Wanasheria wachambua kesi ya Mama aliyefungwa miaka 22 kwa kukutwa na nyama ya swala

gstar

JF-Expert Member
Jun 19, 2011
759
1,250
Anaitwa Maria Ngoda, mkazi wa mtaa wa Zizi la Ng'ombe, Iringa. Siku ya tukio alikutwa karibu na makazi yake na ndoo iliyosadikika kuwa na vipande 12 vya nyama. Baada ya utambuzi, vikabainika ni nyama ya Swala.

Nyama hiyo, imetajwa kuwa na thamani ya TZS 900,000. Maria akajitetea akasema hakujua kama nyama hiyo ni ya Swala, pia sio yake alikabidhiwa na kijana anaitwa FUTE ili auze. Maria anasema, ndoo ilikuwa na vipande 13, Fute akaondoka na kimoja.

Baada ya hilo, uongozi wa Mtaa ukaongozana na Maria mpaka nyumbani kwa ndugu Fute. Lakini, kabla ya lolote kujadiliwa, uongozi huo UKAMLAZIMISHA Maria ajitwike ndoo hiyo kichwani na safari ikaanza kuelekea kituo cha polisi. Maria akawekwa chini ya ulinzi. Fute hakuguswa, akabaki kuwa mtu huru.

Jalada la mashtaka likafunguliwa, kesi ikafika kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa. Tangu kesi inaanza mpaka kumalizika kwake, Maria hakuwa na mwakilishi (WAKILI). Maria AKAKIRI kukutwa na nyama hiyo, lakini akagoma kuwa yeye sio MMILIKI. Baada ya utetezi huo, na kesi kufungwa, upande wa DPP ukaoimba mahakama kutoa ADHABU KALI ili iwe fundisho kwa wengine. Ndipo Hakimu Mkazi Mkuu wa Iringa, siku ya tarehe 3 Novemba 2023, akamuhukumu Maria kifungo cha miaka 22 gerezani.

JE, SHERIA INASEMAJE!

Maria amehukumiwa chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 (The Wildlife Conservation Act, 2009, R.E 2022) kifungu cha 86(1),(2),(c), sambamba na Sheria ya Uhujumu Uchumi, SURA 200, kifungu vya 57(1) ukisoma sambamba na Aya 14 ya Jedwali la kwanza (First Schedule) na kifungu 60(1) na (2) vinavyotaja adhabu ya miaka isiyopungua 20 lakini isiyozidi 30 mtuhumiwa anapokutwa na hatia.

Sheria hii inakataza kuua, kuuza au kukutwa na nyama ya mnyamapori pasipo KIBALI, na wanyama hao wameorodheshwa kwenye sheria ya Wanyamapori kwenye Jedwali la Kwanza, Sehemu ya Kwanza.

MJADALA NA UDHAIFU WA KESI:

Wengi, ikiwemo na mimi tunaamini huyu mama hakutendewa haki kwa sababu hakuwa na mwakilishi (Wakili). Upande wa DPP ulitumia UDHAIFU huo ili kutimiza lengo la kumfunga mtuhumiwa. Pia, mahakama japo ya kupewa taarifa kupitia utetezi wa Maria kuna mtu mwingine anaitwa FUTE ndiye MMILIKI wa hiyo nyama, mahakama haikutuma SUMMONS ili Fute aje kutoa ushahidi.

Pia, sheria imetaja aina ya USHAHIDI unaotakiwa uwasilishwe na baadi ya NYARAKA za utambulisho ili mtuhumiwa akutwe na hatia, kitu ambacho Maria asingekuwa na uwezo wa kuzitambua au kuziCHALLENGE. Tukio hili kisheria ni "NEGLIGENCE" au/na "MISCARRIAGE OF JUSTICE".

Katika hatua hii, Maria ana haki ya kukata RUFAA chini ya Katiba ya nchi, ibara 13(6)(a), na ndicho kinaenda kutokea. Binafsi nataka haki itendekee, hata kama ni kufungwa, basi mtuhumiwa afungwe baada ya KUSIKILIZWA KWA UKAMILIFU kama Katiba inavyosema, haki ambayo hakupewa.

