Uwoya aambulia matusi baada ya kumfananisha diamond na michael jackson

Uwoya aambulia matusi baada ya kumfananisha diamond na michael jackson

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,091
Reaction score
34,899
UWOYA AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUMFANANISHA DIAMOND NA MICHAEL JACKSON



​

Mwigizaji wa filamu za Kibongo, Irene Pancras Uwoya, amelowa mvua ya matusi baada ya kumfananisha mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na aliyekuwa mwanamuziki mkubwa duniani, marehemu Michael Jackson.

Wikiendi iliyopita, Uwoya aliandika kwenye ukurasa wake katika mtandao wa Instagram kuwa msanii huyo anayefanya vizuri katika Bongo Fleva ndiye staa atakayemrithi mkali huyo wa Pop, maandishi ambayo yalizua matusi hayo ya nguoni.

Baadhi ya mashabiki wa mastaa hao walitoa maoni kuwa jambo hilo ni sawa na kufananisha vitu ambavyo havina uwiano hasa ukizingatia Michael Jackson alishafariki dunia Juni 25, 2009.

“Sasa hiyo ni akili gani ya ki…(tusi) kumfananisha mtu aliyeko hai na marehemu?” alihoji Mishish, mmoja wa mashabiki wa Uwoya katika mtandao wa Facebook baada ya ishu hiyo kuwa gumzo mitandaoni.

“Kweli wewe Irene (Uwoya) ni …(tusi) au kwa sababu Diamond amesha…(tusi) ndiyo maana unamsifia kiasi hicho,” aliandika shabiki mwingine kwenye Twitter na kupisha wengine kuendelea kumporomoshea Uwoya matusi ya nguoni.

GPL

UWOYA AAMBULIA MATUSI BAADA YA KUMFANANISHA DIAMOND NA MICHAEL JACKSON - MPEKUZI HURU

 
Ndo nini sasa hii??

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Uwoya haya GPL Wapige rmx na matusi ya JF.
-Uwoya ni mbulura na pia ana tamaa sana mpenda pesa anajipendekeza kwa diamond ili apate umatemate.
 
Back
Top Bottom