Kanyunyu
JF-Expert Member
- May 2, 2012
- 335
- 495
Vijana wazawa wa Singida wameanza kurejea Nyumbani na kufanya uwekezaji mkubwa hasa Ujenzi wa nyumba za kuishi na hotel za kibiashara
REGENCY HOTEL AND RESORT ni Hotel ya kisasa kabisa iliyozinduliwa hivi karibuni na ni moja ya kazi nzuri iliyofanywa na mzalendo na mzawa wa Singida ndugu Raymond Nkingo ambae alienda kutafuta pesa nje ya mkoa wa Singida na Sasa amerudi kuwekeza Nyumbani kwa kujenga hotel ya kisasa kabisa yenye gorofa 9 , Regency Hotel ipo ufukweni mwa Ziwa Singida ikiwa na mandhari mazuri Sana
Uwekezaji wa hotel ni kichocheo kikubwa cha maendeleo mkoani Singida kwa kuwa itasaidia kutoa ajira kwa Vijana, kuvutia wageni na wadau kuwekeza mkoani Singida
Kwa miongo kadhaa wazawa wa Singida wamekuwa na msukumo mdogo kuwekeza Nyumbani, wengi waliofanikiwa kusoma na kupata fedha wamewekeza mikoa ya Arusha na Dar
Tunawakaribisha wadau wote kuja kuwekeza Singida kwani ni centre nzuri ya kibiashara hasa kuelekea mpango wa serikali kuhamia Dodoma
Singida ya jana, sio Singida ya Leo
#Transforming_Singida