UVCCM watangaza vita na BAVICHA (Arusha)

UVCCM watangaza vita na BAVICHA (Arusha)

...you mean 9,000 sleeping youths ... in Arusha? not very true, mere propaganda
Don't underestimate these people(UVCCM-Arusha).....Unajua idadi ya kambi za majeshi zilizomo na zinazozunguka mkoa wa Arusha pamoja na askari waliomo kwenye kambi hizo!?
 
UVCCM wamenogesha game maana sasa hivi tukiandamana hatutaenda polisi tutawatafuta......eti vijana zaidi ya 9000 hapa Arusha...hatakama watakuja pomoja na Askari hawatafikia idadi hiyo na si sila askari yuko upande wao...
 
hata hivyo wametujulisha kwamba wapo ili tujiandae kikamilifu siyo kwa mabomu ya macho tu....
 
CCM haijafunga ndoa na Tanzania, tafadhali wanaCCM kama wananchi wamewakataa/wamewachoka msijinganganize kwao
 
Kama vile nchi inaelekea mrama hivi...sasa baada ya ile habari ya mabomu dodoma,na vurugu dar yote khs katiba.imefuatia hii kutoka arusha uv-ccm arusha wanasema wana vijana zaidi ya 9,000 tayari kupambana na cdm,ili kuwazuia wasiandamane kupinga meya ars,source chanel ten habari saa moja jioni hii.
Na tegeta nako waua mabaunsa watano,kisa kuzuia ubomoaji makazi...kulikoni.......???

haya yote yanatendeka wakati mtu anayeitwa rais anakula urojo na juisi za miwa zanzibar
 
Kama vile nchi inaelekea mrama hivi...sasa baada ya ile habari ya mabomu dodoma,na vurugu dar yote khs katiba.imefuatia hii kutoka arusha uv-ccm arusha wanasema wana vijana zaidi ya 9,000 tayari kupambana na cdm,ili kuwazuia wasiandamane kupinga meya ars,source chanel ten habari saa moja jioni hii.
Na tegeta nako waua mabaunsa watano,kisa kuzuia ubomoaji makazi...kulikoni.......???

naona kama waongea kishabiki zaidi.nchi gani inaenda mrama kwa kulipuliwa vibomu vya machozi?waganda wasemaje na konyi wao.
Si mnawashwa vita bac tusubiri hiyo tarehe tutawaona kwanza kwa wengine mtasaidia kutuchangamsha taarifa ya habari,maana siku hizi inaboa sana.
 
hakika nchi yetu inaelekea pabaya ccm mnaitumbukiza kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa ajili ya maslahi yenu binafsi. Vijana wa ccm wametangaza vita dhidi ya cdm tunawaambia huo mziki wanaoutaka
wasije wakashindwa kuucheza .tunawaambia bora kufa katika fikra hai kuliko kuishi katika fikra mfu. Haki ya mtu haiombwi bali inatafutwa kwa njia yeyote ile hata kama ni kwa vita mliotangaza tunawasubiri
 
Baada ya kuangalia taarifa ya habari ya itv jana, nimegundua kuwa uvccm Arusha wamechanganyikiwa na siku 21 walizopewa na cdm. Mjumbe wa h/kuu ya taifa na katibu wa vjana amesema kwamba wamejipana kupambana na maandamano yasiokuwa na ukomo yatakayotangazwa na cdm ikiwa uchaguzi wa meya hautarudiwa. Wamesema wana vijana zaidi ya elfu 9 na wamejipanga kupambana na hawatakubali kushindwa! Wakati huohuo vjana kutoka kata ya ungalimitedi wamewaomba kuhudhuria vikao vya madiwani hapa manispaa walivyosusia ili kuleta maendeleo. Ukiwaona kwenye mikutano hii miwili utajiuliza mbona wanaomba na huku wanatisha? Huku sio kuchanganyikiwa? Mbona ni wachache na wanadai wapo elfu 9? Wanapatawapi hii jeuri wakati wanafahamu uchache wao hapa Arusha?
Nawasilisha
 
Wanashindwa kupambana na ufisadi ndani ya chama chao wanatoa matamko kama haya,honestly in a country like Tanzania where myriad problems comfront the nation,having a useless club/association like UVCCM,it's a mistake.Did they check the credentials of the youth associations/individuals that make up the coalition before declaring war against Bavicha Arusha?


UVCCM kimekuwa kikundo cha kutanga za vita na kutoa matamko tu... They have lost credibility na hawana tena dira

sasa hapa sijui nani atakua anavunja amani UVCCM au wakazi wa arusha wanaotaka haki
 
TANZANIA TUJIANDAE KUWAZIKA WENGI WA WAZEE WETU WAKIWA NA DONGE SUGU MOYONI SHAURI YA MADUDU YA KILA LEO CCM, NA KWINGINEKO KUWAPAMBA MAJAMBAZI KAMA VILE NDIO MASHUJAA HALISI WA KIZAZI CHETU

NI UCHUNGU KUSEMA LAKINI NDIO UKWELI WA MAMBO KWAMBA HAYA MAJUTO YOOOTE YOOTE TUNAYOISHI LEO NI SHAURI TU YA UKWELI KWAMBA WATU TUMEAMUA KWA DHATI KUABUDHU FEDHA ZA WATU AMBAPO MASLAHI BINAFSI HUKIRIMIWA ZAIDI NA MASLAHI JAMII HUKEJELIWA NA KWAMBA TUMEAMUA KUWATENGA WAZEE WENYE HEKIMA NA HESHIMA ZAO KATIKA NCHI HII NA SISI KUJITIA SIKIO KUZIDI KICHWA VILE
.


