Chadema, kimeomba kufanyika mdahalo wa wagombea wote wa ubunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ili kutoa fursa kubwa kwa wapigakura wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla, kuwafahamu.
Meneja Mwenza wa kampeni wa Chadema, Vincent Nyerere, alitoa ombi hilo jana katika mikutano ya kampeni ya chama hicho, katika Kijiji cha Kikatiti na Maleu, wakati mgombea ubunge wa chama hicho, Nassari akiomba kura.
Nyerere ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini, alisema uchaguzi wa Jimbo la Arumeru Mashariki unasura ya kitaifa, hivyo ni busara kutoa fursa kwa Watanzania wengi kuwajua wagombea, sera zao na nini wamejipanga kuwafanyia wakazi wa jimbo hilo.
"Sisi Chadema tunataka wagombea wengine wakubali hasa CCM ambao wamekuwa wakikacha midahalo ili tutowe fursa kwa Watanzania kuwajua wagombea wao kwani kipindi cha kampeni ni kifupi sana, hivyo hakitowi nafasi wagombea kujulikana,"alisema Nyerere.
My take: Naunga mkono hoja -Mdahalo utasaidia sana wapiga kura kuwaelewa wagembea na mambo wanayoyasimamia.