Uwanja wa Taifa (Uhuru) Unabomolewa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwanja wa Taifa (Uhuru) Unabomolewa!

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kakalende, Apr 18, 2011.

 1. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Nimepita leo asubuhi, jukwaa la kijani limeshaporomoshwa chini, na tingatinga linaendelea kubomoa!

  Nakumbuka uwanja huu uliachwa kwa nafasi yake katika historia ya UHURU wa Tanganyika, ndio maana Wachina wakajenga uwanja mpya pembeni.

  Huyu aliyeamua ubomolewe; hata kama ni Magufuli, atuambie ametumia sheria ya mwaka gani?
   
 2. F

  Froida JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Yaani nchi hii hatutaweka kitu chochote cha historia kama ni kweli basi mawazo yangu nitasikitika sana
   
 3. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Elezea vizuri mkuu, mbona habari kama ina-hang?
   
 4. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  Taarifa za uhakika zinasema uwanja huo unakarabatiwa kwa kujenga jukwaa la ghorofa mbili kuanzia eneo lililopkuwa green stand hadi kwenye mzunguko wote..(kwa walalahoi) ili litakapokamilika watu wengi zaidi wapate fursa ya kuketi kwa raha zao wakiwa uwanjani hapo. Kwa sababu hiyo uwanja huo sasa umefungwa kwa muda hadi kazi hiyo itakapokamilika.
   
 5. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Nani anyefanya funding ya mradi huo?
  Je ni TFF?...Wizara husika?...Na je ndiyo kipaumbele kwa sasa?...kuna uharaka huo wa uwanja kupanuliwa ukilinganisha na mahitaji mengineyo hata ndani ya wizara hiyohiyo?
  Je si watu wachache wameamua kujipatia maisha kwa njia hiyo?
  Kumbukumbu zangu pia zinasema kuwa uwanja huo wa Uhuru ni sehemu ya Historia ya nchi, na utabaki kama ulivy
  o!
   
 6. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  tunashukuru kwa taarifa nzuri. kwani siyo vibaya kuboresha historia.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  naona unaongea kwa uchungu sana,
  hii ni nchi ya ajabu sana isiyo kuwa na vipaumbele kwa sasa, huo uwanja kwa sasa hauna umuhimu wala uharaka wa kujengwa ili hali watoto wanakalia vumbi kusoma (hayo macement yangeweka sakafu madarasa mangapi?)

  watu wamekaa na kuamua kutengeneza kazi ili mambo yao yaende
   
 8. Dr wa ukweli

  Dr wa ukweli JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 892
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  jamma anajitahidi kutimiza ilani ya vya siasa alianza na ya chadema sasa anatimiza APPT Maendeleo
   
 9. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Pamoja na hayo je wizara au TFF kama wameamua kuupanua kiasi hicho, je hakuna maeneo mengine nchi hii ambayo hayahitaji viwanja?

  Kwa nini kubanana Dsm wakati maeneo mengi tu ya nchi hii hakuna viwanja....sijui ni lini serikali itajua vipaumbele
   
 10. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Duuhh!! Mkuu umenifanya nimecheka...sijui akimaliza ataanza na ya chama gani tena....labda cha Dovutwa kama takrima ya kumwombea kura dakika za mwisho
   
 11. Silas Haki

  Silas Haki JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 368
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata kama kuna uharaka, kwa nini watanzania tuna akili mbovu zinazofikiria kukarabati vitu vile vile tena kwa gharama sawa na kujenga uwanja mwingine mpya? Kwa nini tusifikirie kuongeza viwanja vingine vipya sehemu mbalimbali za nchi yetu ili kunapokuwa na mashindano timu zisipate taabu ya viwanja? Uwanja wa uhuru uko pua na mdomo na uwanja wa taifa, kwa nini tuendelee kuwazia kupanua uwanja wa uhuru wakati kuna uwanja mzuri hapohapo unaoweza kutumika kama tutaona kuwa uwanja wa uhuru unazidiwa uwezo?
   
 12. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  National Stadium (Dar Es Salaam)[​IMG]

  Mkuu umepost bila kuleta data za kutosha na "wanahistoria" wananchanganyikiwa kwa kuto kuwa na background ya kutosha.
  Lakini hizi lawama ni za bure, si wengi wananelewa kuwa katika uhai wake ,kiwanja hiki cha uhuru kimepitia maboresho mengi sana.
  "Green Stand" haikuwa hivyo zamani , ilikuwa ya steel structure ambayo ilikuwa hatari sana na kuna wakati ilipiromoka kwa uzito wa watazamaji.
  Lango kuu la kutokea Indoor stadium miaka iliyopta halikuwepo na lilijengwa katika maadhimisho ya kitaifa zaidi ya miaka 30 iliyopita.
  Hata hiyo tartan surface ya riadha imewekwa si miaka mingi iliyopita.
  Zaidi ya yote si wengi wanaofahamu kuwa mahala hapa kilikuwa kiwanja cha ndege wakati wa vita kuu ya pili na Indoor Stadium ilikuwa hangar la ndege.Na mimi nikiwa mdogo nimechezea ndege zilizoharibika nyuma ya In Stad.

  History is only relative
  Hata hivyo Mkapa atakumbukwa kwa hii stadium mpya na ya kisasa, a stadium of International standards, lakini in 100 years itakuwa history.
  Benjamin Mkapa National Stadium[​IMG]

  [​IMG]
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  TFF siyo uwanja wao hivyo ukuu panua hawawezi...
   
 14. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Maandalizi ya sherehe kubwa ya miaka 50 ya uhuru, jk anataka watu wajae palw decembar 9,2011
   
 15. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kutumia kodi zetu kwa staili hii ni upumbavu.
   
 16. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kinyesi!
  hivi wewe ndo wale waliosapoti nyumba za serikali ziuzwe ili zijengwe zingine? hebu toa pumba zako hapa. back to topic; hebu tujifunze kutokulaumu na kulalama kila kitu, mtu mwenye data kamili aje nazo hapa, nani anabomoa? nini kitafuata? fundi zimetoka wapi? na ni kwa malengo yapi? at least from there tunaweza anzu kujadili. si kurukia rukia tu mara tff mara wizara.
   
 17. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #17
  Jun 21, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  DSM Sports Complex
   

  Attached Files:

  • dsm.bmp
   File size:
   667.2 KB
   Views:
   23
Loading...