Mwisho, kuna haja ya kupitia sheria hizi maana hazitoi haki, na hazina MASLAHI kwa Taifa. Pia, kuna UDHAIFU katika UTEKELEZAJI wa sheria hizi, na wengi wako magerezani kwa sababu ya udhaifu huu. Tangu sheria hii imeanza kutumika, wananchi wengi wameumizwa na wanaendelea kuumizwa na hakuna tija kwa Taifa.

maxresdefault.jpg
 
Pana ndege ilitua KIA ya Urusi iliondoka na Wanyama wakiwa hai kabisa baadae tuliambiwa kuwa ile ndege ya jeshi ilileta watalii yaani watalii wapande ndege ya mizigo harafu Mtanzania anakamatwa na vipande vya swala anafungwa miaka 22 huko Australia walikamata Simba aliesindikwa airport inasemekana alitoka Tanzania(KIA) na taarifa zipo mtandaoni huyo DPP hayo hayaoni yupo na wamama wa Iringa hiyo sheria ningeiona ipo kama kwa hayo Majambazi sugu pia yangeguswa huyo Mama mtoeni tusiendelee kulaaniwa kwa kuonea wanyonge...
 
Nilipoendelea kusoma. Nikaacha na kurudi kwenye kichwa cha habari, KWAMBA WANASHERIA NDIO WAMECHAMBUA KESI.
Nakuja kushtuka ni mtu ambaye kama sio sheria mwaka wa kwanza basi atakua failure au ana disco ya law na bado anaipenda sheria. Vifungu anaweza fungua ila si kutetea.
HATA WEWE MWANDISHI WA HII THREAD TAYARI UNAWEZA FANYA MARIA ARUDI RUMANDE NA KUSHINDWA KUSHINDA RUFAA YAKE. UMEANDIKA UJINGA SANA.

Tunamtetea maria ila sio kwa grounds zako ulizoweka.

Maria Kwanza Amekutwa na vipande hivyo na kukubali, swala la fute kuwepo au kutokuwepo si ground ya kuwa na uzito kushinda rufaa. Futebis out on this, we need maria not fute.

Mbili, usije ropoka tena kwamba hakimu kataka kutimiza lengo lake kumfunga ni upuuzi, tutachosema , hakimu arejee kesi ya awali na atusaidie kadri ya matakwa yetu, kumpa haki yake maria.

Tatu, Maria kuwa bila wakili sio ground ya rufaa, mawakili wataojitokeza wataenda kusaidia ila kesi kuamuliwa bila wakili ni sawa kabisa.

Kuna kitu kinaitwa pro se representation,
(For one self au for self representation)

Kesi inaweza kwenda bila wakili.

Sasa tengeneza grounds ukitaka kumtoa maria, au kushinda rufaa au apunguziwe muda.

Yaani maria mwenyewe kaweza kujitetea yeye ni mlezi hivo apunguziwe na mahakama imekubali ombi lake,
Wewe unasema ni mwanasheria hata grounds heavy za kushinda rufaa huna.
Gadamn.
 
Sa

Sawa bushlawyer
 
Sasa kumbe hata aliyempa nyama hakuitwa kutoa ushahidi?! Yaaani tuna mahakimu wenye magonjwa ya akili! Ni Sadists!!
Inaonekana huyo Mwenyekiti aliamua kumpa matatizo Mama Maria ila watu weusi tuna roho mbaya sana aisee...huko Iringa na Mbarali watu wanawinda mbuga ya Ruaha kama yao vile na hawafanywi kitu wanakuja kuwaonea wanyonge tuu inauma sana kusikia hizi mambo aisee..
 
Roho mbaya haitokani na rangi ya ngozi,acha ujinga
 
Anaitwa Maria Ngoda, mkazi wa mtaa wa Zizi la Ng'ombe, Iringa. Siku ya tukio alikutwa karibu na makazi yake na ndoo iliyosadikika kuwa na vipande 12 vya nyama. Baada ya utambuzi, vikabainika ni nyama ya Swala.

Nyama hiyo, imetajwa kuwa na thamani ya TZS 900,000. Maria akajitetea akasema hakujua kama nyama hiyo ni ya Swala, pia sio yake alikabidhiwa na kijana anaitwa FUTE ili auze. Maria anasema, ndoo ilikuwa na vipande 13, Fute akaondoka na kimoja.

