Uwezekano wa Bradley Effect Kwenye Matokeo ya Tafiti za REDET na SYNOVATE | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwezekano wa Bradley Effect Kwenye Matokeo ya Tafiti za REDET na SYNOVATE

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kulikoni Ughaibuni, Oct 17, 2010.

 1. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  [​IMG]

  Moja ya mambo yaliyokuwa yakiwaumiza vichwa wafuasi wa Barack Obama wakati wa kinyang'anyiro kati yake na Hillary Clinton kupata mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats mwaka 2008 ni theory inayofahamika kama Bradley Effect.Kwa kifupi kabisa,Bradley Effect (au Wilder Effect) ni hali inayoweza kutokea kwenye kura za maoni katika chaguzi nchini Marekani panapokuwa na mgombea Mweupe (White) na asiye mweupe (non-White).Pengine ili wasionekane wabaguzi wa rangi,wahojiwa Weupe katika kura za maoni hueleza kuwa chaguo lao ni mgombea asiye Mweupe au husema kuwa hawajafanya uamuzi kuhusu chaguo lao (Undecided).

  Kwahiyo,matokeo ya kura ya maoni yanaweza kuonyesha mgombea asiye Mweupe anapendwa zaidi kuliko mgombea Mweupe lakini inapofika kwenye hatua ya kupiga kura (ambapo mpiga kura anakuwa peke yake),wapiga kura Weupe wanampigia Mweupe mwenzao.

  Asili ya Bradley Effect ni katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa uchaguzi wa gavana wa jimbo la California mwaka 1982 ambapo licha ya mgombea Mweusi,Meya wa Jiji la Los Angeles Tom Bradley kuongoza kura za maoni,aliishia kushindwa uchaguzi huo kwa mgombea Mweupe George Deukmejian.

  Baadhi ya wachambuzi wa chaguzi nchini Marekani wanaamini pia kuwa Bradley Effect ilijitokeza tena kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa chama cha Democrats kwenye jimbo la New Hampshire ambapo licha ya Obama kuongoza katika kura za maoni,Hillary Clinton aliibuka mshindi kwenye jimbo hilo (japokuwa baadaye Obama alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla,na kupitishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Democrats,na hatimaye kushinda nafasi ya urais).

  Katika post hii najaribu kubashiri (hypothesize) namna Bradley Effect inavyoweza kuwa sababu ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,kuongoza katika tafiti za taasisi za Redet na Synovate kuhusu nafasi za wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa Tanzania hapo Oktoba 31.Hapa ntawazungumzia wagombea wawili tu,Kikwete na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

  Japo Bradley Effect 'halisi' inahusu mgombea Mweupe na asiye Mweupe,sababu inayopelekea matokeo ya kura kutorandana na mwelekeo wa kura za maoni inaweza kutumika kuelezea kwanini kura za maoni za Redet na Synovate zilimpa Kikwete ushindi na sio Dokta Slaa.Kama ilivyo kwenye chambuzi mbalimbali,kuna mambo flani inabidi 'kupuuzwa' ili kufikia matokeo yanayokusudiwa.Katika uchambuzi huu,naomba 'nipuuze' urafiki kati ya taasisi hizo na CCM na badala yake nikazanie kwenye uwezekano wa Bradley Effect pekee.

  Inawezekana kabisa kuwa wahojiwa kwenye tafiti za Redet na Synovate ni wananchi waliotoa majibu 'kuwaridhisha watafiti',yaani walisema wanampenda zaidi Kikwete kuliko Dokta Slaa.Moja ya sababu za kutoa majibu ya aina hiyo ni mazingira halisi ya Tanzania ambapo licha ya 'siasa za mkono wa chuma' za zama za chama kimoja kuonekana kama historia,ukweli unabaki kuwa baadhi ya wananchi wanaamini kuwa kusema lolote lisilowapendeza watawala ni kujitafutia matatizo.

  Naomba kufafanua kidogo katika hilo.Nilipokwenda Tanzania mwaka 2005 kufanya fieldwork ya utafiti wangu wa shahada ya uzamifu (PhD) nilikumbana na wakati mgumu kuwahoji baadhi ya maustaadh (mada yangu inahusu masuala ya Waislam na Uislam nchini Tanzania) kwa vile baadhi yao walidhani mie ni wakala wa serikali niliyetumwa kuwachunguza ili 'serikali iweze kuwadhibiti zaidi'.Bahati mbaya,fieldwork hiyo ilifanyika wakati jeshi la polisi lilikuwa linamsaka mwanaharakati wa Kiislam,Sheikh Issa Ponda.Ilichukua kitambo kujenga uaminifu kati yangu na maustaadh hao.

