Uwekezaji unatuletea pesa za kigeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwekezaji unatuletea pesa za kigeni?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Honoje, Jun 15, 2010.

 1. H

  Honoje New Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: Jun 14, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwekezaji unatuletea pesa za kigeni?

  Ninawasiwasi na hili na kama ni kweli basi ni la muda mfupi tu. "Privatization" wakati wa serikali ya awamu ya tatu ulikuwa mkubwa mno. fedha za kigeni zilijaa, kila kona. je, ni nini kinachotokea baada ya muda mfupi? nadhani ni wawekezaji kupata faida kubwa - mabillion ya fedha za kitanzania (Madafu). kwa fedha ndogo walizoleta hawa tuliowauzia mashirika yetu, teyari fedha zao zimesharudi mara nyingi tu. kwa hiyo fedha za madafu walizo nazo wanatakiwa wazichukue kwenda makwao. je watapata wapi fedha za kigeni walizotuletea muda mfupi uliopita? nadhani watazipata kwenye mabenki yetu, maduka ya kubadilishia fedha, nk. matokeo yake ,ni dola kuwa adimu na kushusha dhamani ya shilingi yetu.
  ningeshauri tu, tujitahidi sana sana kuhakikisha faida kubwa inayozalishwa hapa nchini inabaki hapa hapa. tusaidiane sis wenyewe sio tu kukimbilia 10% ya dola chache na kuwaruhusu wageni kuondoka na mamillion ya dola kila mwaka. shilingi yetu itazidi kudorora tu tusipokuwa makini. Tujiulize, ni nini tunachozalisha na kuuza nje ya Nchi ili kituingizie pesa za kigeni? ni wazalendo wangapi waliwezeshwa katika kununua haya mashirika ya Umma yaliyobinaifishwa? Wa-asia ndiyo wanaakili zaidi au badi tu, tunaonea wivu kuona mswahili anamiliki kiwanda. hotel, nk?
   
Loading...