Uwajibikaji ni uzalendo wa kweli kuliko utumbuaji majipu

Oct 26, 2010
52
29
Rais wetu mpendwa kazi anayofanya ya kutumbua majipu ni nzuri sanaaaa.... Lakini jambo hilo linampa sifa yeye kama yeye na wal ai serikali yake... Nionavyo mim ni heri awabane na kuwalazimisha watu anaowatumbua waresign wenyewe kabla ya kuwatumbua... Hii ingekua inawatia watu moyo zaidi maana tatizo letu hatuna hali ya uwajibikaji... Mtu akijiudhuru na watu waliochini yake wakaona... Kesho na keshokutwa watawajibika bila hata ya Rais kuwatumbua... Ila kwa hali ilivyo sasa akiondoka Mh... Rais basi tutarudi kulekule... Maana hatuna mfano wa mtendaji yeyote aliejitoa bila kutumbuliwa...
 
Mtu anafanya madudu katika wadhifa aliopewa, na haoni kama anafanya madudu au anahisi ni haki yake. Hapo tu inaonesha jinsi asivyo na uzalendo, sasa unategemea atajiwajibisha aje ikiwa wala haoni kuwa analofanya si sahihi? Ni kweli pengine mwisho wa uongozi wa sasa tukarudi kwenye uozo tena, hapo ni sheria na uwajibikaji wa kila mtu na taasisi unahitajiwa.
 
Kwa niaba ya Rais,utumbuaji majibu ni sehemu ya uzalendo Na uwajibikaji.kulazimisha watu wa jiudhuru wenyewe sio majukumu ya Rais.
 
Back
Top Bottom