ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,019
- 7,223
Tuambiane ukweli.
Tukishaambiana ukweli, tufanye maamuzi.
Tukishafanya maamuzi, tukubali kuishi na matokea ya maamuzi yetu.
Kumekuwa na kauli kuwa uwekezaji kwenye uchimbaji mafuta na gesi ni wa gharama kubwa kiasi kwamba wawekezaji wa ndani hawana uwezo wa kumudu gharama yake.
Kauli hii imeungwa mkono na watu wengi, lakini wote walioinga mkono wana sifa moja - sio wadadisi.
Kwa mujibu wa hotuba ya Rais. Kisima kimoja kinagharimu dola za kimarekani milioni 100. Kwa bei ya dola ya sasa hii ni sawa na shilingi bilioni 160.
Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Dau katika mada aliyoitoa katika mkutano wa tatu wa wadau wa NSSF alisema kuwa NSSF inao uwezo mkubwa wa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali. Hata hivyo uwezo huo wa NSSF hautumiki ipasavyo kwa vile miongozo ya uwezekezaji inaizuia NSSF kuwekeza katika maeneo hayo.
Dola milioni 100 kwa NSSF sio pesa nyingi na wala sio pesa inayoshindwa kuwekeza kwenye kisima cha mafuta iwapo miongozo ya uwekezaji ingetoa ruhusa kwa mifuko ya hifadhi za jamii kuwekeza kwenye maeneo hayo.
Kwa lugha nyingine ni kwamba sisi wenyewe tunakataa wawekezaji wetu wa ndani kuwekeza kwenye uchimbaji mafuta na gesi, kwa kuweka miongozo inayowakataza kufanya hivyo.
Dkt. Ramadhan Dau akitoa Mada kwenye Mkutano wa 3 wa Wadau wa NSSF II- MICHUZI MEDIA - YouTube
Katika tovuti ya NSSF wameweka jedwali la miradi waliyowekeza na gharama zake. Katika jedwali hilo inonyeshwa kuwa NSSF imewekeza shilingi bilioni 277.9 katika jengo la College of humanities and social science ya chuo kikuu cha Dodoma - UDOM katika kipindi cha mwaka 2008-2011.
Projects
Kama kwenye mradi mmoja tu NSSF imewekeza bilioni 277.9 ambazo ni nyingi kuliko shilingi bilioni 160 za kuchimba kisima kimoja cha mafuta, je NSSF haina uwezo wa kuwekeza kwenye mafuta? Je, mifuko mingine ya hifadhi haina uwezo wa kuwekeza kwenye uchimbji mafuta na gesi?
Mimi nadhani watanzania tuangaliane tena machoni halafu tuulizane kama tuko tayari kuishi na matokeo ya maamuzi tunayoyafanya hivi sasa.
Kupanga ni kuchagua...