Ni kutoka na yale yanayoendele kushuhudiwa kwa mtindo tofauti kabisa leo hii na kusababisha miguno isioisha katikati yetu. Wengine leo hii huhoji mtu kama Tambwe Hiza auPrince Bagenda kutumwa na CCM kwenye masuala muhimu saaana kama katiba inaleta maana gani.

Jamani wenzangu mimi nasema mbona kama vile hatuelewani hapa; CCM hivi sasa hakuna hata mtu mwenye akili zake timamu na pia heshima zake timilifu ambaye yuko tayari kujitokeza hadharani mbele ya Watanzania kukitete wala kubainika wazi wazi kuwa ndio TRUE FACE OF THE PRESENT TIME CCM.

Kutokana ukweli huo ndio maana karibu kwa kila tukio jipya watu tunajikuta tukiwa tunagongana ukumbini au kwenye televisheni na sura ambayo kama ni enzi za CCM chini ya Mwalimu Nyerere basi ni kweli kabisa kwamba wao wenyewe, kwa KWA MTAJI WA HISTORIA WENYE MASWALI MENGI SANA TUNAVYOWAFAMU katika jamii yetu hii, wangejionea aibu kubwa hata kudiriki kujongea meza kuu kwa madai ya kuwiwa kukiwakilisha maoni ya kutegemeka.

Lakini siku hizi Chama kile Cha Mwalimu chenye heshima kedekede mbele ya macho ya wazazi wetu enzi hizo leo hii ni jambo la kawaida kabisa LINJEMBA LOLOTE LILILOTOKA KUSIKOJULIKANA, eti kwa sababu tu ni RUGARUGA liaskari la kukodisha basi linajitokeza tu mbele bila hata KUJIHOJI KWANZA NA HATA KUJIKANA NAFSI YAKE kama kweli jamii itamvumilia awapo pale mbele!!!!!!!!

Nasema ni huruma sana kuona mara leo TAMBWE HIZA na hapo kesho PRINCE BAGENDA wakati CREAM YA CHAMA HICHO TUNAOWAJUA LAKINI HAWATAKIWI KWA KUWA HAWABURUZIKI bado wangali hai ndani ya nchi hii!!!

Jamani naongeza hiviiiiiii, mtu ukijiweka katika viatu vya wazee hawa wa CCM na kuanza kujenga picha akilini kwamba pengine enzi hizo ambapo Mzee Sinde Warioba alikuwa akitumikia uchipukizi ama ndani ya TANU au CCM na vituko anavyolazimika kuviona leo kwa kuwa hajarudi kwa muumba wake; wanavyojihisi hivi sasa akina Mzee Kisumo, Arkado Ntagazwa, Mama Getrude Mongela, na wengine enzi zao walipokua CCM kama vile Mzee Edwin Mtei, Prof Lipumba, Dr Slaa, Mutamwega, Mziray, Prof Luhanga, ...

... leo hii ingalikua ni kwamba watu tungalikua na uwezo wa ki-Mungu na kumuona kila mmoja kila mahali wakati wote basi mjue ya kwamba wazee hawa na wengine wengi zaidi humwaga nyongo karibu kila siku kwa hasira majumbani kwao kali siku waonapo MADUDU YANAYOFANYIKA NDANI ya chama walichokitumikia kwa karibu maisha yao yote!!!!!!!!!!!!!!!!! Hebu jiulize ni nani mwenye akili zake timamu ambaye angependa akatumie mikono yake mwenyewe kubomoa nyumba zuri aliyotumikia miaka mingi kukijenga?????????

Je, unafikiri sisi vijitoto vya leo (UVCCM) ambao kwa uchanga wetu hata midomo bado inanuka maziwa ya mama zetu tuwapendao, pindi tunapojitokeza tu na kujitangazia mambo ovyo ovyo tu kwenye vyombo vya habari mara leo tunapendekeza afukuzwe uanachama mzee huyu (lakini si kufanya hivyo kwa mafisadi), mara yule tumemrushia tusi na huyu huku tumemuondoa ukamanda; basi ni vurugu tuuuuuuu bila hata kuweka kwenye mizania viwango vyetu vya uwekezaji wa nguvu, akili, fedha na muda katika uhai wa chama husika!!!!!!!!!!!!!!!!

Pindi uonapo watu katika kijiji fulani huonelea kwamba ni aheri kutia kiberiti nyumba yao, hata kama ni wa kuezekwa kwa majani tu, ili ikaungue na kuteketea kabisa KUSUDI KIJIJI KIZIMA KIWEZE KUWA SALAMA TENA, basi mtu usisubiri kukumbushwa kwamba kuna hatari kubwa saaannnaaa iliotamalaki kila kona ya nyumba hiyo.

