Uwepo Mdahalo wa Wagombea Arumeru

bucho

JF-Expert Member
Jul 13, 2010
5,113
3,117
Ndg wananchi ingependeza kama vyombo vya habari hapa nnchini vingeandaa mdahalo wa moja kwa moja kati ya sio na nasary , hi ingesaidia wananchi kupima uwezo wao .

MNAONAJE HILI WAZO WAKUU ?
 
Ingekuwa vizuri sana kuwaona wakimwaga sera.
 
Kwa nchi za wengine Mdahalo ni njia nzuri sana ya kuwapima wagombea Ufahamu na Uelewa wa kujibu maswali ya papo kwa papo.

WanaArumeru watapata nafasi ya kutosha ya kuwasikiliza wagombea 'live', lakini Watanzania wengine wana kila sababu ya kusikia aina ya Mbunge anayegombea ili kuingia Bungeni kutunga sheria za nchi, ni wa aina gani, na ni njia ya Mdahalo wa wazi ndiyo inayoweza kuwapambanua hawa wawili, kiasi kwamba hata wapiga kura wanaweza kubadilisha mawazo baada ya kutazama mdahalo.

Naunga mkono hoja hii nzuri, Wajitokeze akina Mwakitwange waandae mdahalo utakaorushwa live nchi nzima!
 
Tatizo magamba watamkatalia sioi asishiriki kwa vile wanajua kamanda Nasary atamsambaratisha huku umma wa watanzania ukishuhudia.
 
Ndg wananchi ingependeza kama vyombo vya habari hapa nnchini vingeandaa mdahalo wa moja kwa moja kati ya sio na nasary , hi ingesaidia wananchi kupima uwezo wao .

MNAONAJE HILI WAZO WAKUU ?
Naunga Mkono HOJA,lakini kwa kuongezea tu, mdahalo uwe wa wagombea wote (hata wale wasindikizaji)
 
yaani wakubwa mnataka SIOLEWI akose posa kabisa?? mbona mnamtia majaribuni na midahalo yenu?? chondechonde jamani lo!!!
 
Mtu ambaye anafaa kuongoza awe fair kwa wagombea asiwe na upendeleo wowote.
 
yaani wakubwa mnataka SIOLEWI akose posa kabisa?? mbona mnamtia majaribuni na midahalo yenu?? chondechonde jamani lo!!!

hatutaki lugha chafu na kejeli hapa . Nenda kule kwenye utani sio hapa .
 
Itabidi na yeye ajinyonyoe manyoya kama KAFU, ila kuhusu kuitwa SIOLEWI siyo lugha chafu ni kinyume cha jina lake kwani mm ndo nilimbatiza jiana hiho?
 
Itabidi na yeye ajinyonyoe manyoya kama KAFU, ila kuhusu kuitwa SIOLEWI siyo lugha chafu ni kinyume cha jina lake kwani mm ndo nilimbatiza jiana hiho?

haina haja ya maneno mengi tuandae mdahalo ili tupime uwezo wao wote wawili.
 
FANYENI NA WAGOMBEA WA VYAMA VInGINE SISI TULISHANYIMWA NA MAKAMBA,HATUSHIRIKI NGOOOOOOOOOOO
 
Back
Top Bottom