Uwongo unanitesa je nifanyeje niipuke aibu hii?

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,947
10,815
Nimekuwa mwongo sana tangu nikiwa mvulana. Sasa nimekuwa baba mtu mzima ila bado nadanganya hata vitu visivyo na maana najikuta nimedanganya.
Nifanyeje ili niishinde kadhia hii... maaana nina aibika na kuumbuka na kudanganya huku najikuta tu tayari nimesha danganya
 
Halafu Watu waongo wanakuwa MAKAUZU sana.

Anakudanganya halafu wala hana wasi hata kidogo.

Nafikiri Uongo ni Kipaji au Kilema fulani
 
Cha kwanza badirisha Id yako, weka jina lako halisi. Kisha kama muislam anza kuswali swala 5 huku ukitubia makosa ya uongo. Endelea na ibada, hakikisha ibada inakua sehemu ya maisha yako. utayashinda yote inshaallah
 
Nimekuwa mwongo sana tangu nikiwa mvulana. Sasa nimekuwa baba mtu mzima ila bado nadanganya hata vitu visivyo na maana najikuta nimedanganya.
Nifanyeje ili niishinde kadhia hii... maaana nina aibika na kuumbuka na kudanganya huku najikuta tu tayari nimesha danganya
Mwamini Bwana Yesu Kristo, Yeye pekee atakuwezesha kushinda dhambi zote ikiwemo hiyo ya uongo.
 
Nimekuwa mwongo sana tangu nikiwa mvulana. Sasa nimekuwa baba mtu mzima ila bado nadanganya hata vitu visivyo na maana najikuta nimedanganya.
Nifanyeje ili niishinde kadhia hii... maaana nina aibika na kuumbuka na kudanganya huku najikuta tu tayari nimesha danganya
Tabia haina dawa
 
Cha kwanza badirisha Id yako, weka jina lako halisi. Kisha kama muislam anza kuswali swala 5 huku ukitubia makosa ya uongo. Endelea na ibada, hakikisha ibada inakua sehemu ya maisha yako. utayashinda yote inshaallah
Asianze kuswali kabla hajaacha uongo ataleta machafuko bure maana atajikuta amesema kuna bomu wakati uongo.
 
Nimekuwa mwongo sana tangu nikiwa mvulana. Sasa nimekuwa baba mtu mzima ila bado nadanganya hata vitu visivyo na maana najikuta nimedanganya.
Nifanyeje ili niishinde kadhia hii... maaana nina aibika na kuumbuka na kudanganya huku najikuta tu tayari nimesha danganya
We ni mwanasiasa?
 
Omba Mungu hiyo roho ikutoke,si unajua kuwa uongo ni dhambi...?
 
Pole sana...

Kuwa muwazi, unadanganya kwenye nini haswa? Au watu wa aina gani unapendelea kuwadanganya zaidi?

Muongo siku zote ni yule mtu anayependa sifa...

Ila mtoa mada umeongea kwa Code...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom