Uyaudi na watu weusi

sony23

Member
Mar 27, 2018
11
20
Leo naendelea na huu uzi pale ambapo niliishia mara ya mwisho..

Baada ya kuona ushahidi wa wana historia mbalimbali juu ya uwepo wa wayahudi weusi ndani ya Afrika kaskazini na Afrika ya magharibi... leo nitatoa ushahidi wa wana historia na kuonyesha kuwa wayahudi weusi walijenga Empires za West Africa au the Western sudanic states...

Tunaanza na ushahidi wa professor Rudolf Windsor ambaye anatueleza kuwa wayahudi weusi wengi walihama kutoka Sudan na kuingia eneo la Niger river (west Africa) na wengine wakahama kutoka North Africa na kuingia eneno hilo hilo la Niger river. Anasema mwanahistoria Nahum schoulz kuwa wayahudi wengi ambao walipita Sudan na kuelekea eneno la Niger river walikuwa wametokea Ethiopia kwa sababu katika karne ya 2 na ya 3 AD Wayahudi weusi wengine walikuwa wakitoka Yemen (Arabia) na kuingia ndanya Ethiopia ila anasema kuwa hawa wayahudi weusi ambao walitokea huku Ethiopia wakipita Sudan walikutana na Wayahudi weusi wenzao ambao walikuwa wametokea North Africa kwenye maeneo kama Tunisia, Algeria, Morrocco na Egypt.

Wayahudi weusi hawa ambao walikuwa wametokea North Africa walikuwa wamekimbia Jihad baada ya kuvamiwa na waarabu, na hili eneo walilokutana hawa wayahudi weusi kutoka pande hizi mbili tofauti za Africa palikuwa ni katikati ya Senegal na Niger river ambapo hapo walitengeneza confluence centre ambayo ili develop na kuja kuwa a large commercial na educational centre iliyoitwa timbuktu,.. kuna mwanahistoria na mwandishi mwingine kwa jina la John J williams yeye alisema kuwa Wayahudi weusi walihama kutoka North Africa kwa kuvuka nile na kupita miji kama Memphis, Elephantine na khartoum na baadae anaamini kuwa kuna baadhi ya wayahudi weusi ambao wali settle kwenye eneo la white Nile na aki amini kuwa kuna mji unaitwa Shilluk ambayo upo mpakani mwa Uganda na Sudan ila anaamini wayahudi hao wengi walipita eneo la Kordofan, kuelekea Darfur na baadae wakapita Lake chad na kuingia Niger river ila wanahistoria hawa wote wanakubaliana kuwa wayahudi weusi waliingia west Africa mnamo mwaka 300 AD.

Tunaanza na Wayahudi weusi wa Ghana empire.

Ghana empire ilianzishwa na Myahudi mweusi aliyeitwa Za el Yemeni ambaye mwanahistoria John j Williams anasema kuwa alitokea Yemen na akapita Ethiopia kisha akaingia mji wa wayahudi weusi wargla, Algeria na baadae mnamo mwaka 300 AD akaingia west Africa, wanahistoria wawili DR Berth na Professor Godbey wanasema kuwa Za el Yemeni ndo aliyekuwa Myahudi mweusi wa kwanza kuanzisha Dynasty wa kiyahudi ndani ya west Africa dynasty ambayo iliitwa the za dynasty. Waarabu na moors wanaotokea Afrika ya kaskazini wanakubali kuwa wayahudi weusi ndo watu wa kwanza kujenga empire za west Africa anasema Professor Rudolf Windsor anatoa kuwa hawa wayahudi weusi walikuwa na advantage kuliko native Africans kwa sababu walikuwa wametembea sehemu nyingi duniani kama Uarabuni na Ulaya na kingine ni kuwa walivyokuwa Jerusalem walikuwa na knowledge na wealth vya kutosha.

