Mbona kuna nchi nyingi tu Duniani si ajabu hata nyingine ni Tajiri kiuchumi kuliko Dubai na hazina Uwanja kama huo? Kumbuka sio swala la kujenga tu, bali ni swala la mahitaji na Vipaumbele, sasa kama Ndege zinazotua Dar kwa Siku hata tano hazifiki Uwanja kama huo utakuwa na Maana gani? kumbuka Miji kama Dubai na mingineyo kila dakika ndege inatua na kupaa ukiaangalia ubao wa Matangazo mpaka sehemu ya kuandika hakuna ndege zinazotua na kupaa, hivyo ni sawa kwao kuwa na Uwanja kama huo kwani wana hayo mahitaji!
Sisi kwetu hatuhitaji huo Uwanja bali tunahitaji madawati shuleni, Chakula cha kutosha kwa watu wetu yaani milo 3 tu kwa siku, Bara bara za vijijini na Mijini, tunahitaji umeme wa uhakika sasa hv ktk nchi yetu ya milioni 40 ni asilimia 14 tu ndio wana umeme sasa Dubai ni 99%, tunahitaji maji ya kunywa masafi kwa watu wetu sasa hv TZ watu wenye maji nyumbani hawafiki hata asilimia 15 wakati Dubai 100%!
Sasa unaona hapo, hivyo Uwanja kama huo kwetu hautakuwa na maana yoyote ni sawa tu raisi Mkapa alivyokwenda kutumia dola za Kimarekani miloni 40 kununua radar ambayo haina matumizi TZ kwa maana hatuna hiyo teknolojia!