  Kuna wanaoilaumu Redet na Synovate kuhusu aina ya watu waliohojiwa wakidai kuwa huenda wahojiwa walikuwa watu walio karibu na CCM (kwa mfano mabalozi wa nyumba kumi).Uwezekano wa Bradley Effect 'yetu' (yaani isiyohusiana na ishu za ubaguzi wa rangi) ni mkubwa kwa vile wahojiwa wanaweza kutoa majibu yasiyoonyesha 'wanambagua mgombea wao' na hivyo kusema huyo ndio chaguo lao japo mioyoni wana dhamira na/au chaguo tofauti.

  Of course,inawezekana tafiti hizo za Redet na Synovate 'zilipikwa' ili kuendana na matakwa ya CCM.Inawezekana pia kuwa aina ya watu waliohojiwa ni ambayo isingetoa majibu tofauti na 'ushindi kwa Kikwete'.Lakini,kama makala hii inavyojaribu kubashiri,inawezekana kabisa kuwa wahojiwa 'waliwazuga' jamaa wa Redet na Synivate 'ili isiwe shida'.Nani yuko tayari kuona genge lake au kibanda cha biashara kinabomolewa kwa vile tu amechoshwa na namna CCM inavyozidi kuahidi maisha bora lakini wanaonufaika ni mafisadi pekee?Mtu wa aina hii haoni shida 'kudanganya leo' kisha 'akaungama siku ya kupiga kura' kwa 'kumwadhibu Kikwete na CCM kwenye sanduku la kura ambapo hakutokuwa na wa kumtoa mimacho kwanini hajampigia kura Kikwete au CCM'.

  Huu ni ubashiri tu.Unaweza kuwa sio sahihi lakini kama zilivyo bashiri nyingine-hususan zinazoambatana na mifano hai-unaweza kuwa na ukweli ndani yake.Kadhalika,Bradley Effect 'yetu' inaweza kutoa matokeo ya kuwashangaza wote wenye imani kuwa CCM na Kikwete watarudia kupata ushindi wa kishindo kama wa mwaka 2005.

  Pengine kuna watakaohoji kwanini Bradley Effect 'yetu' haiwezi kutumika kwenye utafiti mwingine (wa TCIB) unaoonyesha kuwa Dokta Slaa anaongoza.Jibu langu ni kwamba watoa maoni hawana cha kupata (nothing to gain) kuwadanganya watafiti kuwa wanampenda Dokta Slaa wakati ukweli wanayempenda ni Kikwete.Likewise,kwenye tafiti za Redet na Synovate,inawezekana baadhi ya wahojiwa walikuwa na cha kupoteza laiti wangesema hawampendi Kikwete (si unajua kuhusu umoja na mshikamano ndani ya chama?).Vilevile,yawezekana wahojiwa hawakuwa na cha kupoteza (nothing to lose) kwa kudanganya kuwa wanampenda Kikwete (kwa minajili ya kuwaridhishwa watafiti na 'kulinda ugali wao') kisha wakamnyima kura katika usiri wa chumba cha kupigia kura.

  Mwisho,naomba kusisitiza tena kuwa hypothesis hii imejaribu kupuuza sababu za 'wazi' kama vile upendeleo wa watafiti,uoga wa wahojiwa,na kubwa zaidi,UCHAKACHUAJI.

  KULIKONI UGHAIBUNI: Uwezekano wa Bradley Effect Katika Tafiti za REDET,Synovate
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,031
  Trophy Points: 280
  i know what you tried to mean! the article is true
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 419,846
  Trophy Points: 280
  In our election the Bradley effect is only in your conjuration. The only thing you can intelligently interject upon is the effect of what I call "inevitability" that may stampede the eventual winner with at most twenty percent more votes than he truly deserve because those voters do not want to vote in vain.......i.e by picking on eventual loser.................voters are humans and those undecided ones may pick on Dr. Slaa because there is an aura of inevitability around his candidacy implying the electorate contemplates he will emerge victorious.............................and that is where they would like to be identified with.........success.........this works all over the World - time and time around............................
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huyo Mzungu hakuwa na mabaya mengi sana kiasi cha kuwafanya wamchukie.

  Amini nakuambia, kama ingelikuwa jamaa na MBAYA sana Kitabia, ungelishangaa........

  Kama angelikuwa ni Rais Makini kidogo na Slaa yupo kama alivyo sasa, basi watu wangeliamini hili. Ndiyo maana zamani walikuwa wakitishwa, wanaamua wabaki na Mkapa kuliko kuingia kichwa kichwa kwa Mrema. Ila hii njia ya kutisha wameitumia sana hadi imeishiwa. Sasa kivumbi kimeanza maana watu wamechoka kweli kweli. Hebu soma hiki kituko na niambia kama watu bado watataka kumchagua mbunge kama huyu...

  Ameiandika Mpoki Bukuku "Mzee wa Sumo" katika blogu yake anasema,

  "Wagombea wengine bwana! Mmoja kaja kwetu kaahidi daraja la kisasa tuweze kuvuka mto kirahisi. Tukamwambia hatuna mto. Akaahidi kutuletea na mto pia."
   
 5. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sikuwa nimesikia hii kabla lakini can be true. Kwa TZ ukifika tu na makaratasi basi watu wanadhani wewe ni serikali na hapo lazima wakufunge kamba. Hii ni kwa sababu CCM ina elements nyingi za kikoloni na mtu anahofia maslahi yake
   
 6. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe kabisa Bradley Effect inaweza kutokea, fikiria wafanyabiashara wanaolazimishwa kuchangia CCM au kubandika picha za mgombea fulani kwenye biashara zao say daladala si kweli wote wanakipenda chama hicho ila wanafanya hivyo kulinda biashara zao, watu kama hao ni rahisi sana kudanganya kama watafikiwa na tafiti kama za REDET na Synovate.

  Mfano mwingine wa mwanasiasa aliye affected na Bradley Effect ni bwana mapesa John Cheyo yeye si kuwa anajionyesha kuipenda CCM kama wafanyabiashara wengine la hasha yeye anafanya kinyume chake anajifanya haipendi CCM ili aendelee kuwa upande wa upinzani aaminiwe na upinzani wakati huo huo akiendelea kutumiwa na CCM, kwa hiyo mtu kama huyo akifikiwa na utafiti hawezi kutoa hali halisi ilivyo na watafiti wataondoka na jibu tofauti na lililo moyoni mwa interviewee.
   
 7. Mnyisunura

  Mnyisunura Member

  #7
  Oct 17, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 69
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  This is true
  Leo nimetoka kuongea na kaka yangu kwenye simu nikamuuliza utamchagua nani! kwanza alianza kucheka akaniambia ngoja kidogo akaondoka alipokuwa. Baadae akaniambia nilikuwa naogopa kukuambiwa kuna watu wengi pale mi namtaka Dr. Slaa. Kwa hali ilivyo inaonekana ukisema ukweli unawekewa nembo na unakuwa matatani. Ni hii imejidhihisha kwenye mikutano ya Kampeni kamatulivyoona. Watu wako open zaidi kwa Dr. Slaa na wanajisikia huru kumwambia mtu wanayemtaka lakini si kwa kikwete. Ukisema humtaki flani mbele ya kikwete unakuwa matatani hivyo watu wabaki kimya lakini wanajua hawamtaki wanasubiri kumsulubu siku ya kupiga kura. Ni kama ule msemo wa akumulikae mchana usiku akuchoma!
   
 8. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #8
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  You lost me,Mr Public Policy Analyst.Could you kindly please explain in Swahili?
   
 9. Kulikoni Ughaibuni

  Kulikoni Ughaibuni JF-Expert Member

  #9
  Oct 17, 2010
  Joined: Dec 12, 2007
  Messages: 235
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Sikonge,

  Tatizo la ubaguzi wa rangi-ambalo ndio msingi wa Bradley Effect-linamfanya mhusika kufumbia macho maovu au unsuitability ya mgombea,na wakati huohuo kufumbia macho kila zuri la mgombea husika.Kwa wabaguzi hao,all that matters ni rangi ya mgombea.

  Mwanafilosofia wa Kifaransa Voltaire aliwahi kusema (namnukuu) "Prejudices are what fools use for reason".Kwa mbaguzi,anachoona kwa mlengwa wake ni mabaya tu,ikiwa ni pamoja na kutafsiri mazuri kuwa mabaya.Likewise,mbaguzi hujaribu kila awezavyo kutafsiri mabaya kuwa mazuri.

  Mfano wa mbali (ambao hauhusiani kwa karibu na ubaguzi) ni namna wanufaika wa ufisadi wanavyojaribu kutafsiri kila zuri la Dokta Slaa kuwa ni baya huku wakifanya kila wawezalo kugeuza kila baya la Kikwete kuwa ni zuri.Rasoning haina nafasi kwa viumbe wa aina hii,na pengine katika kuthibithsha hilo ndio maana wanakacha midahalo kwa vile itaibua reasoning.
   
Loading...