Anasema kuwa kwenye Ghana empire wafalme wa kiyahudi walikuwa na majina mawili la kwanza ni Kayamanga (master of gold) na la pili ni Ghana (war chief).. anasema Professor Rudolf Windsor anatoa kuwa Ghana empire ilitawaliwa na wafalme wa kiyahudi 22.. na pia ndani ya Ghana empire kulikuwa na wasomi wengi sana kama astronomers, mathematians, doctors, engineers, teachers, architects and etc.
Mwandishi mwingie kwa jina la El zouhri anasema kuwa Ghana empire ilikuwa ikimiliki chuma ya kutosha na ndio maana waliweza kushinda vuta dhidi ya surrounding states anasema Professor Rudolf Windsor kuwa Za el Yemeni alijenga his capital for the Ghana empire ndani ya Gao..

Baada ya hapo Native Africans walichukua power na kujenga Mali empire ambayo ilifika climax chini ya Mansa kankan Musa, emipre ya Mali ilijengwa na waafrika wa kabila la Mandingo ambao walikuwa chini ya himaya ya wayahudi weusi ya Ghana, baada ya Ghana empire kuanguka hawa waafrika wa Mali empire wakajenga empire na kuuita Mali empire chini ya mtu aliyeitwa Sundiata, Mali empire iliendeshwa kwa kiislamu (yaani wafalme wa Mali empire walikuwa waislamu na wananchi wote wa Mali empire) kwa sababu kwa asilimia kubwa wafalme wa Mali empire kama Mansa kan kan Musa walikuwa wakifanya biashara na Waarabu wa North Africa... kipindi hichi cha Mali empire wayahudi weusi walilazimishwa kuwa waislamu kitu ambacho kilifanya wayahudi weusi wengi kwa wakati huo kukimbilia Afrika ya kati, Afrika mashariki na Afrika ya kusini katika wimbi ambalo wanahistoria waliliita BANTU MIGRATION.

Kipindi hiko himaya ya wayahudi weusi ya Ghana ilikuwa imevunjika vipande vipande ilikuwa mnamo mwaka 1240 AD anatueleza professor Rudolf Windsor, anatuambia kingdom pekee ambayo ilikuwa bado ina nguvu ambayo ilikuwa chini ya wayahudi weusi ni GAO tena na yenyewe ilikuwa chini ya utawala wa Mali empire.... ila wayahudi weusi walirudisha nguvu yao ndani ya Afrika magharibi mnamo mwaka 1350 AD ambapo prince wa 16 wa dynasty ya wayahudi weusi iliyoitwa Za dynasty ambayo jina lake ni Sonni Ali aliteka makabila ya karibu wakati akitawala GAO na akajenga empire ambayo iliitwa SONGHAY EMPIRE. Kipindi hiki wayahudi weusi wengi waliokuwa wanaishi Afrika magharibi walikuwa wamesha adopt uislamu ikiwemo pia Sonni Ali mwenyewe... ila tunajulishwa na professor Rudolf Windsor kuwa wafalme wengi wa Songhay empire ikiwemo wananchi walikuwa waislamu jina tu ila waliendelea na practice za kiyahudi ki siri siri,.... kipindi hiki cha Songhay empire wayahudi weusi walikuwa wakitawala tena huko Afrika ya magharibi na wafalme wa Songhay empire walikuwa wame mix imani yaani walikuwa ni waislamu na pia ni wayahudi... anasema Professor Rudolf Windsor anatuambia kuwa kipindi Ghana empire ina fall wayahudi weusi wengi sana walikimbilia to the coast of Afrika na pia wengine to the remote areas ndani zaidi ya Afrika sana sana wayahudi weusi wengi walikimbilia central Africa na East Africa katika makimbizi yale wanayoyaita BANTU MIGRATION... Mwanahistoria Nahum slouchz anasema kuwa wayahudi wengi walivyohama na kukimbilia maeneo ya ndani zaidi ya Afrika ya magharibi, na Afrika ya kati na pia Afrika ya mashariki huko walikutana na pagan beliefs za local African tribes,... anatujuza Nahum slouchz kuwa maeneo waliyokaa hawa wayahudi weusi hasa west Africa na central Africa baada ya kuanguka kwa Ghana empire kulikuwa na mchanganyiko wa imani tatu, Judaism, paganism na Mohammedanism(islam)... kitu ambacho kilileta cultural diffusion kwa hawa wayahudi weusi kwa sababu kilienda kupoteza identity yao.....