Kwa wale ambao huenda wamechelewa kung'amua hili naomba niwapashe habari niyoweze tu kupata kwa kuangalia, kupima na kulinganisha mambo ya CCMyalivyo hivi sasa, nasema KUNA JOKA KUBWA, YENYE GAMBA SUGU, NA LENYE SUMU KALI NA HATARI zaidi ndani ya nyumba ya CCM - juhudi za kuweza kulitoa joka hili ili nyumba iwe salama kuishi watu tena, busara zinatuelekeza kwamba ni mara mia watu tukajenga nyumba nyingine katika eneo salama zaidi ili hata mayai ya nyo huyu yasitukaribie katu!!!!

Lakini tusisahau kamwe sisi vijana kuwatafuta wazee wa kutumainika ili wakatupemwongozo wao kwa upendo kabisa kwamba kizazi hiki tukafanye nini ili kujikinga mi-joka vamizi siku za usoni ili nyumba zetu za sasa tunazojenga ziendelee kuwa salama zaidi miaka yote bila kulazimika tena kujichomea nyumba tunayojijengea sisi wenyewe leo na kesho.

Endapo tutaharakisha kidogo katika hili na ba Watanza mijini na vijijini, Bara na Visiwani, wake kwa waume, wasomi kwa akina kabwela; wao watapata sababu zuri ya kuwaaminisha kwa kwa HAIKO JIRANI KUTAWALIWA NA MIJIBWA - na ndio maana kila siku natumia muda wangu mimi kuandika humu kama sehemu ya mchango wangu kuhakikisha kwamba Tanzania ya NEVER GOES TO THE DOGS ambao hivi sasa wakichukua Mateka Chama Cha Mapinduzi ya enzi zile na kukibadilisha kabisa sura, dira na jalada zima.

Sote tunalo jukumu katika hili la kuzuia nchi kutokwenda kwa mijibwa: na njia pekee na ya uhakika kufanya hivyo ni KUTETEA KWA GHARAMA YOYOTE ILE swala zima la Mchakato wa kuunda Katiba Mpya ya nchi chini ya mamlaka kamili na thabiti ya Umma wa Tanzania kujiamulia hatima yetu. Na kila siku hakikisha umeelimisha japo watu 3 tu juu ya jambo hili la msingi linalozidi kwa mbali tofauti zeti za kiitikadi nchini.

Toa mchango wako katika hili tangu sasa na kuendelea!!!
ndugu yangu uwezo tunao... huna haja ya kuweka post hii kwenye kila thread.... kila mtu ana uchungu na nchi yake lakini si lazima kujaza the asme post everywhere
 
Kama vile nchi inaelekea mrama hivi...sasa baada ya ile habari ya mabomu Dodoma,na vurugu Dar yote kuhusu katiba, imefuatia hii kutoka Arusha UV-CCM Arusha wanasema wana vijana zaidi ya 9,000 tayari kupambana na CDM,ili kuwazuia wasiandamane kupinga Meya Arusha. Source Chanel ten habari ya saa moja jioni hii.
Na Tegeta nako waua mabaunsa watano,kisa kuzuia ubomoaji makazi...kulikoni.......???

Hivi nchi hii hakuna serikali???? JK yuko wapi kalala au?? maana hawa uvccm wanachofanya ni ugaidi ndani ya nchi yenye serikali
 
Don't underestimate these people(UVCCM-Arusha).....Unajua idadi ya kambi za majeshi zilizomo na zinazozunguka mkoa wa Arusha pamoja na askari waliomo kwenye kambi hizo!?

mkuu ...katika wanyonge wakubwa hapa tanzania na wasio support serikali underground ni pamoja na wanajeshi na askari wa kawaida .... data zako haziko makini
 
Wanajua wako wengi maana na polisi wote si ni UVCCM au CCM......
 
Wanajua wako wengi maana na polisi wote si ni UVCCM au CCM......

hata ukiangalia waliokuwa kwenye mkutano ungaltd ni kama 10 hivi. Na hao waliokuwa kwenye mkutano wa mkoa hawafiki 15! Ndio maana najiuliza wametoa wapi hiyo jeuri? Maana hata ukijumlisha na askari waliopo hapa hawafiki 9elfu. Au wanajumlisha na jwtz?
 
hata ukiangalia waliokuwa kwenye mkutano ungaltd ni kama 10 hivi. Na hao waliokuwa kwenye mkutano wa mkoa hawafiki 15! Ndio maana najiuliza wametoa wapi hiyo jeuri? Maana hata ukijumlisha na askari waliopo hapa hawafiki 9elfu. Au wanajumlisha na jwtz?

na Chuo cha Polisi Moshi
 
Hapo sawa, sasa twende kwenye field tuone. Halafu refa awe mzuri.😛anda:
 
kama wazee wao wamechanganyikiwa wao watashindwaje kuchanganyikiwa...hahaaaa Chichiemu bana
 
Back
Top Bottom