Uwongo wa Pamoja Haudumu

Uwongo wa Pamoja Haudumu

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267
balaaa Madenti wa5 wa chuo kikuu kimoja hapa nchini
walikuwa wanatakiwa wafanye mtihani siku
inayofuata. Bahati mbaya wakanywa pombe mpaka
mida mibaya na hivyo wasingeweza kufanya mtihani
huo kesho yake. Wakatunga uongo wa kwenda
kumdanganya mwalimu wa somo husika, kwamba walikuwa kwenye harusi na wakati wanarudi gari
yao ilipata pancha na wakavamiwa na vibaka na
kuibiwa na kupigwa. Yule lecturer alikubali na
akawapa siku 3 za kujiweka sawa na kujiandaa na
special exam. Siku ya mtihani wa special yule lecturer
aliwapa mtihani na aliwasimamia mwenyewe. Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama ifuatavyo:
o Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano
o Ili wafaulu majibu yao ni lazima yawe sawa, na
yakiwa tofauti wote wanapata ziro na wanafeli
o Mtihani huu una maswali matano na lazima yote
yajibiwe. Maswali ya mtihani yalikuwa hivi:
1. Harusi ilifanyika katika ukumbi gani?
2. Gari mliotumia mpaka mkapata ajali/pancha
inaitwaje?
3. Ajali imetokea eneo gani?
4. Nani alikuwa dereva? 5. Tairi ipi ilipata pancha, ya mbele au ya nyuma? NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!!
 
ningekuwa mimi ndio lecturer ningekula kabaaang na kuyashika ma------ kwa molari yote!
 
Hahahahaha! AMAVUBI umenichekesha na kunifanya nijiulize hivi: sasa wakipasi uwo mtihani itakuaje?
-watapewa credit zao?
-watapewa mtihani mwengine au itakuwaje?
Embu nisaidie basi..!
 
Back
Top Bottom