UVCCM: Usalama wa taifa haumsaidii rais, unavuruga nchi kwa maslahi yake

Kikwete hakuwahi kuhojiwa na wananchi kabla ya kupata kazi aliyo nayo. Mwaka 2005 hakukuwa na mdahalo, na mwaka 2010 pia hakukuwa na mdahalo. Kwa hiyo alipewa kazi kazi bila intavyuu, na sasa ni wazi kuwa alipewa kazi asiyoijua na asiyoiweza.
 


Yaani umelenga baadhi ya mambo kwa undani na uzuri sana na hata hili la kuchomolewa hoja yako uliyoiweka humu jamvini lina ukweli mkubwa hawa jamaa wana mkono humu tena mkubwa
na wa kutosha na kama huamini jidai unaishupalia hii idara utona jinsi mada hiyo itakavyotupwa kapuni anyway tuyaache hayo maana njaa zetu ni mbaya sana ila ukweli umewekwa wazi na wachangiaji kwa kiwango kikubwa sana na Arafat, na kwa undani Dk. Slaa baadhi kashfa ameziweka humu ndani na kuna nyingine nyingi kiasi ambacho ukiziorodhesha hapa utaona hili dude ni janga la kitaifa na ni chombo maalum ambacho mafisadi walioko madarakani wamewaweka viongozi wakuu wa idara na wengine kibao kwa masilahi yao na hivyo rais hafurukuti na hana maamuzi na kama akipishana nao kidogo na viongozi wa idara hii au kuwachukulia hatua mafisadi maisha yake yanakuwa hatarini maana sehemu zote ameshikwa pabaya.
 
Hivi tiss ni nini hasa kwa tz? Maana walianza kulala tokea enzi za mkapa kny nbc na nmb.
 
UVCCM wanakuwa waropokaji,these guys are lazy in the head,they cant even think of creative solutions to solve Youth problems. I feel they sometimes speak from a perspective of what they personally wish to happen rather than allow the wing be informed as to what is most likely to happen based on what is actually on the ground.

Uchaguzi wao 2012 watajikuta wamebakia na options za candidates ambao ni pro-
CHADEMA covertly.Hii ni strategy ya divide them from within.Yes i said tunaweza kuwafanyia hivi

They failed to understand the system and National agenda on vital issues.
The success of government depends on the level of creativity, dynamism and coherence in T
azania. The government is an innocent mirror of the collective consciousness of the nation. If Tanzaniais not strong and integrated, no government policy, no matter how wise or how well conceived, will be able to generate progress and success. When collective consciousness is coherent and awake in Tanzania, the life of the nation grows to be in tune with Natural Law. Until now, this important element has been missing from the functioning of government in Tanzania and as a result, the government has continued to be beset by problems. This is why governments have continued to perform with lack of efficiency and effectiveness and have not succeeded in fulfilling their responsibilities to the nation and not the fallout or weakness of TISS. UVCCM ni desperate Entity with immaturity .

Ngoja Tuchukue uongozi wa BAVICHA tuwafundishe kazi !!!We are going to establish a credible entity and Management style of Leadership with perfect managers that discharges the job descriptions perfectly,we believe Bad leadership causes bad followership! UVCCM watch our steps!!



 
UVCCm wanatumwa kusambaratisha chama chao,wanajitahidi kutoa umma kwenye agenda za kitaifa na wanalengo la kiini macho kuwazuga vijana nadhani uongozi wa UVCCm kama ulivyo kwa sasa hauna agenda zaidi ya kusimamia maslahi ya Jakaya Kikwete,wamekosa heshima kwa viongozi wengine wa CCM huo si mwenendo mzuri hata kama ningependa CCM ijizike
 
Wakati TISS walipoingiza kontena la kura kule Tunduma mbaona UVCCM hawakuona wanavuruga nchi?
ukiangalia matokea ya uchaguzi wa mwaka 2010 haiingii akilini kwamba TISS waliingiza makonteina ya kuchakachua kura. Binafsi naona Rais asingepata asilimia 61 kama tulivyoshuhudia. Hizi ni propaganda za kisiasa za kulikuza jambo hili ingawa mtazamo wangu haondoi ukweli kwamba hakuna uchaguzi unaoweza kukosa malalamiko.
 
mimi nadhani vijana wa CCM kuna kitu cha kuwafanya wawe machizi wamelishwa kwanini uwezo wao wa kufikiri ni mdogo kiasi hiki?
 