Wayahudi weusi wengi kama nilivyosema hapo awali walikuwa wakiiona asili yao kama mzigo na wengi wakaendelea kufanya asili yao kama wayahudi ya kuwa ni siri kwa sababu waliogopa kufa chini ya mikono ya uislamu(Jihad) huko Afrika ya magharibi, anasema Professor Rudolf Windsor anatoa sababu kwa kuwa walikuwa na rangi sawa kama ya Waafrika wengine basi waliweza kujichanganya kirahisi... Nahum slouchz anataja kabila moja ambalo lipo Congo linaloitwa Bavumbu au Mavumbu anasema kuwa hawa jamaa ni moja kati ya makabila mengi yenye asili ya kiyahudi na walihama west Africa na kuingia Congo baada ya the fall of Ghana empire.. ila wengi wao hili kabila wana practice paganism (African local beliefs) ni baada ya kukutana na local Africans.. japo pia professor Rudolf Windsor anatujuza kuwa hawa jamaa wanasema kuwa wengine wao walitokea Ethiopia na wengine wao walitoka kwa wayahudi weusi waliokuwa Angola..

Professor Rudolf Windsor anatujuza pia kuhusu wayahudi weusi maarufu waliokuwepo hispania na pia ni majina makubwa kwenye falsafa akiwemo Moses maimonides ambaye anasema kuwa jina lake kamili lilikuwa ni Rabenu Moshe ben maimon.. alizaliwa cordova hispania mnamo mwaka 1135 march 30, baba yake alikuwa ni mzawa wa familia ya wasomi na watu wa dini.. na kizazi chao kilitokea kwa mtu anayeitwa prince Judah ambaye alikuwa mmoja wa watu wa kwenye baraza la mfalme Daudi, alijifunza mambo mengi tofauti na Torati.. na elimu hizo alizojifunza Moses maimonides zilikuwa ni natural sciences, mathematics, philosophy, metaphysics na pia logic na alisoma chini ya walimu wa kiyahudi na Moors, na mwengine ni Baruch spinoza naye alikuwa msomi mwanafalsafa ambaye alikuwa ni myahudi mweusi na alikuwa ni msomi wa torati na masomo ya falsafa kama alivyosoma Moses maimonides na wengine wayahudi weusi wengi sana maarufu..

Nitaishia hapa kwenye huu uzi nitaendelea siku nyingine... itaendelea.
 
Nadhani hili la black Israerites sio siri kiviiile, linaeleweka vizuri. Thanks for the nice share brother; labda swali, walikujaje huku while kwao ni pale mashariki ya kati? Tukumbuke hawa jamaa waliwahi kuishi Misri kwa zaidi ya miaka 400 na mara nyingi pale kwao ilikua ikitokea shida yoyote either njaa au vurugu tu kati yao na wavamizi, makimbilio yao ilikua ni Misri, haya yalitokea kabla mfereji wa Suez canal haujachimbwa so ilikua ni rahisi tu kwenda na kurudi mashariki ya kati to Egypt, wale wa Ethiopia ambayo miaka hiyo nchi hi ilijulikana kama Kushi wengi wao walikuja enzi za mfalme Suleiman, Suleiman aliwahi kutembelewa na mfalme wa Ethiopia (Kushi ya enzi hizo ) mfalme huyu alikua mwanamke, yasemekana Suleiman alifanya yake na huyu mama aliondoka na mimba ya kaka Sele, while going back to her home place (Ethiopia ) mfalme Suleiman alitoa escort ya Wayahudi kadhaa (remeber kipindi hiki neno au jina JAHUDI ) lilikua halijaanza kutumika, walikua tu wanaitwa Waisrael, wengi wa walio escort msafara hu walipendezwa na mazingira ya Ethiopia/Africa and hence hawakurudi tena kwao but again kukatokea connection za kibiashara between those two countries and hence mashariki ya kati na Ethiopia (hope na majirani zao as well ) ikashamiri, hawa watu katika kutembea kwao is obvious walikua wanapata HUDUMA ya kimapenzi na wenyeji wao, huduma hi wakati mwingine ilitengeneza UZAZI and hence uzao wao ukajikuta unaongezeka mitaa hi ya Africa; so sio jambo la ajabu kua na hawa black Israerities in Africa or anywhere in the other parts of the world.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom