Kwa nchi za wengine Mdahalo ni njia nzuri sana ya kuwapima wagombea Ufahamu na Uelewa wa kujibu maswali ya papo kwa papo.
WanaArumeru watapata nafasi ya kutosha ya kuwasikiliza wagombea 'live', lakini Watanzania wengine wana kila sababu ya kusikia aina ya Mbunge anayegombea ili kuingia Bungeni kutunga sheria za nchi, ni wa aina gani, na ni njia ya Mdahalo wa wazi ndiyo inayoweza kuwapambanua hawa wawili, kiasi kwamba hata wapiga kura wanaweza kubadilisha mawazo baada ya kutazama mdahalo.
Naunga mkono hoja hii nzuri, Wajitokeze akina Mwakitwange waandae mdahalo utakaorushwa live nchi nzima!