Uwekezaji Singida washika kasi

Uwekezaji Singida washika kasi

Mkuu ni Maziwa kweli au ni mito? hilo ziwa singida linatoka wapi kwenda wapi? I mean linaanzia singida kwenda wapi na linaishia wapi?
Ujuaji mwingi mbele Giza!... toka lini duniani uliona ziwa linatoka hapa kuelekea kule? limekuwa mto au mfereji? unajua ziwa linatokanaje? tofauti yake na bwawa, MTO na mfereji unajua? muulize mwl kaijage akusaidie!
 
Nilishtuka nikajua Leo tarehe 01 April, ghorofa 3 una sema 9? Mikakati yenu ya marketing inahitaji maboresho makubwa sana.
 
Vijana wazawa wa Singida wameanza kurejea Nyumbani na kufanya uwekezaji mkubwa hasa Ujenzi wa nyumba za kuishi na hotel za kibiashara

REGENCY HOTEL AND RESORT ni Hotel ya kisasa kabisa iliyozinduliwa hivi karibuni na ni moja ya kazi nzuri iliyofanywa na mzalendo na mzawa wa Singida ndugu Raymond Nkingo ambae alienda kutafuta pesa nje ya mkoa wa Singida na Sasa amerudi kuwekeza Nyumbani kwa kujenga hotel ya kisasa kabisa yenye gorofa 9 , Regency Hotel ipo ufukweni mwa Ziwa Singida ikiwa na mandhari mazuri Sana

Uwekezaji wa hotel ni kichocheo kikubwa cha maendeleo mkoani Singida kwa kuwa itasaidia kutoa ajira kwa Vijana, kuvutia wageni na wadau kuwekeza mkoani Singida

Kwa miongo kadhaa wazawa wa Singida wamekuwa na msukumo mdogo kuwekeza Nyumbani, wengi waliofanikiwa kusoma na kupata fedha wamewekeza mikoa ya Arusha na Dar

Tunawakaribisha wadau wote kuja kuwekeza Singida kwani ni centre nzuri ya kibiashara hasa kuelekea mpango wa serikali kuhamia Dodoma

Singida ya jana, sio Singida ya Leo

#Transforming_Singida

View attachment 417107
Ajira kwa kahoteliii kamoja tyuu... Makubwa
 
Ujuaji mwingi mbele Giza!... toka lini duniani uliona ziwa linatoka hapa kuelekea kule? limekuwa mto au mfereji? unajua ziwa linatokanaje? tofauti yake na bwawa, MTO na mfereji unajua? muulize mwl kaijage akusaidie!

Jibu Swali, hilo ziwa lililopo Singida linatokea wapi kwenda wapi? kwani ukijibu swali utakuaje? kama unajua jibu.

Ziwa Victoria limeunganisha nchi kadhaa, Tanganyika limeunganisha nchi kadhaa, sasa hilo ziwa lililopo singida linapita wapi hadi wapi?

Najua siyo lazima liunganishe nchi kadhaa hilo ziwa kutokana na Formation yake, sasa swali langu hilo ziwa Singida limepita wapi?
 
Mimi Singida nilipafurahia kipindi napita hapo na Gogo kwenda shule, yaani kuna sehemu nadhani salanda tukifika tunakula nyama mpka kuchoka, unakuna na mtu kwenye behewa anauza mishikaki ya maini, sinia limejaa. Yaani nikawa nikijiuliza ina maana huku bei ya maini ni ndogo kuliko nyama yenyewe au?
 
Aisee maajabu yani mkoa mzima mnashangilia kujengwa kwa hotel ya horofa tatu!!?VP bado mjazindua na lift uko?mkizindua mtaniambia
 
Mimi Singida nilipafurahia kipindi napita hapo na Gogo kwenda shule, yaani kuna sehemu nadhani salanda tukifika tunakula nyama mpka kuchoka, unakuna na mtu kwenye behewa anauza mishikaki ya maini, sinia limejaa. Yaani nikawa nikijiuliza ina maana huku bei ya maini ni ndogo kuliko nyama yenyewe au?
Yaani hapo ulikula kila aina ya mnyama na ndege lakini maadam msafiri kafiri haina shida
 
Jibu Swali, hilo ziwa lililopo Singida linatokea wapi kwenda wapi? kwani ukijibu swali utakuaje? kama unajua jibu.

Ziwa Victoria limeunganisha nchi kadhaa, Tanganyika limeunganisha nchi kadhaa, sasa hilo ziwa lililopo singida linapita wapi hadi wapi?

Najua siyo lazima liunganishe nchi kadhaa hilo ziwa kutokana na Formation yake, sasa swali langu hilo ziwa Singida limepita wapi?
Singida kuna ziwa usiishi kwa Ku cremisha
 
Kweli mna kiu ya uwekezaji!
Mpaka huu mnausifia hivi!!!
Kweeeeli mna hamu muwekezewe!!!

Unataka kutuambia wawekezaji wa kichaga waliowekeza hapo singida miaka kibao walikuwa wanakosea maana walipaswa kuwekeza kwao Kilimanjaro.

Sijui mmelogwa na Mwigulu au Nyalandu?
Wachagga oyeeee.
 
Ghorofa zuri singida ni lile lenye duka la madawa la BLUE na zilipo ofisi za NHIF ni hayo tu na TRA lilokaa kizamani huyo mzushi aache uongo uwekezaji singida bado litakuwa ni lisisiemu hilo na majengo yao ya Zuluma baada ya vyama vingi 1992 yakashindwa kumalizia maviwanja na majengo
 
Naona umeamua kutangaza biashara tunaomba ulipie tafadhali
 
Jibu Swali, hilo ziwa lililopo Singida linatokea wapi kwenda wapi? kwani ukijibu swali utakuaje? kama unajua jibu.

Ziwa Victoria limeunganisha nchi kadhaa, Tanganyika limeunganisha nchi kadhaa, sasa hilo ziwa lililopo singida linapita wapi hadi wapi?

Najua siyo lazima liunganishe nchi kadhaa hilo ziwa kutokana na Formation yake, sasa swali langu hilo ziwa Singida limepita wapi?
Ziwa Volcano halina chanzo kasome tena geography
 
Hakuna ghorofa 9 sgd, jengo refu lina ghorofa 4 ambayo ni jengo la uhamiaji(rangi ya bluu) liko karibu na mahakama ya wilaya,Singapore bado sana wazee tukaze buti,tatzo wanyampaa hata mwamko wa kuwahoji viongozi wetu juu ya maendeleao ya mkoa wetu hatuna,ccm wametufanya ni mtaji wao,wako radhi wahonge wakati wa uchaguzi lkn sio kuwaletea maendeleao. Kapita pale mhindi miaka kumi lkn alichokifanya ni 0.01%. Bado sana ila tutafika hata kwa kutambaa
 
Back
Top Bottom