Uvumi umezagaa NEC imo kwenye hati hati ya kuuahirisha uchaguzi huu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uvumi umezagaa NEC imo kwenye hati hati ya kuuahirisha uchaguzi huu...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 19, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 69,694
  Likes Received: 3,200
  Trophy Points: 280
  Tetesi za kuahirisha uchaguzi huu zinazidi kushika kasi kwa sababu ya mazingira yafuatayo:-

  1) CCM hawapo tayari kushiriki uchaguzi huu baada ya kufahamu wapigakura wanaghadhabu kubwa na ya muda mrefu dhidi yao kutokana na utendaji wao duni. Uzoefu wa mwaka 1995 wa Mkoa wa Dar-Es-Salaam unawahamasisha CCM kuishinikiza NEC kuahirisha chaguzi hii.

  Mwaka 1995, NEC iliahirisha chaguzi ile kutokana na uzembe wa makusudi wa NEC yenyewe katika kusambaza vifaa vya kupigia kura na ilifanya hayo yote kwa manufaa ya CCM. Uchaguzi uliporudiwa mahudhurio yalikuwa kiduchu kutokana na wapigakura kuchoshwa na usumbufu tajwa na CCM ilipeta.

  2) Tetesi za TRA kukamata kura haramu za "NDIYO" kwa JK hata kabla ya makabrasha ya NEC kuwasili nchini na kusambazwa yanaleta picha ya kuwa "mtihani" umevuja na dawa ni kuurudia tu. Yaani zoezi zima lianze upya na makaratasi yenye NEMBO tofauti yakachapishwe upya. Hii itahitaji muda zaidi wa maandalizi yasiyopungua mwezi mmoja hivi na chaguzi itakuwa imeahirishwa.

  Bila ya kufanya hivyo imani ya wapigakura ya kuwa uchaguzi huu ulikuwa ni huru na wa haki hautakuwepo kwa sababu hatujui ni kiasi gani ya kura haramu za kumbeba JK tayari zimo nchini na hazijashikwa na hivyo kuharamisha uhalali wa uchaguzi huu.

  3) Ili kuwapooza viongozi wa kikristu ambao walilalamikia NEC kuichagua siku ya Jumapili ambayo ni siku ya ibada katika kupiga kura sasa itakuwa ni sababu sindikizi ya kuahirisha uchaguzi. NEC watachagua siku nyingine ya kati ya Jumatatu hadi Alhamisi ili kudai imezingatia malalamiko hayo!


  4) Madai ya wanafunzi wa vyuo vikuu kutOshiriki chaguzi hii nayo yatatumika na NEC kama sababu nyingine sindikizi katika kuahirisha uchaguzi huu.

  Zote hizi ni njama za NEC na CCM katika kutuchaguliwa viongozi ambao hatuwataki kabisa...............................CHAGUA DR. SLAA..CHAGUA CHADEMA......KUJIHAKIKISHIA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.............
   
 2. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tusubiri tuone
   
 3. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #3
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 1,979
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Bwana Public Policy Analyst nadhani sasa kuna umuhimu wa hard news kuliko hizi tetesi na uvumi.Downside ya tetesi/uvumi ambao haujathibitishwa ni kuwakatisha tamaa baadhi ya wananchi wanaoamini kuwa Dkt Slaa ndio ufumbuzi wa matatizo.Nasema hivyo kwa sababu baadhi ya wapigakura (wanaomsapoti Dkt Slaa) wanaweza kupata picha kuwa hata wakipiga kura bado JK ataendelea kuwa rais.

  I'm not against kuibua hujuma dhidi ya Chadema lakini wasiwasi wangu ni kuwa alarmist stories (nyngine zikiwa ni mawazo binafsi tu) zinaweza kuathiri ushindi wa DokTA Slaa.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 11,314
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Sababu kamilifu ya kujastify huu uamuzi hawana. Anyways bado ni uvumi tu. Hapa mafisadi wakubali matokeo tu!
   
 5. Mwanaukweli

  Mwanaukweli JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2010
  Joined: May 18, 2007
  Messages: 4,274
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  ngumu kuamini. tusubiri kuona.
   
 6. M

  Mundu JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hizi ni tetesi tu, hatuna haja ya kusadiki. Lakini hata uchaguzi ukiahirishwa kwa sababu hizo, au nyinginezo, haitabadili mawazo na mtizamo wa wapiga kura. Wapiga kura wengi, nikiwemo mie, mpaka sasa nimeshajua nani nampigia siku ya siku itakapofika. Kama kweli NEC na CCM wana mpango huo, wajue hauna athari zozote za kimatokeo ya uchaguzi ujao.
  Ni heri, uchaguzi ufanyike kama ulivyopangwa ili mambo mengine ya maendeleo (kama yapo) yafanyike.
   
 7. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,849
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Sasa ngoma imenoga!asiye na mwana,aeleke jiwe!
   
 8. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,535
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  Mimi sioni haja ya kuumiza vicha kwani TUNDUMA panaleweka jiografia yake ofisi za TRA zinafahamika zilipo, na bandari kavu ya tunduma inajulikana ilipo na mwisho kuna ndugu zetu, jamaa zetu na marafiki .busara itumike kwa wana jf wenye mawasiliano na hao niliotaja ili kupata uhakika kama kweli kuna gari la AZAM limekamatwa? hata muuza karanga anayefanya biashara maeneo hayo aulizwe swali moja kuwa;
  • EEEbwaaana e kuna gari lolote la AZAM liko kwenye yard ya TRA????? jibu tutapata na itakuwa mwisho wa mjadara.
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,906
  Likes Received: 231
  Trophy Points: 160
  Too much complain......
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 9,780
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Kikwete ni mtu wa kijiweni. Mtu wa fitna. Mtu wa Pwani. Mtu wa taarabu.

