Uwekezaji Kwenye Mafuta na Gesi - Gharama Ziko Ndani ya Uwezo Wetu...

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Tuambiane ukweli.

Tukishaambiana ukweli, tufanye maamuzi.

Tukishafanya maamuzi, tukubali kuishi na matokea ya maamuzi yetu.

Kumekuwa na kauli kuwa uwekezaji kwenye uchimbaji mafuta na gesi ni wa gharama kubwa kiasi kwamba wawekezaji wa ndani hawana uwezo wa kumudu gharama yake.

Kauli hii imeungwa mkono na watu wengi, lakini wote walioinga mkono wana sifa moja - sio wadadisi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais. Kisima kimoja kinagharimu dola za kimarekani milioni 100. Kwa bei ya dola ya sasa hii ni sawa na shilingi bilioni 160.

Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Dau katika mada aliyoitoa katika mkutano wa tatu wa wadau wa NSSF alisema kuwa NSSF inao uwezo mkubwa wa kuwekeza kwenye miradi mbalimbali. Hata hivyo uwezo huo wa NSSF hautumiki ipasavyo kwa vile miongozo ya uwezekezaji inaizuia NSSF kuwekeza katika maeneo hayo.

Dola milioni 100 kwa NSSF sio pesa nyingi na wala sio pesa inayoshindwa kuwekeza kwenye kisima cha mafuta iwapo miongozo ya uwekezaji ingetoa ruhusa kwa mifuko ya hifadhi za jamii kuwekeza kwenye maeneo hayo.

Kwa lugha nyingine ni kwamba sisi wenyewe tunakataa wawekezaji wetu wa ndani kuwekeza kwenye uchimbaji mafuta na gesi, kwa kuweka miongozo inayowakataza kufanya hivyo.

Dkt. Ramadhan Dau akitoa Mada kwenye Mkutano wa 3 wa Wadau wa NSSF II- MICHUZI MEDIA - YouTube

Katika tovuti ya NSSF wameweka jedwali la miradi waliyowekeza na gharama zake. Katika jedwali hilo inonyeshwa kuwa NSSF imewekeza shilingi bilioni 277.9 katika jengo la College of humanities and social science ya chuo kikuu cha Dodoma - UDOM katika kipindi cha mwaka 2008-2011.

Projects

Kama kwenye mradi mmoja tu NSSF imewekeza bilioni 277.9 ambazo ni nyingi kuliko shilingi bilioni 160 za kuchimba kisima kimoja cha mafuta, je NSSF haina uwezo wa kuwekeza kwenye mafuta? Je, mifuko mingine ya hifadhi haina uwezo wa kuwekeza kwenye uchimbji mafuta na gesi?

Mimi nadhani watanzania tuangaliane tena machoni halafu tuulizane kama tuko tayari kuishi na matokeo ya maamuzi tunayoyafanya hivi sasa.

Kupanga ni kuchagua...
 
NSSF ina miradi mingi iliyowekeza pia bado aijaanza kulipa. na NSSF inaendeshwa kwa pesa za wafanyakaz hivo haiwezi kurisk pesa za watu kwenye miradi mikubwa na RISK kama gas.

kuwekeza kwenye gas kunaitaj mitaji mikubwa si ya kubahatisha na ujue kwamba wakat mwingine mitambo inalipuka hivo ukiwa na mitaji ya kubahatisha ni janga.

Zile pesa za NSSF si zao hivo usitegemee wa risk pesa za watu
 
Ni mradi gani waliowekeza NSSF ambao hauna risk?

Msikilize Dr. Dau kwenye paper yake anavyoelezea hasara ambayo nssf inapata kwa kuwekeza kwenye treasury bills. Miongozo inawalazimisha kuwekeza huko na wanapata hasara.

Katika takwimu ulizonazo, ni makampuni mangapi yamechimba gesi na mafuta kwa hasara?

Hapa naona kuna dhana nyingine inayojengeka kuwa kuchimba mafuta ni biashara ya pata potea. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameondoa pata potea kwenye uchimbaji mafuta na gesi.

Hakuna biashara isiyo na risk...
 
