Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,851
- 15,265
Uwanja mdogo wa ndege kisongo ambao mara nyingi hutumika na watalii wanaokodi ndege ndogo kwenda kutalii katika hifadhi za taifa na sehemu za serengeti, ngorongoro na sehemu nyingine zenye vivutio vya utalii, hauna kabisa hadhi ya kuitwa uwanja wa ndege kwa maisha ya kileo. Maana muonekano ni ule ule wa kizamani.
Nyasi na majani., kiwanja hichi cha Ndege ambacho hutumika na ndege ndogo za watalii na abiria Wa ndani ya nchi, Nyasi na majani yamejitoea hovyo ndani ya uwanja na hakuna mpangilio maalum unaonekana wa ukataji wa Nyasi hizo bali ni ule wa hovyo hovyo na sehemu nyingine ndani ya uwanja huo nyasi na majani hazijakatwa bali zimeachwa zijiotee vyovyote vile.
Taa hasa upande unaongalia barabarani maana uwanja huu upo kando ya barabara hii ya kisongo kuelekea monduli na kuelendelea, ni barabara kubwa na muhimu kwani ndio inayotumika na Mabasi yanayoenda Mwanza, singida Dodoma na Pia ndio bara bara kuu inayopitisha watalii kwenda hifadhini lakini ukiangalia vizuri eneo hilo ni giza Mida ya usiku.
Mabango, Kwa hadhi ya kuitwa uwanja mdogo wa kitalii kulipaswa kabisa pembeni ya uwanja na hata kwenye uzio huo ambao unaangalia barabarani basi wengeweka mabango yenye picha yanyoonyesha wanyama wanaopatikana hifadhini, na hata vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi zetu ingependeza na kuvutia zaidi na kufanya uwanja kuwa katika hadhi yake.
Pia majengo yaliyomo ndani ni ya kizamani na hayana muonekano mzuri