Leo hii Tanzania imejaa bidhaa nyingi zenye ubora duni zilizotengenezwa China na ndani ya Tanzania, na kwa kiasi kidogo toka India na Thailand.
Leo hii, ni rahisi sana kuikunja nondo ya 16mm iliyotengenezwa Tanzania kuliko nondo ya 12mm iliyotengenezwa Kenya. Mathalani, ukienda dukani kutaka kununua nondo ya 6mm, utaulizwa unataka 6mm nene (imetengenezwa Kenya) au nyembamba (imetengenezwa Tanzania). Unajiuliza, hivi unene wa 6mm unawezaje kuwa na unene wa aina mbili? Ni sawa na mtu akuulize kama unataka kilo moja nyepesi na kilo moja nzito!!
Leo hii, siyo ajabu ukaingia dukani kununua kiatu kilichotengenezwa China, ukavaa asubuhi, jioni kikawa kimechanika.
Kwenye vifaa vya umeme na machinery, huko nako ni balaa. Kila duka zimejaa bidhaa za China, na kwa kukadiria, zaidi ya 70%, zina ubora hafifu kabisa. Mwaka 2017 nilinunua safety boot nchini Australia iliyotengenezwa China (made in China Australian standard) kwa Australian dola 100 (sawa kama U$80 au shilingi 170,000). Mwakajana nilinunua safety boot Dar iliyotengenezwa nchini China kwa shilingi 120,000. Ile ya Australia, mpaka leo, hakuna kilichobadilika, ni kama mpya, LAKINI ile ikiyotengenezwa China hukohuko lakini nikanunulia Dar, nilivaa miezi 4 tu, sole ilibanduka, na haikufaa tena. Huu ni mfano mdogo.
Kilicho dhahiri ni kuwa China inafahamika kwa kutengeneza bidhaa nyingi zenye ubora duni, na chache zenye ubora mzuri ambazo zinapelekwa kwenye mataifa ya watu wanaojitambua, na ambayo yana taasisi zenye uwezo mkubwa wa kupima na kudhibiti ubora.
Kilicho dhahiri hapa kwetu, TBS ni taasisi yenye ubora duni, itawezaji kudhibiti bidhaa zenye ubora duni? TBS ni duni kuanzia uwezo wa wataalam wake, vifaa na hata kimaadili. Wao wanachojali ni kulipwa pesa, ja siyo ubora.
Leo tuna mpaka bidhaa ndogo kama misumari ambayo ni ya kiwango duni kabisa. Misumari ambayo ukipiga kwenye ubao, kama ni hard wood, una uhakika wa zaidi ya 90% lazima utapinda au utashindwa kuingia kabisa.
Pendekezo:
Kwa kuwa taasisi yetu ya viwango haina kiwango, EAC iwe na taasisi moja tu ya kudhibiti viwango, ambayo itakuwa na wataalam wenye uwezo, nyenzo na maadili. Kwa bidhaa ambazo uwezo wa EAC kutambua ubora, ni mdogo, tuyaombe mataifa yenye uwezo kama Australia, tutumie viwango vyao. Mathalani bidhaa zitakazoruhusiwa kuingia nchini zilizotengenezwa China ziwe ni zile zenye label "Made in China Austrakia and EAC standards".
Taifa na watu wake tunapoteza pesa nyingi, tunapata hasara kubwa kwa kuingiza nchini bidhaa zenye ubora duni. Unaweza kununua bidhaa ya kiwango kizuri kwa shilingi 100,000 ikadumu kwa miaka 5, lakini unaweza kununua bidhaa yenye ubora duni kwa shilingi 50,000 halafu ikadumu kwa miezi 3 tu, ni bidhaa ipi inaendana na tjamani ya fedha yako? Watanzania tunaibiwa sana, na mataifa kama China kwa kuwa dampo la bidhaa duni, zisizofaa kuwafikia wateja. Hasara kubwa tuliyo nayo ni kuwa na shirika la viwango kama TBS lisilokuwa na viwango.