Uvumilivu una kikomo chake

Uvumilivu una kikomo chake

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2015
Posts
14,242
Reaction score
34,917
Kama nilivyosema jana jioni; Uvumilivu siku zote huwa una kikomo chake. Hatuwezi tena kuendelea kujificha kwenye kivuli cha kile kinachoitwa amani ni tunda la roho wakati roho zetu zikiwa na huzuni kila tuamkapo.

Wale wanaoitangaza hii Amani; ukiwatazama kwenye kwapa zao, wameficha Visu na Mapanga. Nchi gani hii ya kidemokrasia.

Ninachoweza kusema; hata hiyo Demokrasia ya Kenya, Uhuru wa Bunge lake na Mahakama ama ule wa Vyombo vya habari uliopo Kenya hivi sasa; haukupatikana kwenye sahani kama kipande cha Mkate. Kuna watu wali-sacrifice maisha yao kwa ajili ya watoto na wajukuu wao, leo hii Wakenya wanaishi raha mstarehe.

Ikumbukwe kuwa; Wakenya walichoshwa na udharimu uliokuwa unafanywa na KANU enzi zile na wakaamua kwa gharama yoyote ile kuidai Katiba Mpya iliyowasaidia kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi hatimaye dhamira yao ya kuing'oa KANU ikatimia.

Muda na wakati wa kuonyeshana meno na CCM na Watu wake haupo tena; hawa walishadhamiria kung'ang'ania madaraka na hawatakuwa tayari kuona wanawekwa benchi kwa hii kitu inaitwa Uchaguzi.

Sisi tufanye siasa kupitia haya majukwaa ya chaguzi ndogo; lakini tutambue kwamba, dhamira ya CCM ni dhamira hasi iliyojaa uovu ndani yake.
 
Hii paragraph yako imenichekesha sana, ''
''Ikumbukwe kuwa; Wakenya walichoshwa na udharimu uliokuwa unafanywa na KANU enzi zile na wakaamua kwa gharama yoyote ile kuidai Katiba Mpya iliyowasaidia kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi hatimaye dhamira yao ya kuing'oa KANU ikatimia''.

Tatizo la copy&paste kutoka kwenye mitandao na kuleta Jamiiforums.

KANU haikuondolewa madarakani kwa sababu ya katiba mpya.

Kwa kukusaidia naomba utambue kuwa KANU iliondolewa madarakani Desemba 2002 wakati katiba ya Kenya iliundwa mwaka 2010.

Jielimishe kwanza kabla ya kuleta uharo hapa Jamiiforums!
 
Utakua ni UPUMBAVU uliozidi kipimo kama upinzani utaingia kwenye chaguzi yoyote ile chini ya Tume ya Uchaguzi inayoteuliwa na Rais Mr. Stone. Narudia tena utakua ni UPUMBAVU usio na mfano.
 
Kuna jamaa alikuwa mmoja wa waangalizi kwny kituo kimojawapo cha kupiga kura huko ukonga jana, anasema mahali hapo waliojiandikisha kupiga kura: 498
waliopiga kura: 65
Nadhani hii inaweza kuwapa sign ccm ni kiasi gani wananchi wa kawaida wamewachoka
 
Mwanahabari huru wa HOVYO kabisa kutokea hapa duniani!
Kwa taarifa yako tu CCM NI CHAMA TAWALA na kama HUTAKI ama HAMA NCHI au KUFA!
True walahi!
Alafu lilivyo jinga halijui kuwa KANU BADO INATAWALA NI MAJINA YA CHAMA NDIO YANABADILIKA!
Ovyo kabisa walahi!
9E19FD93-FA9F-4EE4-8E81-1C00DF895B0B.jpeg
 
Hii paragraph yako imenichekesha sana, ''
''Ikumbukwe kuwa; Wakenya walichoshwa na udharimu uliokuwa unafanywa na KANU enzi zile na wakaamua kwa gharama yoyote ile kuidai Katiba Mpya iliyowasaidia kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi hatimaye dhamira yao ya kuing'oa KANU ikatimia''.

Tatizo la copy&paste kutoka kwenye mitandao na kuleta Jamiiforums.

KANU haikuondolewa madarakani kwa sababu ya katiba mpya.

Kwa kukusaidia naomba utambue kuwa KANU iliondolewa madarakani Desemba 2002 wakati katiba ya Kenya iliundwa mwaka 2010.

Jielimishe kwanza kabla ya kuleta uharo hapa Jamiiforums!
hahaa hao ndo wasomi wa ufipa na habari zao uchwara.
 
Tulishavurugwa na gia ya angani 2015 maradhara yake Ndio haya.

Tusubiri tena hadi 2035
 
Back
Top Bottom