Tunaposema Mkwere ni kukuza ukabila usiokuwa wa lazima. Tukianza leo kuwabatiza viongozi wetu majina yao kugeuka ya kabila lao kwa mfano kusema yule Mchaga kwa Mbowe, Mbulu kwa Dr Slaa, Mnyamwezi kwa Lipumba, Mzanaki kwa Nyerere, Mmakua kwa Mkapa, Muunguja kwa Mwinyi, hakika tunalipelekea taifa pabaya. Kila jambo baya huanza taratibu na baadaye kuwa janga la kitaifa.
 
Kama nimemwelewa vizuri mtoa hoja alitaka tumsaidie kuthibitisha kama kweli UVCCM walizungumzia kuwa TISS hamsaidii Rais na ndio mada yenyewe, kwa maana hata yeye hakutaka kwenda kwa ndani hana uhakika lakini jambo la ajabu kabisa sisi sote tumeshindwa kuthibitisha na mara moja tumejikuta tunachangia kwa ushabiki zaidi.
 

Hakuna Rais aliyewahi kutoa hotuba kwa vipindi viwili vya utawala wake hapa duniani au kwa miaka kumi hapa Tanzania na hotuba zake zote zikapendwa na wananchi wote. Ni haki yako kuona kwamba Rais hakuongea kitu cha maana lakini pia uwape haki hiyo hiyo watanzania wenzako wanaoona kwamba hotuba ya Rais haikuwa na kasoro kubwa kiasi cha kuibeza kabisa kabisa.
 
Maudhui ya taarifa hii ni kama imetoka kwa mwanachadema ambaye alikaa pamoja na Dr Slaa wakipata bia ndipo stori za TISS na UVCCM zikajitokeza. Dr Slaa aliota CCM muda wote lakini hii isitufanye wote tukashindwa kuchambua ukweli wa thread za kichochezi kama hii. TISS inaweza kuwa na mapungufu kama ilivyo kwa taasisi zingine zote lakini tuitendee haki penye kuhitajika haki.
 

Lakini hawa vijana wanataka TISS ndiyo wawe wanasema kwenye media? Je wanataka TISS iwaambie inamsaidia vipi rais?
 
Mkuu Saigon, avatar yako imetulia sana, kipindi hiki cha kasi zaidi...teh..teh..teh....
 

Kuna kipindi chadema ya Mbowe na Mtei walikuwa wanalalamika chama hicho kuhusishwa na wachaga leo tena CCM ya Kikwete inahusishwa na wakwere.... Ni yale yale ya kuleta ukabila kwenye siasa.
 

Hizi ni siasa za kale zilizojaa ukongwe. Tumekuwa tunasisitiza mara kadhaa TISS isijihusishe na siasa wala chama fulani cha siasa. TISS inaishauri serikali sio chama cha siasa au UVCCM kama hili lilijitokeza katika vikao hivyo ni makosa. TISS ni above UVCCM... TISS haipo kushawishi chama fulani kushinda ni makosa kuiingiza TISS katika mjadala wa kushinda au kushindwa kwa CCM katika uchaguzi uliopita.

TISS ibaki na kazi yake ya kushauri tu yanayotokea katika uwanja wa siasa ni ya wanasiasa wenyewe..... TISS iwajibike kwenye uwanja wa usalama wa nchi.
 
Tatizo hapa JF mkwere linatumika kama jina la kumdhihaki Rais. Tuheshimu makabila ya watu.

Wewe ndio Salva Rweyemamu? hebu tuondolee kiwingu, huna uwezo na hautokuwa nao wa kutufundisha sisi tumuite kwa jina lipi Mkwere, kama inakukera nakushauri nenda kapoteze muda wako kwenye website ya ccm uangalie miradi ya chama, huko utakutana na taarifa ambazo unapenda kuzisikia, hapa umepotea njia, hatupo hapa kumpaka mafuta Mkwere wakati ndugu zetu wanakufa njaa kwa kukosa milo mitatu.
 
Hao UVCCM ina maana walikuwa hawajui kuwa TISS imegeuka taasisi ya ccm kama uwt, uvccm na umoja wa wazazi?TISS ni kama green guard kazi yao kulinda maslahi ya ccm?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…