Uwezo Duni TBS Unaligharimu Taifa

Uwezo Duni TBS Unaligharimu Taifa

Miaka ya 90 kurudi nyuma bidhaa ghushi hazikuwa nyingi kiasi hiki...inaogopesha kuona hata tairi na vipuri vya magari vingi vipo chini ya ubora na Mamlaka husika ipo kimya tu...unajiuliza vinaingilia Bandari ya waapi!?

TBS ijitathmini haiwezekani tukawa na bidhaa duni nyingi kiasi hiki tunahatarisha USALAMA wa wananchi wetu.
 
TBS hawana maana, nilinunua tyubu ya pikipiki isiyo Bora kuijaza tuu upepo ikapasuka.Napendekeza Raisi aifumue TBS.
 
Kwenye vifaa vya umeme na machinery, huko nako ni balaa. Kila duka zimejaa bidhaa za China, na kwa kukadiria, zaidi ya 70%, zina ubora hafifu kabisa.
Upo sahihi hii TBS ingefutwa tu haina chochote wanachofanya
 
Serikali iwekeze kwenye viwanda vyetu.

Serikal itoe scolarship kwa wanafunz wakajifunze technolojia nje ya nchi then waajiliwe hapa kwetu..

Bila kuwekeza kwenye elim hili tatizo litaendelea forever...
 
kuna kitu nitapenda kueleza.

kama tanzania itapenda kufika mbali kimaendeleo.

basi hiki chama naomba kiache kudili na vyama pinzani na mambo ambayo kuona inaogopa kutoka madarakani.

nimegusia tu.

ila wenzetu walicho tuzidi ni kwamba sisi TBS tumewapa kila kitu kushugulikia vitu vyote ndio maana ni tatizo.

TBS ilitakiwa kuwa mama wa idara kama TANROAD kwa tarura.


TBS ilitakiwa kuwa na idara ambazo zinanguvu na zina mikakati yake na taratibu zake bila kuingiliwa na kuwa na chata maalumu ya kutoa vibali.

mfano south africa wana TBS yao ila kuna idara ambayo ni maalumu na inanguvu kwa ajili ya kusimamia vifaa vya mawasiliano kwa ubora na kiafya
IMG_1028.jpg


inaitwa ICASA.

lakini cha kushangaza hapa kwetu kila kitu TBS kutaka kubeba vyote.

kwa nini zisiwe idara uhuru kuanzia kama madawa na chakula tulivoweka uhuru TFDS ila japo na yenyewe kama imalala.

hizi ni moja za idara za vifaa ambazo hata kampuni utambua na azipeleki vifaa vyao nchi fulani au kutumika bila kupata kibali
IMG_1027.jpg
 
Leo hii Tanzania imejaa bidhaa nyingi zenye ubora duni zilizotengenezwa China na ndani ya Tanzania, na kwa kiasi kidogo toka India na Thailand.

Leo hii, ni rahisi sana kuikunja nondo ya 16mm iliyotengenezwa Tanzania kuliko nondo ya 12mm iliyotengenezwa Kenya. Mathalani, ukienda dukani kutaka kununua nondo ya 6mm, utaulizwa unataka 6mm nene (imetengenezwa Kenya) au nyembamba (imetengenezwa Tanzania). Unajiuliza, hivi
Mamlaka zishughulikie hili jambo kwa haraka.Tzn sio dampo la bidhaa feki zinaua uzalishaji wa ndani.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Yote tisa,

Kumi hujauziwa kadet nzuri ya kung'aa alafu ukiweka kwenye maji tu inageuka rangi, kama ilikuwa ya kijivu inakuwa nyeupe au njano
Huko kwenye nguo ni balaa,na wafanyabiashara wanaenda china wananunua bidhaa feki kwa bei za chini wanakuja kutupiga.

Hii hoja ni ya muhimu sana Serikali tafadhari Sana shughulikieni hili,ni aibu duka linauza bidhaa unaambiwa unataka feki au original.
 
Umasikini wa watanzania ndio unafanya kuwepo na bidhaa duni sokoni, TBS hawawezi kukaza kwa 100% wanasiasa watawajia juu.

Fikiria TV zote madukani zingekuwa na bei za Samsung, LG n.k au simu zote zingekuwa na ubora na bei za iphones, watanzania wangapi wangeweza kumudu?

Kitu pekee ambacho TBS wanakizingatia kwa asilimia kubwa ni usalama / afya za watumiaji. Kwenye bidhaa suala la kudumu muda mrefu au la ni wewe na urefu wa mfuko wako.

Mwenye pesa kidogo nenda kariakoo kanunue tecno, kama zipo za kutosha nenda mlimani city kanunue iphone. The same kwa bidhaa nyingine zote.