Tuwe wakweli Jeuri ya waziri na katibu mkuu wizara ya nishati na madini inathibitisha wizi na ufisadi mkubwa wa hawa watu. Maswi hawezi sema vikampuni vya akina mengi, watanzania hakuna anaeweza kuwekeza ni dharau kubwa na isiyo vumilika. 120bn si fedha nyingi kwa wafanyabiashara watanzania kuchimba kisima baharini na si nyingi 40bn kuchimba nchi kavu. tumefika hapa kwa kodi za hivi vikampuni vinavyodharaulika. labda wamesahau kwamba walipakodi wakubwa ni watanzania na si wawekezaji wa nje. Rushwa imewapa jeuri na kiburi hawa watu.
 
Ndio maana inabidi tuangaliane machoni na tuulizane kama tuko tayari kuishi na matokeo ya maamuzi tunayofanya...
 
...

Kauli hii imeungwa mkono na watu wengi, lakini wote walioinga mkono wana sifa moja - sio wadadisi.

Kwa mujibu wa hotuba ya Rais. Kisima kimoja kinagharimu dola za kimarekani milioni 100. Kwa bei ya dola ya sasa hii ni sawa na shilingi bilioni 160.

Mkurugenzi wa NSSF, Dr. Dau ....

Kupanga ni kuchagua...

... daah, haya bhana! Naona hili la gesi hujaishia kwenye msuli tu, bali umelivalia kikoi na mkongojo umeushika kisawasawa. Sijui ni matusi ya Prof. kwa wawekezaji wa ndani yamekutibua, ama...?! Unanikumbusha ishu ya Sheikh Ponda alipopigwa risasi, jinsi vile ulivyoreact...

... all in all, yaonekana kutetea maslahi ya Taifa kwa manufaa ya wengi kwako wewe kunakuja pale tu interests zako zinapokuwa directly impacted na maamuzi ya "wateuliwa wasio wadadisi!"

... ama kweli, kupanga ni kuchagua!
 
Mkuu Steve Dii,

Sina kumbukumbu ya kureact Ponda alipopigwa risasi. Kuna uwezekano unachanganya watu.

Lengo la thread hii ni kukumbushana kuwa wawekezaji wenye uwezo tunao, ila iko miongozo inayowakataza kuwekeza.

Baada ya kuambiana ukweli tutafanya maamuzi ambayo tutawajibika kupokea matokeo yake.
 
walienda ku-bid wazawa maana amna mtu aliezuiwa, ukitoa huko marekani tena kwenye vijivisima vidogo vya mafuta huko Texas kwengine biashara ya gas na mafuta ni pretty much an oligopoly industury, hata Russia akina Abromovich wote wamerudisha visima na serikali inashirikiana na big players only kwenye soko la mbali.

Mchakato wa kusafirisha gesi kuitoa Tanzania mpaka inapokwenda mbali na ukishaipata ni a different case, gharama za kiwanda chake si ya biashara ya na juice na matunda. Vitu vingine ni kujifurahisha tu embu fanya kuangalia hii biashara inavyofanyika na players wakoje halafu ndio ujue ni kitu gani tunataka kutetea kwa wale walio upande wa wazawa tutasubiri miaka mia hamna mtanzania atakae weza kuwekeza huko binafsi hata akipewa mkopo na benki unless na yeye atafute partners kama serikali inavyofanya na main players ni wale wale tu maana ndio wanao control masoko ya nje na kwenye mahitaji makubwa ya gesi.
 
Kukata tamaa siku zote ni jambo rahisi kuliko kufanya jitihada. Hata hivyo mkata tamaa anapaswa kujua jinsi ya kuishi na matokeo ya kukata tamaa...
 
Havard is private, Princeton is private, Cornell is private, yale is private, berkerly califonia is private, stanford is private. Hii ni mifano ya private industries zilizofanikiwa. Sasa si kina kabokomchizi na mzee kabwela serikali ndo mama, baba, mjomba, shangazi kaka dada, the alfa and omega. So parthetic!!

Ni Serikali ya watu makabwela tu ndo inawaza kwa kutumia ubongo wa panzi. Open up men!! Acheni kudanganya these besutiful people of tanzania.
 
Kukata tamaa siku zote ni jambo rahisi kuliko kufanya jitihada. Hata hivyo mkata tamaa anapaswa kujua jinsi ya kuishi na matokeo ya kukata tamaa...
Kukata tamaa kunatokana na sababu nyingi ignorance, ability and the ways things work (or chances).

You can challenge on chances, lakini likija swala la ability kununua ugomvi na simba utaishia kuwa kitewoe hizo ni facts kwa binadamu bila ya kuwa na silaha. Ndio kama unavyoona walienda ku-bid kwenye hivyo vitalu hao wazawa, huo huwezo hawana.

Mkuu hivi unajua hata hayo mafuta wachezaji wakubwa (mataifa) yanapangiwa how much to pump in quota's from OPEC and the likes. Usidhani kwakua unamafuta ndio unaweza kuuza unavyotaka wewe, maana ukikaidi Saudi Arabia wanaweza ku-pump mafuta na kukizi mahitaji ya dunia wao pekee kwa muda mrefu sana kwa bei chee, wao ndio wana control prices kwa sasa. Kwa hivyo those who are in this business understand the risk and the way things operate and are not in any hurry to recoup their investment.

Mkuu unatetea tu hapa huo huwezo wa watanzania kwenda wenyewe kwenye mafuta hawana unless washinde bid na watafute external investors same thing the government is doing.
 
Havard is private, Princeton is private, Cornell is private, yale is private, berkerly califonia is private, stanford is private. Hii ni mifano ya private industries zilizofanikiwa
Hao wapo kwenye uwekezaji wa mafuta na gesi. Kwani issue ni private ownership tu, au kuwapa wazawa nafasi ambapo huwezo hawana.
 
Ni mradi gani waliowekeza NSSF ambao hauna risk?

Msikilize Dr. Dau kwenye paper yake anavyoelezea hasara ambayo nssf inapata kwa kuwekeza kwenye treasury bills. Miongozo inawalazimisha kuwekeza huko na wanapata hasara.

Katika takwimu ulizonazo, ni makampuni mangapi yamechimba gesi na mafuta kwa hasara?

Hapa naona kuna dhana nyingine inayojengeka kuwa kuchimba mafuta ni biashara ya pata potea. Maendeleo ya sayansi na teknolojia yameondoa pata potea kwenye uchimbaji mafuta na gesi.

Hakuna biashara isiyo na risk...

wewe unataka NSSF ifilisike kwanza haina uzoefu na biashara hiyo ya gas.

Uwekezaji wa gas ni mkubwa .uwezo wetu ni wa kuwekeza kwenye viwanda vya juice,soda, ngano na mikate.

hivi unakumbuka BP ilivyotozwa fine ya dolla billion 10 na marekan kwa kuaribu mazingira na ikalipa fasta.

hiyo dolla billion 10 ata bajet ya nchi aifiki hiyo pesa. uwekezaji wa gas mkuu ni mkubwa ata juzi Rais kikwete alisema hakuna bank inayoweza toa mkopo wa kuwekeza apo.
 
tatizo hamna utaalamu wa mafuta na gas mnapost kila siku humu.
unajua garama za kutafiti gas ni kiasi gani
unajua garama za kujenga mitambo ya kuchimba gas offshore? PDO na PIO?
unajua garama ya kujenga bomba za kuleta gas onshore?
unajua garama za kujenga kiwanda cha kuchuja hiyo gas na kuiprocess?? LNG plant?
Tusijidanganye hakuna mtanzania anaeweza kufanya yote haya.
.kisima hakijengwi tu bila kuwa na miundo mbinu yote hiyo......
kama alivosema waziri Muhongo watanzania hatuna huo uwezo kifedha,,
Tunajidanganya tunaweza lakini ukweli hatuwezi labda makampuni kumi makubwa tanzania yaungae ndio yaweze kujenga plant kwenye block moja tu
makampuni makubwa kama statoil, BP wanahisa na nchi zao zinawapa fedha hizo
Msichanganye ishu ya mafuta na gas na siasa, its not easy as you think guys
soma post zangu katika mada zilizotangulia kuhusu mada hii hiii utanielewa.
TUTABAKI TUNAJIDANGA UKWELI HATUNA HUO UWEZO...
 
mkuu bora na wewe umeongea maana watu wanaingiza siasa umu na wala awajafanya utafiti kuhusu uwekezaji wa gas wanajua uwekezaji wa gas ni sawa na kuanzisha kiwanda cha juice au unga
 
Lokissa na stunna mna mawazo ya kitumwa. Nawafananisha na Nwoye mtoto wa Okwokwo kwenye kitabu cha Chinua Achebe "things fall apart" mvivu na mwoga.

mnaridhika serikali yenu kukopa fedha word bank kwa ajili ya kujengea matundu ya choo na kuwafundisha watu kunawa mikono, Nilidhani mngepiga kelele kuitaka serikali kukopa huko benki ya dunia ili mchimbe gesi na mafuta yenu.

