bigmind
JF-Expert Member
- Oct 28, 2015
- 12,457
- 12,705
Rafiki yangu, mwanahabari huru tuache jazba turudie akili yetu na tutafakari pia.Kama nilivyosema jana jioni; Uvumilivu siku zote huwa una kikomo chake. Hatuwezi tena kuendelea kujificha kwenye kivuli cha kile kinachoitwa amani ni tunda la roho wakati roho zetu zikiwa na huzuni kila tuamkapo.
Wale wanaoitangaza hii Amani; ukiwatazama kwenye kwapa zao, wameficha Visu na Mapanga. Nchi gani hii ya kidemokrasia.
Ninachoweza kusema; hata hiyo Demokrasia ya Kenya, Uhuru wa Bunge lake na Mahakama ama ule wa Vyombo vya habari uliopo Kenya hivi sasa; haukupatikana kwenye sahani kama kipande cha Mkate. Kuna watu wali-sacrifice maisha yao kwa ajili ya watoto na wajukuu wao, leo hii Wakenya wanaishi raha mstarehe.
Ikumbukwe kuwa; Wakenya walichoshwa na udharimu uliokuwa unafanywa na KANU enzi zile na wakaamua kwa gharama yoyote ile kuidai Katiba Mpya iliyowasaidia kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi hatimaye dhamira yao ya kuing'oa KANU ikatimia.
Muda na wakati wa kuonyeshana meno na CCM na Watu wake haupo tena; hawa walishadhamiria kung'ang'ania madaraka na hawatakuwa tayari kuona wanawekwa benchi kwa hii kitu inaitwa Uchaguzi.
Sisi tufanye siasa kupitia haya majukwaa ya chaguzi ndogo; lakini tutambue kwamba, dhamira ya CCM ni dhamira hasi iliyojaa uovu ndani yake.
CCM siyo wajinga, eti chadema wapewe uhuru na kuitukana na kudhalilisha chama tawala kizembe kiasi hicho.
Hivi kwa akili tu ya kawaida mnategemea Mh. Mbowe huyuhuyu ninayemfahamu ongoze chadema kufanya maoinduzi/mageuzi kuiondoa CCM?? Hizi ndoto za mchana tena mkiwa post mpya saa 8 za mchana.
Mbowe sina uhakika kama anajua ata theory walau moja ya kimapinduzi/mageuzi duniani. Msifanye siasa ni nyepesi kuasi kile imani yenu juu ya Mbowe porojo za majukwaani ndipo mnamuona anaweza ila mkae mkijua strategically he is too poor. Chadema ilikiwa dr. Slaa wala si mtu mwingine kitendo cha kuwapoteza watu kama akina ZITTO, KITILA, dr. SLAA ilikuwa pigo sana wengi hamukuona.
Hamuwezi kuifanya elimu kitu kisicho hitajika kiasi hiki mpk mfikirie Mbowe aongoze taasisi inayotaka kupora/kipokea madaraka kwa CCM kwanza fikirieni CDM siyo tu kiuongozi iko vibaya bali ata kitaasisi iko hoi kuliko mnavyojiaminisha. Politics is several miles apart from political rallies lazima ihusishe ujasus, ujengaji wa taasisi na uchumi kwa chama.
Mikakati ya Mbowe sawa na kubeti tatu Mzuka tu, ni ujinga na kukosa maono ukiangalia hali ya kisiasa ya chadema na kushindwa kutumia fursa ya wasomi hasa vijana, kwa zaidi ya miaka 10 kuna vijana wengi wasomi walitakiwa kutumika kujijenga na kujiimairisha mwishowe CCM wamestuka na kuziba mianya yote mnabakia kupiga kelele tu.
Wengi sasa hivi mnafikiri zaidi kutia nguvu zaidi ya akili, ni kweli kwa kiasi fulani rafu zipo na ni kawaida kwa mtu aliyeshika madaraka hasa Africa lakini je, hiyo ndiyo ibaki sababu tosha ya kwanini chadema inashindwa si kweli kabisa.
Mwisho, CHADEMA hasa Mbowe atambue hawa wanao hama si kweli kwamba wanahongwa na kuhaidiwa vyeo, waweza kubisha kwasababu tu umeona waliohama wamepewa ila ni kwasababu wengi wao ni watu makini waliona hakuna future chadema na kwa ccm ni lulu maana walikuwa wameishiwa vijana wenye maono. Mh. Rais JPM anakili kuwa amewanyanganya silaha upinzani lazima awatungue nazo.
Ni hayo tu kwa leo.