Uwekezaji kupitia UTT

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Sep 29, 2012
3,409
0
Unit Trust Fund of Tanzania (UTT)
Katika maelezo niliyoyapata kidogo kwenye internet ni kwamba wananchi wanawezw kufaidika kupitia wao kwa kununua hisa, but how does it works? Ni hisa kiwango gani cha chini (minimum) ambacho mwananchi anaweza kununua? Hisa zao zinafaida?

Mwenye taarifa kamili kuhusu hawa watu amwage taarifa zote hapa.
 
Ruge Opinion

JF-Expert Member
Mar 22, 2006
1,829
2,000
UTT hawauzi hisa ila wanauza vipande (units). Muundo uko hivi: unanunua vipande vya mfuko mmojawapo wa UTT (Jikimu, Liquid, n.k.) kwa bei ambayo itakuwepo kwenye soko siku unanunua. UTT itachang'anya hiyo pesa yako pamoja na za wawekezaji wenzako na kutafuta fursa nzuri za kuziwekeza. Itaziwekeza kwenye hisa za makampuni (Company Shares), Amana za Serikali (Government Bonds/Treasury Bills), Amana za makampuni (Corporate Bonds) na fursa zingine zenye hatarisho (risk) ndogo. Kila UTT inapopata faida kutokana na uwekezaji huo na thamani ya kila kipande cha aliyewekeza kwenye mfuko inaongezeka. Kwa mfano, kama wakati unanunua bei ya kila kipande ilikuwa Sh. 200 baada ya muda ukitaka kuuza bei ya kipande inaweza kuwa Sh. 250, ikiwa na maana utapata faida ya Sh. 50 kwa kila kipande. Hivyo ukubwa wa faida utakayopata utategemea vile vile ulinunua vipande vingapi. Ununuzi na uuzaji wa vipande ni rahisi kwa sababu hautegemei kuwepo mteja wa kununua kutoka kwako bali ni UTT/Mfuko wenyewe ndiyo unauza na kununua hivyo vipande.
 
Nashukuru sana mkuu, kwa maelezo yako mi nadhani ni bora kununua hisa kuliko kununua vipande UTT? we una mtazamo upi? unadhani wapi ni bora zaidi na kwanini? asante
 
xfactor

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
1,511
1,250
UTT hawauzi hisa ila wanauza vipande (units). Muundo uko hivi: unanunua vipande vya mfuko mmojawapo wa UTT (Jikimu, Liquid, n.k.) kwa bei ambayo itakuwepo kwenye soko siku unanunua. UTT itachang'anya hiyo pesa yako pamoja na za wawekezaji wenzako na kutafuta fursa nzuri za kuziwekeza. Itaziwekeza kwenye hisa za makampuni (Company Shares), Amana za Serikali (Government Bonds/Treasury Bills), Amana za makampuni (Corporate Bonds) na fursa zingine zenye hatarisho (risk) ndogo. Kila UTT inapopata faida kutokana na uwekezaji huo na thamani ya kila kipande cha aliyewekeza kwenye mfuko inaongezeka. Kwa mfano, kama wakati unanunua bei ya kila kipande ilikuwa Sh. 200 baada ya muda ukitaka kuuza bei ya kipande inaweza kuwa Sh. 250, ikiwa na maana utapata faida ya Sh. 50 kwa kila kipande. Hivyo ukubwa wa faida utakayopata utategemea vile vile ulinunua vipande vingapi. Ununuzi na uuzaji wa vipande ni rahisi kwa sababu hautegemei kuwepo mteja wa kununua kutoka kwako bali ni UTT/Mfuko wenyewe ndiyo unauza na kununua hivyo vipande.

So far hawa UTT wamewekeza kwenye kampuni zipi au miradi ipi?

Najua kuwa wapo kwenye ule mradi wa kupima na kuuza viwanja Lindi japo mimi nimeona ile kama ni move ambayo haikuwa smart sana kwa sasa maana vitachelewa sana kulipa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom