“Uwatendee Raia Kama Wazazi Wako” - Rais Xi Jinping wa China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
1.jpg


Mwezi Januari, 2008 Mji wa Guizhou ulipokumbwa na maafa ya mvua, theluji na barafu, Xi Jinping alipokuwa mjumbe wa kudumu wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama na Katibu wa Ofisi ya sektretarieti ya Kamati Kuu ya Chama alikwenda nyumbani kwa mwanakijiji Tang Shaowei kuwapa pole

“Ni lazima tukumbuke kuwa serikali yetu ni ya umma”, “Umuhimu wa umma akilini mwa maofisa huamua umuhimu wa maofisa akilini mwa umma”, “Kila wakati, tunapaswa kupendana na umma, kwa kuchukulia furaha yao kama furaha yetu, na maumivu yao kama maumivu yetu na kushikamana na kushirikiana vizuri nao”.... Mara kwa mara Bw. Xi Jinping ameelezea upendo wake wa dhati kwa wananchi katika vipindi na sehemu tofauti.

Bw. Xi anawakumbuka wananchi kila wakati, maneno aliyosema yanakaribia wananchi na amejitolea kwa ajili ya maslahi ya wananchi. Upendo wake kwa wananchi unatokana na malezi yake ya kipekee.

Kuanzia mwaka 1962, wakati baba yake Bw. Xi Zhongxun, aliyekuwa ofisa mwandamizi wa Chama cha Kikomunisti cha China alipokosolewa na kufedheheshwa, hivyo mtoto wake Xi Jinping alihusishwa na kesi yake na kukabiliwa na ubaguzi. Wakati wa “Mapinduzi ya Utamaduni”, alifedheheshwa hadharani, aliwahi kukumbwa na njaa, aliwahi kurandaranda na hata alitiwa kizuizini.

Mwanzoni mwa mwaka 1969, alipokuwa chini ya umri wa miaka 16, alifanya kazi katika kijiji kimoja kilichoitwa Liangjiahe katika Wilaya ya Yanchuan, kaskazini mwa Mkoa wa Shaanxi nchini China. Katika nyumba yake kulikuwa na viroboto wengi, ambao walimwuma sana na kila mara alilazimika kuwaua kwa kutumia dawa za kilimo.

2.jpg

Xi Jinping, mwaka 1972 aliporudi nyumbani Beijing kutoka kijijini.

Maisha ya kijiji kilichoko kaskazini mwa mkoa wa Shaanxi yalikuwa magumu lakini alikichukulia kijiji hicho kama jukwaa lake la kwanza la utendaji wa kazi, na kuonesha uwezo wake mkubwa. Ili kuongeza eneo la mashamba ya kilimo, aliwaongoza wakulima kujenga boma kwenye ardhi yenye matope katika majira ya baridi, ambayo wakati huo hakuna kazi nyingi za kilimo, huku akisimama peku kwenye ardhi yenye barafu kutoboa barafu na kutengeneza msingi wa boma. Pia aliwashirikisha wahunzi pale kijijini kuanzisha Ushirika wa kutengeneza vyombo vya kilimo ili kukidhi mahitaji ya kijijini pia kuviuza hivyo katika vijiji vingine ili kuongeza mapato ya ushirika.

Baada ya kusoma gazeti alipata habari kuhusu watu wa sehemu moja mkoani Sichuan walizalisha gesi ya kinyesi, hivyo alikwenda sehemu hiyo kujifunza kutoka kwao, baada ya kurudi kijijini kwao alijenga shimo la kwanza la gesi, baadaye aliwaongoza wanakijiji kukijenga kijiji chao kiwe kijiji cha kwanza cha matumizi ya gesi ya kinyesi katika Mkoa wa Shaanxi, nishati ya gesi iliyozalishwa kijijini humo imetosheleza mahitaji ya wanakijiji katika kupika chakula na kwa matumizi ya taa. Bw. Xi alipofanya kazi kijijini humo, kila mara aligawanya mikate ya ngano kwa wanakijiji, na yeye mwenyewe kula makapi ya mkate. Aliwahi kusifiwa kuwa kijana mtangulizi wa kuigwa na kutunukiwa pikipiki yenye magurudumu matatu na serikali kuu, pikipiki hii ya wakati ule ilikuwa ni yenye thamani kijijini lakini alitafuta njia ya kuibadilisha kuwa trekta na mashine ya kusaga unga, kupepeta ngano na pampu ya maji, ambavyo vilihitajika sana kwa wanakijiji wa kijiji alichoishi.

3.jpg

Xi Jinping (kulia) Mwaka 1977 alipokuwa mwanafunzi wa
Chuo Kikuu cha Qinghua.

Mwaka 1975, Xi alichaguliwa kusoma katika Chuo Kikuu cha Qinghua. Katika siku yake ya kuondoka kijiji, wanakijiji wote walipanga foleni ya kumwaga, wengi wao walilia na hata baadhi yao walimsindikiza mbali sana. Wanakijiji walimzawadia feremu yenye cheti cha kumsifu kuwa ni “Katibu mzuri wa wakulima maskini”.

Baada ya kuondoka kijijini huko Shanbei, Bw. Xi siku zote anawakumbuka wanakijiji wa huko. Siku za baada ya hapo, alikisaidia kijiji kupata umeme, kujenga daraja na kukarabati shule ya msingi.

Bw. Xi aliwahi kusema, waliompa msaada mkubwa zaidi maishani mwake ni “wanamapinduzi wakongwe na wanakijiji wenzake wa Mkoa wa Shanxi”. Kwani alipokwenda kijiji cha mkoani Shanxi, alikuwa mtoto mwenye umri wa chini ya miaka 16, wakati huo kwa muda mfupi alikuwa hajui lolote; alipoondoka huko alikuwa kijana mwenye umri wa miaka 22, mwenye nia thabiti ya kutimiza lengo la maisha yake – “Nitafanya kazi halisi kwa ajili ya wananchi”.

4.jpg



Xi Jinping, Mwaka 1983 alipokuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Wilaya ya Zhengding ya Mkoa wa Hebei, aliweka meza mtaani akikaa kusikiliza maoni ya wakazi wa huko.

Mwaka 1988 Bw. Xi alikuwa Katibu wa Kamati ya Chama ya Sehemu ya Ningde mkoani Fujian, sehemu hiyo ilikuwa moja kati ya sehemu 18 zenye hali ya umaskini zaidi wakati huo nchini China.Ili kutembelea vijiji vyote vya sehemu hiyo, mara kwa mara alipanda gari aina ya jipu kusafiri kwa siku kadhaa mfululizo mlimani kwenye njia mbovu sana kiasi kwamba baadhi ya wakati alitingishwa vibaya garini hata alishindwa kushuka kwenye gari kutokana na maumivu kiunoni. Katika sehemu za mbali milimani zisizo na barabara ya kupita magari, alitembea kwa miguu kwenye njia yenye hatari zilizojaa matope. Siku moja alitembea kuanzia saa moja na nusu asubuhi, na mpaka saa sita na zaidi mchana akafika kwenye Tarafa ya Xiadang. Alipofika huko alikaribishwa kwa uchangamfu na shangwe, wanakijiji wa huko walisema, yeye ni “Ofisa mkubwa wa kwanza aliyetembelea tarafa hiyo”. Kadhalika alihimiza kazi ya kuwasaidia wakulima wapatao elfu kadhaa kukarabati nyumba zao mbovu za nyasi, huku akiwajengea makazi wavuvi waliokuwa wakiishi kwenye meli kizazi baada ya kizazi, na kuwawezesha waende baharini kuvua samaki, baadaye wakae kwenye nyumba mpya kandoni, na kuishi maisha ya utulivu na furaha.

Katika mkesha wa Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa 2005 wa China, Bw. Xi alikwenda kwenye Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Changguang mkoani Zhejiang, akapanda kigari kufika chini ya kimo chake karibu ni mita 1,000, kisha akatembea kwa zaidi ya mita 1,500 chini ya chimbuko akiwa aliinama na kutembea kwa kufuata kijia cha chimbuko chenye kimo fupi na chembamba, ili kuwatembelea wachimba mgodi.

Bw. Xi anatilia maanani sana kuwasiliana na watu kwa kupitia vyombo vya habari. Aliandika makala 232 kwenye safu ya gazeti la Zhejiang Daily, akitumia jina Zhe Xin. Katika makala hizo, alijibu maswali ya umma yanayohusiana zaidi na maisha yao. Maneno aliyotumia kwenye makala yake yalikuwa rahisi na kueleweka kirahisi na kukaribishwa sana na watu, ambao walimsifu kwa kusema “alitumia maneno ya kawaida kujadili matatizo makubwa”.

5.jpg

Novemba 3, 2013, Xi Jinping alipofanya ukaguzi mkoani Hunan, aliongea na maofisa na wanakijiji katika Kijiji cha Shiba Dong cha Tarafa ya Paibi wilayani Huanyuan katika eneo linalojiendesha la kabila la Watujia na Wamiao la Xiangxi
Ingawa Bw. Xi ni mtu mwadilifu na mtulivu lakini anashikilia kanuni sana katika kushughulikia makosa yanayodhuru maslahi ya umma. Mara kwa mara anawahimiza maofisa kufanya kazi kwa ajili ya umma badala ya wao wenyewe. Wakati alipochunguza kesi ya ujenzi haramu wa nyumba za maofisa wa Ningde, alikasirishwa sana na malalamiko ya maofisa, aligonga meza kwa hasira huku akiuliza, “Mnataka tuwachukize maelfu ya maofisa, au tuwachukize mamilioni ya umma?” Alipofanya kazi mkoani Zhejiang, alisukuma mbele ujenzi wa maadili mema kwa nguvu kubwa, na katika mwaka mmoja, maofisa wengi waliadhibiwa kutokana na kuzembea kazi.

Kutokana na utendaji wake na upendo wake kwa umma, alipewa jina la “katibu mkuu kama raia wa kawaida”. “Kwa sisi wakoministi, raia ni kama wazazi wetu wa kutulisha, ni lazima tuwapende kama wazazi wetu na kufanya kazi kwa ajili ya maslahi yao na kuwapatia maisha bora,” Xi alisema.
 
Kutokana na utendaji wake na upendo wake kwa umma, alipewa jina la “katibu mkuu kama raia wa kawaida”. “Kwa sisi wakoministi, raia ni kama wazazi wetu wa kutulisha, ni lazima tuwapende kama wazazi wetu na kufanya kazi kwa ajili ya maslahi yao na kuwapatia maisha bora,” Xi alisema.
Sasa wasio wakoministi wao wanawaoba raia kama kitu gani? Nasubiri majibu.
 
Namkubali Sana Kamanda Xi Jinping ni Rais bora kwa wakati huu hapa duniani. Role model wangu
 
Back
Top Bottom