Wazungu walikubaliana na waarabu ya kuwa kusichimbwe gesi wala mafuta Afrika, kwa upande mwingine waarabu wakaunda OPEC ili kuwa na soko la pamoja la mafuta ili kudhibiti bei, hii OPEC ni zaidi ya shetani kwani gharama za uchimbaji wa mafuta hazitajwi kupanda lakini wao OPEC wanaongeza bei ya mafuta ghafi kwa kasi ya ajabu. huu ni unyonyaji.

Kumbukeni hata huko saudi arabia wamarekani wameajiriwa kuchimba mafuta, tunashindwa nini kuwaajiri waingereza kutuchimbia mafuta! tuanawaogopa wakoloni wetu. Tukakope benki ya afrika, tukajifunze na kupata uzoefu Venezuela kwa HUGO CHAVEZ.
 
Last edited by a moderator:
tatizo hamna utaalamu wa mafuta na gas mnapost kila siku humu.
unajua garama za kutafiti gas ni kiasi gani
unajua garama za kujenga mitambo ya kuchimba gas offshore? PDO na PIO?
unajua garama ya kujenga bomba za kuleta gas onshore?
unajua garama za kujenga kiwanda cha kuchuja hiyo gas na kuiprocess?? LNG plant?
Tusijidanganye hakuna mtanzania anaeweza kufanya yote haya.
.kisima hakijengwi tu bila kuwa na miundo mbinu yote hiyo......
kama alivosema waziri Muhongo watanzania hatuna huo uwezo kifedha,,
Tunajidanganya tunaweza lakini ukweli hatuwezi labda makampuni kumi makubwa tanzania yaungae ndio yaweze kujenga plant kwenye block moja tu
makampuni makubwa kama statoil, BP wanahisa na nchi zao zinawapa fedha hizo
Msichanganye ishu ya mafuta na gas na siasa, its not easy as you think guys
soma post zangu katika mada zilizotangulia kuhusu mada hii hiii utanielewa.
TUTABAKI TUNAJIDANGA UKWELI HATUNA HUO UWEZO...

Kama unachokisema ndiyo uhalisia basi tusichimbe iachwe humo humo ardhini.... tuendelee kuibiwa haya madini mengine mpaka yatakapo kwisha.... Hata Tanzanite tunaambiwa hatuna uwezo wa kuchimba.... yes hatuna mitaji...hatuna mitambo ya kisasa... ndiyo lugha ya watawala....Kukiwa na utashi wa kuwawezesha wazawa wanauwezo wa kuchimba au kumiliki kwa ubia....hakuna kisichowezekana hii ni kwasabubu ya kutokuwapo kwa sheria wala sera inayoongoza uchimbaji huu..ndo sababu ya mikataba hii ya santakalawe amina ..mwenye kupata apate ...mwenye kukosa akose..!?
 
Sisi waTanzania tunaweza kuanzisha na kuendesha viwanda vya Juice na sio Gas...
 
Nchi nyingi wananchi hawakuwa nauwezo lakini kuliwekwa sera,sheria na kanuni za kuwajengea wazawa uwezo ndio maana leo hii petrobrass,stato oil wameweza kuja huku tanzania nakuja kuwekeza,ukiangalia hili jambo utagundua haliendi sawa ndo maana kuna mkanganyiko
 
[/QUOTE]unajua garama za kujenga mitambo ya kuchimba gas offshore? PDO na PIO?
unajua garama ya kujenga bomba za kuleta gas onshore?
unajua garama za kujenga kiwanda cha kuchuja hiyo gas na kuiprocess?? LNG plant?
Tusijidanganye hakuna mtanzania anaeweza kufanya yote haya.
.kisima hakijengwi tu bila kuwa na miundo mbinu yote hiyo......

TUTABAKI TUNAJIDANGA UKWELI HATUNA HUO UWEZO...[/QUOTE]

Kama wewe huwezi basi wapo wanaoweza!
 
Back
Top Bottom