Uzalendo na ubunifu ndio msingi wa maendeleo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uzalendo na ubunifu ndio msingi wa maendeleo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zing, Jun 24, 2009.

 1. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Hi ni mwanachama mpya na naingia na changamoto ushauri kwa watu wote amabo jamii inawachukulia kama kioo. Hapa namaanisha watu kama wabunge, wasanii, vingozi wa masharika mmbali mbali ya binafsi na serikali lakini pia mimi na wewe

  kwa nn Tanzania tuna lima pamba lakini hatuexport nguo . watunga sera. wabunge , mimi na wewe tunafanya nini kuwasaidia wakulima na viwanda vya ndani?

  Mfano bungeni ni sheria imewekwa kuwa suti ndo vazi rasmi. Katika suti wanzaovaa wabunge, viongozi , mimi na wewe ni ngapi zimetengenezwa tanzania?je kuna hata Mmoja anayeshonesha suti yake angalau asaidie kukuza ajira za mafundi cherehani? Je wangapi tunawaunga mkono wabunifu wa tanzania .

  Kwa nini bunge lisiweke sheria nguo za vitenge kwa wanaume na wanawake ndo zikawa rasmi bungeni. Hii naona kukuzua utamaduni wetu, ajira na ubunifu nchini . Ikiwezekan basi waweke japo siku moja ya bunge iwe ni siku ya kuvaa vazi la kiafrika. Mfano kama huu wa ndo ubunifu ndo unahitajika si tu bungeni lakini sehemu mbali mbali

  Jibu nilolonalo mimi ni uzalendo ndio suluhisho la kwanza kwa maendeleo yetu. Na watanzani na waafrika wengi tumeishiwa na uzalendo. Tunanakili kila kitu kutoka magharibi. Inabidi tuachane na dhan ya kila kitokacho maharibi ni cha kiwango na kizuri kuliko chetu.

  Kwa nini imejegeka akilini kuwa suti ndio vazi official. watu watasema hiyo ni international standard. Kama ni intenrantiona standard je hatuwezi kuwa nanationa standard yetu? Lakini si tunaona viongozi wa nchi za kiarabu wanvaa kanzu .Kwa nini mtu akivaa nguo kama shati ya kitenge ofisini wanasema ni casual wear na si official wear

  Sina uhakika lakini nadhani China leo hii iko juu sababu ya uzalendo wa wanachi wao. wametengenza vitu vyao na wakanakili vya wengine ilipobidi. sababu ya uzalendo wa wachina kupenda vitu vyao viwanda vyao vilianza vidogo, vikawa vikubwa na vimeimarika na vimekuwa vikubaw mpaka vimeanza kuexport. Leo hii tunalazimishwa tuimbe wimbo wa nchi za magharibi kuwa bidhaa za ASIA ni feki. Tunahitaji sana bidhnaa za ASIA na sisi ikiwezekan tujifunze.

  Nawashauri watunga sera tusicheze ngoma wanayocheza UK, USA na kwingineko. uwezo wetu ni mdogo. Tutumie bidhaa hizi feki kujifunza na serikali ihamashihe wabunifu wa ndani hata kama kwa kwatuengeneza bidhaa za kunakili .

  Mtaniwia radhi kwa kukosa mtiririko maridhawa kwa hoja yangu ila namini wazo langu limesomek. UZALENDO + UBUNIFU  Nawasilisha
   
  Last edited: Jun 24, 2009
Loading...