Baada ya hilo, uongozi wa Mtaa ukaongozana na Maria mpaka nyumbani kwa ndugu Fute. Lakini, kabla ya lolote kujadiliwa, uongozi huo UKAMLAZIMISHA Maria ajitwike ndoo hiyo kichwani na safari ikaanza kuelekea kituo cha polisi. Maria akawekwa chini ya ulinzi. Fute hakuguswa, akabaki kuwa mtu huru.

Jalada la mashtaka likafunguliwa, kesi ikafika kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa. Tangu kesi inaanza mpaka kumalizika kwake, Maria hakuwa na mwakilishi (WAKILI). Maria AKAKIRI kukutwa na nyama hiyo, lakini akagoma kuwa yeye sio MMILIKI. Baada ya utetezi huo, na kesi kufungwa, upande wa DPP ukaoimba mahakama kutoa ADHABU KALI ili iwe fundisho kwa wengine. Ndipo Hakimu Mkazi Mkuu wa Iringa, siku ya tarehe 3 Novemba 2023, akamuhukumu Maria kifungo cha miaka 22 gerezani.

JE, SHERIA INASEMAJE!

Maria amehukumiwa chini ya Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Na. 5 (The Wildlife Conservation Act, 2009, R.E 2022) kifungu cha 86(1),(2),(c), sambamba na Sheria ya Uhujumu Uchumi, SURA 200, kifungu vya 57(1) ukisoma sambamba na Aya 14 ya Jedwali la kwanza (First Schedule) na kifungu 60(1) na (2) vinavyotaja adhabu ya miaka isiyopungua 20 lakini isiyozidi 30 mtuhumiwa anapokutwa na hatia.

Sheria hii inakataza kuua, kuuza au kukutwa na nyama ya mnyamapori pasipo KIBALI, na wanyama hao wameorodheshwa kwenye sheria ya Wanyamapori kwenye Jedwali la Kwanza, Sehemu ya Kwanza.

MJADALA NA UDHAIFU WA KESI:

Wengi, ikiwemo na mimi tunaamini huyu mama hakutendewa haki kwa sababu hakuwa na mwakilishi (Wakili). Upande wa DPP ulitumia UDHAIFU huo ili kutimiza lengo la kumfunga mtuhumiwa. Pia, mahakama japo ya kupewa taarifa kupitia utetezi wa Maria kuna mtu mwingine anaitwa FUTE ndiye MMILIKI wa hiyo nyama, mahakama haikutuma SUMMONS ili Fute aje kutoa ushahidi.

Pia, sheria imetaja aina ya USHAHIDI unaotakiwa uwasilishwe na baadi ya NYARAKA za utambulisho ili mtuhumiwa akutwe na hatia, kitu ambacho Maria asingekuwa na uwezo wa kuzitambua au kuziCHALLENGE. Tukio hili kisheria ni "NEGLIGENCE" au/na "MISCARRIAGE OF JUSTICE".

Katika hatua hii, Maria ana haki ya kukata RUFAA chini ya Katiba ya nchi, ibara 13(6)(a), na ndicho kinaenda kutokea. Binafsi nataka haki itendekee, hata kama ni kufungwa, basi mtuhumiwa afungwe baada ya KUSIKILIZWA KWA UKAMILIFU kama Katiba inavyosema, haki ambayo hakupewa.

Mwisho, kuna haja ya kupitia sheria hizi maana hazitoi haki, na hazina MASLAHI kwa Taifa. Pia, kuna UDHAIFU katika UTEKELEZAJI wa sheria hizi, na wengi wako magerezani kwa sababu ya udhaifu huu. Tangu sheria hii imeanza kutumika, wananchi wengi wameumizwa na wanaendelea kuumizwa na hakuna tija kwa Taifa.

View attachment 2809337
Mbona kina rostam azizi wanapakiza hadi twiga kwenye ndege na kuwatorosha tena wanamiliki nyara za serikali makontena kwa makontena na bunduki haramu za ujangili ila awafungi jela hata saa 1
 
Back
Top Bottom