Hata kwenye madawa ya binadamu (TMDA) fumula ni hiyohiyo, kuna paracetamol kutoka UK inauzwa 10,000 na kuna paracetamol ya zenufa inauzwa 100, ni wewe na wallet yako.

Nchi masikini hii ndugu, ebo!
Sasa kaka unatenganishaje usalama wa mtumiaji na ubora wa bidhaa... Unaposema TBS wao wanaaangalia tu usalama wa mtumiaji wa bidhaa ila ubora au kudumu kwa bidhaa miaka mingi sio issue hapo unakuwa umechanganya mambo

Ubora wa bidhaa ni jambo mtambuka lina cover kila sehem.. Mleta mada amekwambia kiatu ndan ya miez 3 kimeachia soli inamaana hakina ubora shukuru mungu hakupata madhara

Imagine akaenda site kakanyaga msumari umetoboa soli na kumchoma au kaangungiwa na kitu kizito mbele ya kiatu vidole vikakatika..

Ametolea mfano wa kuachia soli kuonyesha ubora hafifu na kama ubora hafifu maana yake mtumiaji hayuko salama.. Sasa hao TBS usalama upi wanaosimamia

Na kwenye dawa... Utofauti wa bei unatakiwa utegemee umbali wa bidhaa ilipotoka sio ubora wa bidhaa kama dawa ya UK itauzwa 10k basi iwe nisababu za logistic ndo.zimepandisha bei ila isiwe kuwa inaubora kuliko dawa ya TZ inayouzwa 500. Ikiwa hivyo sio sahihi hata kidogo
 
Nina uhakika TBS ina vifaa bora sana na hata wafanyakazi wake ni well trained and qualified, tatizo la nchi yetu ni commitments kwa kazi, wafanyakazi wengi wa serikalini kwenye issues za ubunifu na uwajibikaji is almost 0 kabisa. Mifano ni kama hiyo ulioitoa ambayo nakubaliana na wewe 100%
 
Umenena vema, tiles za goodwill ni takataka kabisa,tiles zimepishana size madhalani tiles ya 40cmx40cm zimepishana zingine 40.2cm mpaka 40.3cm zingine ni 39.8cm.

Kwakweli sujui TBS wanafanya nini?
Uwepo wa TBS na kutokuwepo, kwa kuangalia ubora wa bidhaa zilizopo.nchini, kama kuna utofauti, basi ni mdogo sana.

Kama TBS wanashindwa kudhibiti vipimo tu vya tiles, ni nini tena wataweza?
 
Pole sana.

Acha fikra hasi, kwa kuamini kuwa kila nchi ipo kwaajili ya kuihujumu Tanzania.

Kama Dunia nzima ingekuwa na watu wenye fikra duni kama wewe, UNO, AU, EEC, ECOWAS, NATO, WTO, n.k. visingekuwepo. Wenye akili wanatambua kuwa kuna wakati ili kupunguza gharama na kuongeza ufanisi, kunahitajika kuundwa kwa taasisi za kimataifa.

Unasemaje juu ya uwepo wa taasisi za kudhibiti ubora wa bidhaa? Nazo zinaihujumu Tanzania?
 
Mkuu ukiangalia manufacturering dates ya hizo tairi? Isije kuwa zilisha expire?
Hapana, zilikuwa zina mwaka toka zitengenezwe, hii Ni kwa mujibu wa taarifa zilizoandikwa kwenye tairi zenyewe.
 
Uwepo wa TBS na kutokuwepo, kwa kuangalia ubora wa bidhaa zilizopo.nchini, kama kuna utofauti, basi ni mdogo sana.

Kama TBS wanashindwa kudhibiti vipimo tu vya tiles, ni nini tena wataweza?
Tena za hapa nchini sijui hizo sample wanazochukuaga wanafanyia nini yaan
 
Ni kweli kabisa mtoa mada, ndiyo maana hata JPM alisisitiza sana kujiridhisha kwanza kabla ya kutumia chanjo tunazoletewa.

Hii inatokana na TBS kutokuwa na uwezo wa kung'amua ubora wa bidhaa tunazoletewa. JPM alimaanisha kwamba, kwenye ISSUE ya madawa na hasa ya binadamu, tukipata hizo dawa kwa kuwa hatuna uwezo huo wa kung'amua ubora wake, basi tunaweza kuchukua Sample tukaenda kupima hata nje ya Nchi kwa wenzetu wenye uwezo zaidi ili kujiridhisha kwanza kabla ya matumizi. Vivyo hivyo hata katika bidhaa zingine zote.
 
Ukitafakari mambo kwa kina sana unaweza kufikia hitimisho kwamba HATUNA serikakti!.
tuna kagenge fulani tu kanajiita watawala/viongozi ambako bahati mbaya sana kamehodhi kila kitu kuhusu maisha yetu wananchi.
 
Back
Top Bottom