  Yeye hata masuala yanayogusa maslahi ya nchi hucheke-cheka tu.

  Amini usiamini. Hizi habari lazima ni za kweli.
   
 11. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #11
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,278
  Likes Received: 1,670
  Trophy Points: 280
  kwanini unaamini ni njama za sisiemu kushinda kwa kusogeza muda wa uchaguzi???...HUONI HAPO NDIPO TUTAPOWAPIGA BAO MAANA HIZO MBINU NI SAWA NA KUAHIRISHA TUMBO LA KUHARA...LAZMA MUDA UTAPOFIKA UTAINGIA MSALANI TUU....NA MAUMIVU MAKALI YA TUMBO YATAKUWA YAKIKUSUMBUA MUDA WOTE UNAOSUBIRIA KWENDA MSALANI....
   
 12. F

  Froida JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,161
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Kama wanataka kujua wananchi tutafanyaje wakiarisha ni kiama na nchi itazizima unawafahamu watanzania wa leo au unakisia bora iwe tetesi
   
 13. DICTATOR

  DICTATOR JF-Expert Member

  #13
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safari hii hakuna kurudi nyuma, ni mbele kwenda mbele. hata wakiahirisha tumeshaamua nchi lazima iwe huru kutoka kwa mkoloni mamboleo. Don't give up, keep fighting tupo pamoja. Mapambano yanaendelea jamani hadi mwisho.
   
 14. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #14
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 38,499
  Likes Received: 3,374
  Trophy Points: 280
  Hizi ni tetesi tu hazina ukweli wowote!
   
 15. M

  MJM JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Jamaa kwa somo la utungaji haujambo. Unatumia historia kufahamu mustakabali wa leo! Mbona mwaka ule Watz wengi walikuwa hawajajiandikisha. Usiogope uchakachuzi wa CCM hizo ndizo kazi za awali kabisa za Dr. Silaa kukamata majizi yote ikiwemo ya kura. Unadhani zile scandals ambazo huwa zinafunuliwa na Chadema source zao haziwezi kunasa wezi wa kura????? waache wajidanganye
   
 16. C

  CAIN Member

  #16
  Oct 19, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kweli TOO MUCH COMPLAINS.

  Nafikiri hatuna haja ya kuingiwa na woga, si kila chama kina wakala wake? Tuache wafanye kazi yao halafu tuone nani ataingia ikulu hiyo Okt. 31

  Tusianze panga mipango ya kutafuta visingizio hapo baadae...
   
 17. K

  Kikwebo JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2010
  Joined: Aug 25, 2006
  Messages: 352
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Wewe jamaa unachuki sana. Haoo unaowaita waswahili ndio waliowakaribisha babu zenu huku mjini.
   
 18. N

  Nasolwa JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,785
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hizi zitabakia kuwa ni TETESI. Gazeti la Mwananchi la leo 19.10.2010 ukurasa wa 11 ikiwa ni siku 12 kabla ya uchaguzi mwenyekiti wa NEC jaji Makame anawahimiza watu waende kwenye vituo walikojiandikisha kupiga kura wakakague majina yao.
   
 19. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 10,357
  Likes Received: 1,309
  Trophy Points: 280
  hahahahaha... :whistle: VUMBI...

  mtaongea mengiiiii.. ushindi 100% guaranteed, JK anarudi ikulu
   
 20. S

  SUWI JF-Expert Member

  #20
  Oct 19, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 550
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Chochote watakachojaribu kufanya NEC/CCM watanzania watahoji maana watz wa leo sio wa mwaka 1995.

  Jana baada ya kazi jioni nikiwa kwenye daladala la masaki ilikuwa hivi... Baada ya kufika kituo cha container kwa mbele kidogo akawa amesimama mama aliyekuwa amevalia t-shirt ya CCM, kanga. Alionekama kujichubua hivi.. gari lilikuwa full ikabidi asimame tena karibu na mlangoni. Kijana mmoja liyeniambia kuwa ni mwanachuo (mlimani) akamwita "mama mama eh njoo ukae hapa maana unaonekana mchovu" mama pasipo kujua lengo la kijana akasema "hapana kaa tu ndo kwanza notoka nyumbani naelekea kwenye kikao"

  Basi hapo akawa kama amewasha moto wa vifuu... mama alishambuliwa kwa maneno si wazee si vijana mara ohh nyie wezi vikao vya usiku mnapanga jinsi ya kuiba kura eh (ilikuwa mida ya saa moja jioni), mwingine hivi we mama CCM unaipendea nini ama ni hiyo t'shrt mbof inakuwehusha...

  Yote tisa, kumi akawa yupo mpiga debe (nadhani ni teja the way alivyokuwa anaongea) alikuwa anampayukia yule mama mdomoni "Slaa anatisha kama njaa" akawa anarudi kama wimbo flani hivi... nilicheka sana ila pia nilifurahi si kwa mama kupigiwa kelele na abiria ila kwa kugundua watu wana ufaham na mwamko mkubwa.

  Thats why ccm itabidi wafanye mbinu zozote chafu ili wabaki madarakani. vinginevyo ni ndoto kushinda kihalali..... ILA WATASHINDWA KWA UWEZO WA MUNGU.
   
Loading...