYAFANYA MTU AMBAYO TUNAONA KWAMBA NI MABAYA KWA MUSTAKABHALI WA NCHI.

William Lukuvi alisema maneno mengi mno ya kibaguzi kuhusu Zanzibar (Ushahidi umo humu JF), lakini hakuna kiongozi aliyepiga kelele, ndio kwanza akawa anateuliwa kwenye vyeo hivi na vile, nani amesahau? Mnataka tuamini kwamba Rais Samia alimtoa kwa vile aliibagua Zanzibar Wakati ule? La hasha, sisi wengine tunaendelea kuamini kwamba aliyemtoa alimtoa kwa kuzingatia utendaji wake.

Natoa wito kwa wale wanaotushambulia kwa kuwakosoa viongozi wanaotokea upande wa pili wa Muungano kwamba waangalie UKWELI WA HOJA ZETU badala ya kutaka kutufunga midomo.

Naomba kuwasilisha.
Vipi kuhusu utanganyika wetu, utumike kama kinga dhidi ya maovu mengi tunayoyafanya?.
 
Tujikite kwenye hoja ya DP World kwa kina, haswa mikataba itakayosainiwa na namna tunavyoweza kutetea maslahi ya kitaifa.

Kuanza kumpiga vijembe SSH ni kupoteza muda tu.
 
Chawa wa mbowe nasikitika na kukupa pole, mbowe maridhiano aliyobakiza mkia tu kummaliza ng'ombe ameyavuruga Kwa ulimi wake mshaurini akipiga zake konyagi asiwe anaingia kwenye platform za kisiasa kuongea make mwisho wake huishia kuharibu, siasa za kibabe za mwendazake zinaenda kurudi kwa Kasi na mtanyooshwa kweli kweli hili limama lilikuwa pisi sana Ila tayari mmeshaliuzi subirini majibu mtayapata.
 
Misukule ya mbowe mna taabu Sana Mie nafahamu kwanini umeleta thread hii, lkn Kwa sababu akili umemkabidhi mbowe ndo hujui kwanini akina waitara na kibajaji wanamshambulia mbowe ni sababu alishindwa kujenga hoja akaanza kumshambulia Samia na mbalawa Kwa uzanzibar wao nikuambie tu CCM hakuna anayemkingia kifua Samia na mbalawa sababu ya uzanzibar wao lahasha Ila tunalaani chokochoko za ukanda anazoeneza babu yako mbowe na lissu
Kumtumia Kibajaj na Waitara kumethibitisha uwezo wako kuwa duni
 
Back
Top Bottom